Msichana wa zamani anahitaji nimchangie anunue iPhone 6

msomso

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
464
Reaction score
152
Ndugu wanajamvi ,

Mimi ni mfanyakazi katika mkoa wa Shinyanga but sasahivi nipo masomoni Dar es salaam ilikuwa wiki iliyopita my X wangu akanipigia simu anaomba nimuongeze pesa anunue simu nilimkubalia kishingo upande nikamwambia anicheki kuanzia Tarehe 1.2.3 mwezi wa pili.

Yeye ni mwalimu yeye akadai kuwa si Tarehe 24 mshahara utatoka kwa hiyo takutumia pesa uninunulie na wewe utanichangia kidogo nikasema poa ila subiri tarehe 1au 2 mwezi ujao jamani ikafika Tarehe 24 nikaona nimuambie anitumie ile pesa yake nimnunulie akatuma laki moja nilipokumbuka aliyonifanyia mpaka tukaachana usaliti nimeamua Kuila hiyo pesa amenipigia simu jana nimemuambia simu imeibiwa hostel. Je nimefanya kosa?
 
#mtemkwa#nilikuwa nakula pensheni yangu yeye amekula pesa zangu zaidi ya hiyo
 
Anataka Iphone 6 alafu anakutumia laki moja? Hujui hata kudanganya... Na siyo kwamba umekula kusudi hiyo hela, unanjaa huna kitu, umeshukuru hata kuipata hiyo hela... Mwambie ukweli tu kama umepigika na hiyo pesa imekuwa msaada kwako ukipata utamlipa atakuelewa..
 
Unasoma chuo hata kuandika hujui... Hili jambazi la namna gani.
 
Yaaani ni kazi alafu mchango wake laki moja nimeila
 
Mwongo huyo kwanza alishamwambia asubiri kuanzia tareh 1,2,3 zimefika hivi?!

Mfanyakazi gani maskini huyo?
 
Sasa mkuu kwani alikutapeli au kukuibia pesa? Si alikusaliti sasa unalipiza kwa kumtapeli sio sawa. Mrudishie hiyo laki na umuambie huwezi kumuongezea.
 
Umri wako tafadhali.
 
Mrudishie "My X girl wako(wangu)" hela yake acha kuendekeza njaa..
 
Umli wangu ni miaka 27 wakuu naomba maoni yenu niamue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…