Msichana Zeruzeru Aliyeongoza Katika Mtihani Wa Darasa La Nane najua Kujieleza Kweli

Msichana Zeruzeru Aliyeongoza Katika Mtihani Wa Darasa La Nane najua Kujieleza Kweli

Ni kweli ila huyo mtoto hajali kabisa au hajui jana ktk mahijiano na BBC idhaa ya kiswahili alijiita hivyo.
Wabongo ndo zao izo...zeruzeru ni neno fasaha la kiswahili na albino ni kizungu...sasa ukimuita albino ama zeruzeru wanakuona unanyanyapaa kumbe umetumia lugha fasaha kabisa...eti wanataka uite mlemavu wa ngozi...
Ni kama ukisema KIPOFU wanakuona mnyanyapaa eti useme mlemavu wa macho!
Inakera
 
Umeukimbi Uzi wako mwenye unakuja kudandia Uzi mwimgine, huu ni ubaguzi kama ulivyo ubaguzi wa kikabila. Sasa na huyu msichamanataka ajulikane kwa ualbino wake badala ya jina lake au utu wake. Sijaona hata mtu mmoja anataja jina lake kwanza kabla ya ugonjwa wake wa ngozi.

Hakuna jipya katika kuongoza mtihani wa KCPE. Wengi wameongoza. Kinachofurahisha wengi wetu kwa ualbino wake ni kuwa jinsi anavyozidi kudhihirisha uerevu wake, ndivyo watu wanazidi kuona kwamba kuwa albino si eti wewe umelaaniwa. Albino wengi watoto wanaona hata wao ni watu kama wengine. Mwenyewe amesema kuwa kilichompa motisha zaidi ni kujua kuwa kuna Jaji wa mahakama ambaye ako kama yeye tu. Mzazi yeyote aliye na mtoto kama yeye itabidi atie bidi akijua kuwa mtoto wake si mjinga kwa ulemavu wake.
 
Tupia hapa hiyo historia watu wasome. Asante
Neno Albino linamaanisha
mtu mweupe, linatokana na
neno la lugha ya Kilatini -
albus-linamaanisha “eupe”.
Kuanzia karne ya 17 neno
Albino limekuwa likitumika
katika kueleza hali ya kundi
la viumbe hai (watu, wanyama
na hata mimea) ambao wana
upungufu au ukosefu wa rangi
katika ngozi, macho na nywele.
Kwa binadamu ni bora kutumia
maneno “Watu wanaoishi na
ualbino
kwani itamaanisha kuwa ni watu kama wengine ila wanaishi na
hali tofauti ya “ualbino”. Katika kitabu hiki maneno haya mawili
yatatumika.
Lugha inajenga dhana na kuunda hali ya ukweli / uhalisi. Kwa
sababu hiyo ni lazima tuache kutumia maneno kama “zeruzeru”.
Neno hili linamaanisha sifuri mara mbili au mtu asiye na
thamani. Utumiaji wa neno hili ni dharau ya utu na kulaumu
watu wanaoishi na ualbino kama kosa lao.

https://www.google.com/url?sa=t&sou...6CHUQFgguMAM&usg=AOvVaw2gawb7eOct8MaSRVz6u-B_
 
Hata hivyo wao wenyewe na jamii yao hawapendi kuitwa hivyo,ni sawa kumwita mtu ana marienge, atapenda kuitwa mlemavu wa macho kuliko 'mwenye marienge'.
 
Wabongo ndo zao izo...zeruzeru ni neno fasaha la kiswahili na albino ni kizungu...sasa ukimuita albino ama zeruzeru wanakuona unanyanyapaa kumbe umetumia lugha fasaha kabisa...eti wanataka uite mlemavu wa ngozi...
Ni kama ukisema KIPOFU wanakuona mnyanyapaa eti useme mlemavu wa macho!
Inakera
Umesema ukweli. Unyanyapaa unatokana na yale unayoyawaza moyoni na unayoyatenda. Kile wanachotaka hawa wanaharakati ni kufanya kila mtu awe guilt conscious kila mara.
 
Hebu tuwekee aliyeongoza form four hapa kwetu Bongo tusikie yai lake
 
Makeup ya ngozi yake ni utambulisho wa kipekee ambao naamini hata yeye anajivunia.

Kwa wasiojitambua ndio hujikataa
Sina imani kama angependa ajulikane kama mlemavu wa ngizo zaidi ya utu wake au jina lake. Kama alama ya mwili ndio utambulisho mtu, kwanini makabila yanayo chanja chale usoni huyatambuwi kwa chale zao?
 
Hakuna jipya katika kuongoza mtihani wa KCPE. Wengi wameongoza. Kinachofurahisha wengi wetu kwa ualbino wake ni kuwa jinsi anavyozidi kudhihirisha uerevu wake, ndivyo watu wanazidi kuona kwamba kuwa albino si eti wewe umelaaniwa. Albino wengi watoto wanaona hata wao ni watu kama wengine. Mwenyewe amesema kuwa kilichompa motisha zaidi ni kujua kuwa kuna Jaji wa mahakama ambaye ako kama yeye tu. Mzazi yeyote aliye na mtoto kama yeye itabidi atie bidi akijua kuwa mtoto wake si mjinga kwa ulemavu wake.
Vyombo vya habari vya Kenya ndio mitindo yao wakikosa cha kuandika. Wanatafuta hata ambacho sio cha kuandikwa na kukikuza mpaka basi e.g. Githeri man. Kilicho mfanya huyo binti kufaulu mtihani ni akili yake na sio matatizo anayo yapitia kijamii. Ngozi yake haikutakiwa kuwa issue lakini vyombo ya habari wako busy kufukia ya uchaguzi kwa habari kama hiyo. Huyo binti amejitahidi kufaulu mtiani kwa nguvu yake mwenyewe na sio NGOZI yake. Hata cheti chake cha kuzaliwa hakiandikiwi kama albino bali mtoto wa kike.
 
Umeukimbi Uzi wako mwenye unakuja kudandia Uzi mwimgine, huu ni ubaguzi kama ulivyo ubaguzi wa kikabila. Sasa na huyu msichamanataka ajulikane kwa ualbino wake badala ya jina lake au utu wake. Sijaona hata mtu mmoja anataja jina lake kwanza kabla ya ugonjwa wake wa ngozi.

Wacha povu, hizi taarifa utazidi kuziona mpaka basi.
 
Ubaguzi ,,,kwann usingesema tu msichana ,,kwan uzeruzeru ni utofauti ???
 
Sina imani kama angependa ajulikane kama mlemavu wa ngizo zaidi ya utu wake au jina lake. Kama alama ya mwili ndio utambulisho mtu, kwanini makabila yanayo chanja chale usoni huyatambuwi kwa chale zao?
Jina ni utambulisho binafsi tu!
Don't be emotional.

Shusha pumzi kisha tamka zeruzeru, means "Eupe eupe"

Kumbuka neno hili linatokana na Blackman perception.
 
Neno Albino linamaanisha
mtu mweupe, linatokana na
neno la lugha ya Kilatini -
albus-linamaanisha “eupe”.
Kuanzia karne ya 17 neno
Albino limekuwa likitumika
katika kueleza hali ya kundi
la viumbe hai (watu, wanyama
na hata mimea) ambao wana
upungufu au ukosefu wa rangi
katika ngozi, macho na nywele.
Kwa binadamu ni bora kutumia
maneno “Watu wanaoishi na
ualbino
kwani itamaanisha kuwa ni watu kama wengine ila wanaishi na
hali tofauti ya “ualbino”. Katika kitabu hiki maneno haya mawili
yatatumika.
Lugha inajenga dhana na kuunda hali ya ukweli / uhalisi. Kwa
sababu hiyo ni lazima tuache kutumia maneno kama “zeruzeru”.
Neno hili linamaanisha sifuri mara mbili au mtu asiye na
thamani. Utumiaji wa neno hili ni dharau ya utu na kulaumu
watu wanaoishi na ualbino kama kosa lao.

https://www.google.com/url?sa=t&sou...6CHUQFgguMAM&usg=AOvVaw2gawb7eOct8MaSRVz6u-B_
Ni jina tu mkuu lina maana "eupe eupe" kwa kiafrika (kiblackman)
 
Jina ni utambulisho binafsi tu!
Don't be emotional.

Shusha pumzi kisha tamka zeruzeru, means "Eupe eupe"

Kumbuka neno hili linatokana na Blackman perception.
Kama utambulisho wa rangi ya ngozi ungekuwa sio tatizo basi watu wenye ngozi nyeusi wasingejisikiwa vibaya wanapotambukiwa kama N**ger. Au hata wachina wangefurahi watu wakiwaonyesha ishara ya maumbile ya macho yao. We need to be judged by our character not by the colour of our skin.
 
Back
Top Bottom