Msidanganyike na magari yao ya kifahari! Ata Matajiri na Mastar wana “Daily Drivers”!

Msidanganyike na magari yao ya kifahari! Ata Matajiri na Mastar wana “Daily Drivers”!

Mtazamo wangu naona ukiwa na magari mawili yaani moja la misele yako ya kilasiku na nyingine Kwaajili ya safari ndefu..hapa utafutahia Sana maisha
Mbona mimi nina magari matatu na naweza kusafiria lolote na ninapigia misele lolote? Ina maana siijoi maisha?
NB: Magari ya kawaida msianze kutoa mapovu.
 
RRONDO namuelewa sana tuu. Yote haya ni umasikini. Bongo 95% tunanunua magari used. Ila kila siku kulalamika na reliability! Ukweli ni kwamba hakuna gari isiyokuwa na fundi. Kuna jamaa yangu alikuwa na Range nzuri kweli kweli. alipokuwa na pesa alikuwa anafanya service kwa dealer. Pesa ilivyopotea akaanza kuipeleka mtaani kwa akina fundi Bakari. Ukimuuliza anakwambia fundi Bakari yupo pale pale kwa dealer kwa hiyo haina shida. Mzee kwani gari ilichukua round??? Kumbe Fundi Bakari wa kwa dealer na fundi Bakari wa mtaani ni watu wawili tofauti ingawa ni wamoja.

Bottomline: Tutatufe pesa tununue magari imara. Gari hata ukiwa nayo moja, ila jilipue (kama mfuko unaruhusu), ununue gari imara. Hata conversation na uchangiaji wetu kwenye hizi nyuzi za Mad Max utabadilika.
 
Mbona mimi nina magari matatu na naweza kusafiria lolote na ninapigia misele lolote? Ina maana siijoi maisha?
NB: Magari ya kawaida msianze kutoa mapovu.
Hahahaha 🤣 🤣 😂 😂 🤣 upo kwenye miongoni mwao wanaokula mema ya nchi.
Kwa hayo magari yote yanapata muda mrefu wa kuishi tofauti na Yule anapigisha gari moja hilohilo kuanzia mjini na safari ndefu mwaka mzima hapa gari hata iwe ngumu kiasi gani litachoka tu
 
Dah ivo vyuma aisee, naishiaga kuvitamani tu
Kuna kampuni ya wabongo wanamiliki mgodi wa makaa ya mawe Ludewa, wao gari za engineers na staff wengine wamewapa Ford Ranger XLT. Mgodi ulipo ni ndani ndani,barabara mbovu na wanaziburuza kweli wengine wanakuja nazo mpaka Dar. Ila gari ikifa bado wanarudi kununua Ford Ranger tena
 
Mad Max number plates za 3D zilipigwa marufuku? if yes, ni kwa nini? nikiweka kwenye gari TRA watadai chao au polisi watakamata gari?
Ile utasumbuana na matrafiki tu.

Wao walisema sio nzuri kiusalama. Hawakua na majibu straight ila kuna tetesi kua camera zao za kudai madeni hazirecord/hazinasi zile namba.

Sijui why, ila same gari ukiingia nayo Mlimani City unabyotoka zile mashine za parking zinasoma.
 
Nilivyokuwa mdogo, kama miaka 13-14, nilikuwa napenda kusoma vitabu vya baba yangu.

Alikuwa anapenda sana kusoma American business and advice books. Lee Iacocca, Harvey Mackay, Jack Welch, Norman Vincent Peale etc.

Nakumbuka kitabu kimoja cha Harvey Mackay kinaitwa "Swimming With The Sharks Without Being Eaten Alive" alitoa ushauri mmoja wa kunujua magari ya bei rahisi na nyumba za bei kubwa.

Alielezea kuwa magari ni liability, ukilinunua tu lina depreciate, lina ku cost.

Nyumba ni kitu kinacho appreciate.

Nikaushika ushauri huo mpaka leo, nanunua magari ya bei rahisi tu nimetoka kwenye BMW X3, nimeenda kwenye BMW X5.

Sitaki magari ya gharama kubwa kwa kufuata ushauri wa Harvey Mackay ninaoukumbuka tangu siku hizo.
Ndio maana mimi ndoto yangu ninunue kati ya ford ranger, amarok, hilux au fortuner au Prado. Naamini moja kati ya hizi gari ntazeeka nayo nikinunua.

Habari ya kununua migari mingi ya gharama tena kila toleo ni ulimbukeni tu.
 
Huu uzi muhimu sanaa!
Ndio maana jioni kuna barabara ukipita unakutana na vyuma vya moto watu wanaenda dinner au kwenye meetings flani ila mchana wako zao na gari za kawaida.
 
Hapa tuwekane sawa. Kuna Mzee wangu flani ana Suzuki swift kama daily Drive alafu ana Grand Vitara kama gari ya mtoko (hii Kila baada ya siku mbili inaoshwa ila haitembei, inaweza kukaa hata miezi sita haijawai Toka nje ya gate)
 
Hapa tuwekane sawa. Kuna Mzee wangu flani ana Suzuki swift kama daily Drive alafu ana Grand Vitara kama gari ya mtoko (hii Kila baada ya siku mbili inaoshwa ila haitembei, inaweza kukaa hata miezi sita haijawai Toka nje ya gate)


Grand Vitara is low class car hata kutokea haifai
 
Back
Top Bottom