Msifunge ndoa kabla ya kufanya utafiti

Msifunge ndoa kabla ya kufanya utafiti

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Imeelezwa kuwa wanandoa wengi wamekuwa wanaharakati zaidi kuliko kuwa walezi wa ndoa zao, jambo ambalo linasababisha migogoro kwenye familia na kuzifanya zivunjike.

Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Mkurugenzi wa Asasi ya TaMCare, Dk Enock Miyuka alipokuwa anazindua kliniki ya ndoa na uhusiano.

Alisema zipo baadhi ya familia, ndoa zimegeuka kuwa jela ya nyumbani na kusababisha upotoshaji juu ya kusudi na maana halisi ya ndoa na familia.

Dk Miyuka alisema hali hiyo imetokana na watu wengi ‘kuvamia’ na kuingia katika ndoa wakiwa hawana ufahamu na maarifa ya kutosha kuhusu taasisi hiyo.

Alisema mbaya zaidi wazazi, ndugu na jamaa wameelekeza nguvu kwenye kuandaa sherehe kubwa za harusi pasipo kuwaandaa vijana wao kuwa waume na wake bora. “Kukosa kufanya uamuzi makini wa urafiki na uchumba wa nani wa kuoa na kuolewa naye kwa sababu si kila mtu ana sifa ya kuwa mume au mke wa mtu,” alisema Dk Miyuka.

Alisema kutokana na hilo, TaMCare itakuwa na kliniki inayotembea itakayokuwa inatoa elimu kwa jamii kuhusiana na masuala ya ndoa, talaka na mirathi kwa jamii.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Majaji na Mahakimu Tanzania, Joaquine De Mello alisema maendeleo yanahitaji ndoa imara.

“Nawataka TanMCare kushughulikia kiini cha tatizo kwa kuwa kuna migogoro mingi katika jamii yetu, ndoa nyingi zinavunjika,” alisema Jaji Joaquine.

Ofisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Usajili, Ufilisi na Uthamini (Rita), Emmy Hudson alisema idadi ya ndoa na talaka imeongezeka nchini. Alitolea mfano kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka 2021, ndoa zilizofungwa ni 35,405 na talaka zilizotolewa ni 443.

Credit: Mwananchi
 
WENGINE WANAKIMBILIA NDOA BASI TU AONEKANE KAOA KUMBE HAJAJIPANGA
 
Back
Top Bottom