Msigwa: Bandari Ilikuwa inaingiza tsh 1 trillion na inamtumia tsh 880 bilioni ndio sababu tumeleta DP World Ili kuongeza Mapato!

Attachments

  • 9CD292BC-2183-46B1-9EB6-DF7B46FABED4.jpeg
    58 KB · Views: 2
  • 4734D82B-25BF-40FA-B619-ABFA3319CB0B.jpeg
    115.9 KB · Views: 2
  • 1D0D8EFB-2418-4D0C-80E7-263D2D90A4CC.jpeg
    4.3 KB · Views: 2
  • A12A8E30-E7E2-45B6-806C-6585B200DBB3.jpeg
    37.8 KB · Views: 2
  • 69F4AD93-7960-49D1-882E-D39E15848540.jpeg
    55 KB · Views: 2
  • B4453D86-A6BC-4723-9900-C23FA06BB623.jpeg
    23.3 KB · Views: 2
  • 602EB37D-D318-4D67-B5A6-D55B690F3A25.jpeg
    66.2 KB · Views: 2
  • IMG_0804.MP4
    5.4 MB
  • B860E3A5-A1D2-48F5-84F0-908446F9BE4D.jpeg
    37.4 KB · Views: 2
  • 472421B0-0430-4C82-B738-D98FD068B28A.jpeg
    140.9 KB · Views: 2
  • 2D93FC57-4027-485E-AE9B-F997D046DF93.jpeg
    79.5 KB · Views: 2
  • 60B17FD1-516F-4DDC-AF47-FF5E0B19F90F.jpeg
    32 KB · Views: 2
  • 1D5B9B05-B83B-4998-AA48-B47FD03B3939.jpeg
    55.3 KB · Views: 2
  • 7F94E5E0-04C8-448B-ADD5-047736DDA031.jpeg
    75.7 KB · Views: 2
  • F9929AF7-8E44-4345-8100-63E73773A171.jpeg
    150.5 KB · Views: 2
  • F9E35806-A370-4E4E-A3F2-0239F1FCAB01.jpeg
    131.1 KB · Views: 2
  • IMG_0547.MP4
    3.4 MB
  • 3675E2F0-0678-4C93-8C57-8EBFAB976E1D.jpeg
    51.3 KB · Views: 3
Machawa siyo kwamba hawajui, wanafanya makusudi tu.

Hata Mbarawa alipoulizwa kuhusu ukomo wa mkataba alijikanyaga tuu:-

Swali: mkataba utakoma lini?
Mbarawa:-
👇
View attachment 2667757
Wanasema kwamba patakua na mikataba mingine midogo midogo ya uendeshaji ambayo hio ndio itakua na ukomo as Bandarini pana huduma nyingi tofauti.

It's confusing.
 
Hivi zenji bandari yao wao wanapata faida? Au hawa DP WORLD hawataki huko zenji ni tz tu? [mention]FaizaFoxy [/mention]
 
Njia nzuri kwa kuongeza mapato ni kusimamia na kupunguza matumizi!

Kubana matumizi umekuwa ni ugonjwa wa serikali zetu! Ndio maana hakuna maendeleo!! Kuna uongo kwenye mapato ya 1t na kuna uongo katika matumizi ya 880!!
Bora Hawa wajanja watawale sio yule mchunga ng'ombe jamani. Kiufupi tu watu waliozalowa vijijini muwapeni madaraka ,angalia viongozi wote wa kiafrika waliozaliwa vijijini hata huko ulaya Asia walivyopiga kazi wakazinyanyua nchi zao
 
WATANZANIA NI WAVIVU . WEZI WA MAPATO YA BANDARI WANAJULIKANA TATIZO NI UCCM WATENDAJI WANATEULIWA KIUPENDELEO KIKABILA KIDINI NA KIITIKADI HATA WASIO NA SIFA WANAPEWA UONGOZI
 
Nashangaa yan bandari inatumia bil 880 anatakiwa afafanue zinatumikaje aache utapeli
 
Kwamba kodi ya magari bandarini itapanda sio.
 
Wanadhani watu wanapinga mwekazaji

Watu wanapinga MKATABA WA KIMANGUNGO.
 
Msigwa ni mngoni Wa
kwanza kuwa asiyejielewa mbona wakati Wa JPM hakuwa zuzu hivi
labda nimsaidie mngoni mwenzangu huo mkataba hauna tofauti na Wa bodaboda
Sio mngoni huyo jamaa

Hata hivyo kabila la mtu halimfanyi awe mjinga.

Ameamua tu kujizima data kutetea LSSE, posho na VXR
 
Kwa wao wanakuja na miujiza gani ambayo sisi tumeshindwa
 
Kumbe hamjauza, mmekodisha? mbona hizo terms za kukodisha zimeifanya nchi kuwa mateka kwa mwarabu! yaani mwarabu atadhibiti uingiaji na utokaji wa kila kitu nchini pamoja na vile vya kutoka nchi jirani, maana umemkodisha kukaa getini, haijulikani atakaa kwa muda gani hapo mlangoni na haijulikani ni nani atakuwa anamdhibiti kiusalama ili asifanye magendo, maana huwezi kumweka baunsa afanye kazi getini ukamwekea baunsa mwingine kumzuia asifanye kazi zake.
 
Tatizo sio mapato, tatizo sio waarab, tatizo sio wawekezaji, tatizo ni mkataba una masharti ya kijinga sana
Hawa watu wa ccm na serikali ni wajinga sana.
Hakuna anayepinga kuwa na mwekezaji, TICTS wamekuwepo kama wawekezaji.
Hakuna anayepinga kuongeza mapato, sote tunataka bandari (na maeneo yote) yafanye kazi kwa ufanisi.
TATIZO NI AINA YA MKATABA TUNAOSAINI (I guess they want to hear us yelling 😒)
1. Ni mkataba wa miaka mingapi (mkataba wa Ticts ulikuwa na ukomo wa miaka!)
2. Terms za kuuvunja mkataba zikoje? Mbona hawasemi tunawezaje kuvunja mkataba?
3. Kwa nini sehemu ya pili ya Muungano imeachwa nje ya manufaa haya manono kutoka kwa mwekezaji?
 
Tunajua ni wajibu wake kuitetea serikali lakini ,wenye nchi ni wananchi kama wana hoja zao zifanyiwe kazi more specially timeframe ya mkataba na vipengele baadhi ambayo raia wengi wasomi na sio wasomi wamekuwa wakinyoosha vidole .Watu sio wapingaji wa uwekezaji lakini terms za hii intergovernmental agreement ndio dira ya wapi tunaenda, sasa kabla haujawa legally binding serikali ikae na dp world wayaweke mambo sawa Yale wananchi wanayo raise as issue of concerns.
 
Mtu akikuambia kiko kipengele chenye matatizo muulize ni kipi iko kipengele? Hawezi kukuonesha maana hakipo. Mwisho wa kunukuu. Huu mkataba lazima utekelezwe hakuna mbadala wake. Huu ndio ukweli mchungu unao takiwa ukubalike kwa wanao ona walakini wa huu mkataba.

Ingekuwa vizuri nguvu kubwa ikaelekezwa kwenye kuutekeleza basi kuliko kwenye propoganda za kushawishi. Hizo fedha za kuelimisha mzipeleke kusaidia mayatima na wajane.
 
Kama wamekiri kushindwa KAZI hadharani,

Njia Bora ilikuwa ni CCCCCM kukabidhi Nchi haraka Kwa CDM Ili idhibiti wizi, ihakikishe mapato yanaongezeka, ufanisi pia unaongezeka,

Kuuza Mali nyeti kama bandari ni uamuzi wa "HOVYO"!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…