Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 34,954
- 80,256
Tunaweza kutofautiana kwenye masuala mengi ila linapokuja suala la uhai wa binadamu tunatakiwa kuongea lugha moja. Bado nazidi kuwashangaa waTanzania wenzangu waliokubali kuaminishwa na mfumo kwamba waTanzania waliuliwa barabani kama mbwa ni wahalifu na walistahili kuliwa kinyama.
unfortunately, most of them are commoners, waajiriwa wa mfumo kama kina Msigwa, wafagiaji wa kuta za CCM ambao wengi tunawaona hapa jukwaani na askari waliotumwa kuwaua ndugu zetu waTanzania kama wanyama. Wanasahau anayewatuma kuua anaitengeneza kesho ya mwanae na tumeona kupitia baraza la mawaziri.
Msigwa wanaokutuma kutoa matamko wanawaandalia watoto wao hicho kiti kinachokutuma kutoa matangazo. na askari uliyetumwa kuua jirani zako hukuwa unaiandaa Tanzania bora ya kesho au ya mwanao bali unamwandalia mtoto wa aliyekutuma kesho iliyo nzuri ili akaendelee kumtawala mwanao au wajukuu zako miaka ijayo.
I guarantee you wote mnaoshabikia mauji ya wadogo zetu au mama mjamzito aliyedondoka barabarani Arusha kama kuku wa kideri hakuna mnachofaidika nacho zaidi ya mishahara na ujinga wa kudanganywa mnaipigania amani ya Tanzania. Tutofautiane kwenye siasa za Uccm na CHADEMA ila kwenye maisha ya mtu tusimamie ukweli. Ajira yako haina thamani kuzidi Mama mjamzito aliyepigwa risasi Arusha Msigwa NA WENZAKO.