PreGE2025 Msigwa: Uchaguzi wa Tanzania utafadhiliwa kwa fedha zetu wenyewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Weka ushahidi

Uchaguzi Tanzania 2020: Kwa mara ya kwanza Tanzania itafanya uchaguzi bila kutegemea msaada wa nje​


Maelezo ya picha,Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba 28Maelezo kuhusu taarifa
  • Author,Na Munira Hussein
  • Nafasi,BBC Swahili Dar es salaam
  • 23 Oktoba 2020
Bajeti ya uchaguzi ni moja kati ya masuala ya msingi zaidi ambayo huenda yakachangia shughuli za uchaguzi kwenda kwa uafinisi ama kusuasua.
Katika uchaguzi wa nchi nyingi zinazoendelea hasa Barani Afrika, fedha za kuendesha shughuli nzima ya uchaguzi huegemea zaidi michango na misaada kutoka nchi zilizoendelea ama mashirika makubwa duniani kama benki ya dunia na mashirika ya kimataifa.
Na kiasi kingine cha fedha hutolewa na serikali ya nchi husika.
Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi huu Oktoba 28. Na tofauti na miaka iliyopita, bajeti ya uchaguzi ya mwaka huu inatolewa yote na serikali ya Tanzania.
Bila kusubiri msaada wa mashirika wa nchi za nje, Tanzania ilitangaza kuwa uchaguzi utagharamiwa na serikali ya nchi hiyo kwa asilimia 100.

BBC
 
Nitajie hata nchi mmoja iliyofadhili uchaguzi wa 2020
Badala ulete ushahidi unauliza swali.

Nyie ndio wale maraga mlikuwa mnamdanganya watu kwamba mnajenga Kwa pesa zenu za ndani kumbe mnakopa πŸ˜†πŸ˜†
 
Badala ulete ushahidi unauliza swali.

Nyie ndio wale maraga mlikuwa mnamdanganya watu kwamba mnajenga Kwa pesa zenu za ndani kumbe mnakopa πŸ˜†πŸ˜†
Ushawekewa uzi humu angalia post namba 18 kijana. Kula vizuri uongeze uwezo wa kumbukumbu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…