Bwana Hamsini amefuta mapingamizi yote hapa Serengeti na kumtaka kila mgombea apigane na hali yake, amesema yeye hana na hataki kujijengea chuki kwa kufuata maelekezo ktoka juu, kuenguana wataenguliwa kwenye sanduku la kura na sio yeye. Ametupilia mbali mapingamizi yote,yaliyowekwa na CCM.
Hongera sana Bwana Hamsini umejitenganisha na wajumbe na kweli wapo watu wanajua kurekebisha usawa. Nakumbuka kitabu cha Mbutolwe mwana wa Umma.
======
UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ZA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI SERENGETI KUWAREJESHA WAGOMBEA WOTE.
KUNA taarifa zinasambaa mitandaoni zikisema, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Serengeti amewarejesha Wagombea wote wa Udiwani na Ubunge, huku taarifa hizo zikienda mbali zaidi na kusema, Msimamizi huyu ameruhusu Wagombea wote wa Udiwani na Ubunge kuingia kwenye Uchaguzi ukiachilia mbali mapingamizi yote yaliyokuwa yamewekwa dhidi yao.
Tumelazimika kutoa ufafanuzi wa taarifa hizi, kutokana na ukweli kwamba, taarifa hizi zimeleta mkanganyiko mkubwa sana kwa umma hususani katika kipindi hiki tunachoipigania haki ya Wagombea wetu wapatao 13 wa Udiwani walioenguliwa kihuni na Wasimamizi Wasaidizi wa Kata husika kwa kile kinachoitwa maelekezo kutoka juu.
Ukweli wa taarifa hizi ambao umefichwa kwa maksudi kabisa ili kuupotosha umma na kuondoa jitihada za Chama katika kuipigania haki ya Wagombea wetu kurejeshwa katika nafasi zao ni huu hapa chini;
1: Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Serengeti, hata kabla ya muda wa michakato ya Mapingamizi na Rufaa kumaliza, aliitisha Mkutano na waandishi wa habari na akatangaza hadharani kwamba, kati ya Kata 30 za Jimbo la Serengeti, ni Kata 16 pekee zitaruhusiwa kuingia kwenye Uchaguzi huu, huku akitambua wazi kwamba, bado Wagombea wetu wapatao 13 waliofanikiwa kurejesha fomu zao kwa wakati sahihi kabisa wanazo haki za kuweka Mapingamizi na kukata Rufaa.
2: Aliyeitoa taarifa hii inayosambaa mitandaoni, hakuzingatia ukweli wa jambo hili na badala yake amejikita zaidi kuonyesha kwamba Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Serengeti ni Msimamizi mwema sana na anayetenda haki kwa vyama vyote vya siasa hata kama kuna Mapingamizi kwa Wagombea, kitu ambacho sio kweli na sio sahihi kabisa.
3: Suala la kuyatupa Mapingamizi yote ni jambo moja, lakini jambo la Pili tunalopaswa kujiuliza, ni Je, Mapingamizi hayo yaliyotupwa naMsimamizi wa Serengeti yalikuwa ya Wagombea wa upande upi na yalikuwa na uzito wa kiwango gani kwenye mizania ya Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi wa mwaka huu?
4: Chama Ngazi ya Wilaya, tunapenda Umma utambue kwamba, kuna Wagombea wetu wapatao 13 wanaoelekea kunyimwa haki yao ya msingi ya kugombea kwa maksudi kabisa kutokana na hujuma za Watendaji wa Tume ambao ni Makada watiifu wa CCM waliopewa maelekezo ya jinsi ya kuwahujumu Wagombea wetu.
5: Tunapenda Umma wa Watanzania ufahamu kwamba, hao Wagombea wetu wa Udiwani kwenye Kata zipatazo 13 walioenguliwa kati ya Kata 30 za Jimbo zima, walifanikiwa kurejesha fomu zao kwa wakati sahihi siku ya tarehe 25 Agosti, 2020 na wote walikuwa wanakidhi Sifa zote za kuwa Madiwani, lakini hadi sasa ninapoandika hapa, wanaelekea kunyimwa haki zao za msingi za kugombea kwa sababu Watendaji wa Tume wamedhamiria kuibeba CCM.
6: Ieleweka wazi kwamba, Kata zilizoruhusiwa kuingia kwenye Uchaguzi, ni zile tu ambazo Wagombea wetu walipata uteuzi baada ya Saa 10:00 za jioni siku ile ile ya uteuzi. Hivyo basi, tunamtaka huyu Mwandishi wa hizi taarifa ajiridhishe vizuri kupitia kwa Msimamizi wa Uchaguzi juu ya hizi habari zake zenye upotoshaji.
7: Kata 13 ambazo Wagombea wetu wameenguliwa kihuni na Wasimamizi Wasaidizi wa Kata bila kupewa sababu yoyote ile ya kuenguliwa kwao kati ya Kata 29 ambazo Wagombea wa Chadema walifanikiwa kurejesha fomu ni pamoja na; Kisaka, Busawe, Majimoto, Kenyamonta, Magange, Mosongo, Nyambureti, Nagusi, Natta, Uwanja wa Ndege, Ikoma, Manchira na Kebanchabancha.
Ni Kata moja pekee ya Ring'wani ambayo Mgombea wetu hakufanikiwa kurejesha fomu zake kutokana na sababu kadhaa zilizokuwa nje ya uwezo wetu kama Chama.
8: Kwa masikitiko makubwa sana, baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi la Polisi wa Wilaya ya Serengeti wametumika kwa kiwango kikubwa kushiriki uovu huu hasa kwenye Kata zote za tarafa ya Ngoreme zilizoenguliwa.
Baadhi ya Askari hawa wa Jeshi la Polisi, wametumika kutisha watu wetu wakiwemo Wagombea ili kutoa mwanya kwa Watendaji kutoroka Maofisini bila kuwapa nakala Wagombea wetu ama kutoa majibu yoyote ya kwa nini hawakuwateua Wagombea wetu kwenye Kata zote 13 nilizozitaja hapo juu.
Mfano; Polisi wametumia Nguvu kubwa sana kushiriki hujuma kwa Wagombea wetu wa Kata za Kenyamonta na Magange huku wakiitumia Nguvu ya kiwango hicho hicho kuhujumu haki za Wagombea wetu wa Kata za Majimoto, Busawe na Kisaka.
HITIMISHO
Kutokana na hali hiyo iliyojitokeza na kwa uhalisia wake, sisi tunaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi itende haki na haki hiyo ionekane kutendeka kwa Wagombea wetu na wapewe fursa ya kuwa Wagombea kwenye maeneo yao ili kuepuka kuwanyima Wananchi haki yao ya msingi ya kuamua nani awe Mwakilishi wao.
Aidha, tunatoa wito kwa Umma wote wa Wana-Serengeti na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kupaza Sauti dhidi ya hujuma zinazofanywa kwa Wagombea wetu 13 wa Udiwani Jimbo la Serengeti walioenguliwa kihuni na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi tena kwa maelekezo yenye lengo la kuibeba CCM.
Francis M. Garatwa,
M/Kiti CHADEMA Serengeti.
30 Agosti, 2020.