Uchaguzi 2020 Msimamizi wa Uchaguzi awanyima fomu CHADEMA Jimbo la Kibamba, adai fomu yao imeshachukuliwa

Uchaguzi 2020 Msimamizi wa Uchaguzi awanyima fomu CHADEMA Jimbo la Kibamba, adai fomu yao imeshachukuliwa

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Mkurugenzi anayehusika na Uchaguzi jimbo la Kibamba amekataa kutoa fomu kwa mgombea wa CHADEMA kwa kile alichodai kuwa kuna mtu aliyedai kuwa Mgombea wa CHADEMA ameichukua fomu husika hivyo hawezi kutoa fomu mara mbili. Hivyo amewataka CHADEMA washirikiane na polisi kumsaka muhusika.

 
Binafsi sioni kama kuna ugumu wowote hapo. Ningemshauri na kumsihi msimamizi atoe form nyingine mana kimsingi yeye ndio katapeliwa.

Then kama wagombea wote wawili watarudisha form si Tume itachambua hizo form za maombi na kumtoa mgombea aliyefanya utapeli?

Kukataa kutoa form nyingine Kwa wagombea halali ni dosari isiyo ya lazima mana kama nchi mzima wakifanya uhuni kama huo si itakuwa ni chanzo cha vurugu?

Pia ushauri wa Mwanasheria unapotosha. Anaonyesha kama vile mgombea akirudisha form automatically anakuwa mgombea rasmi. Hiyo ni form ya maombi ya kuteuliwa/kupitishwa na Tume kuwa Mgombea rasmi, na kwenye maombi kuna kukubaliwa au kukataliwa/kuwekewa pingamizi. So hapo hakuna ugumu wowote, Mkurugenzi anatengeneza tension isiyo ya lazima.

Kwann form iwe mojamoja? Kwan zinashushwa toka Mbinguni?
 
Wakamtafute kwani wao ndio waliomkabidhi form, ana akili lakini huyo? Ina maana bank akienda mtu kuhushi cheque yangu benki watasema hawahusiki wao? Kwenye video huyu mtu hayumo? Hajatowa National ID kama kitambulisho akafuatiliwa kwenye mawssillianonl yake na kupatikana?
 
Binafsi sioni kama kuna ugumu wowote hapo. Ningemshauri na kumsihi msimamizi atoe form nyingine mana kimsingi yeye ndio katapeliwa...
Exactly, labda kama walipewa fomu moja moja kwa kila chama. Lakini yeye ndiye anayetakiwa kuwajibishwa kwa kutoa fomu kwa mtu ambaye hakupitishwa na CHAMA kilichosajiriwa kisheria.
 
Exactly, labda kama walipewa fomu moja moja kwa kila chma. Lakini yeye ndiye anayetakiwa kuwajibishwa kwa kutoa fomu kwa mtu ambaye hakupitishwa na CHAMA kilichosajiriwa kisheria.
Utetezi wa huyo mama mkurugenzi ni wa kijinga mno na unaidhalilisha CCM kwa kuwamiliki wakurugenziccm wasio na weledi wa kutosha na kwa aina ya utendaji wake ni vigumu kumtamgaza mshindi endapo chadema watashinda hapo kwake.
 
Back
Top Bottom