LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi Njombe: Hakuna kijana atakayeweza kutumika kuvuruga zoezi la uchaguzi

LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi Njombe: Hakuna kijana atakayeweza kutumika kuvuruga zoezi la uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya mji wa Njombe, Kuruthum Sadick amesema kuwa kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi mpaka siku ya uchaguzi hakuna kijana atakayeweza kutumika kuvuruga zoezi la uchaguzi kwa kuwa vijana wa Njombe wanaelewa maana ya uchaguzi.
1732023271546.png
Kuruthum ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za halmashauri hiyo ambapo pia amesema kampeni zitaanza kesho Novemba 20 mpaka 26 kuanzia majira ya saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni kulingana na ratiba walizokubaliana na vyama vya siasa.

“Hapa kwetu vijana wamekuwa wakitumika kuhamasisha zoezi la uchaguzi kwa hiyo hakuna kijana anayeweza akatumika kwa njia ambayo ni mbaya kwa sababu wanaelewa uchaguzi ni nini na amani yetu ni kitu gani,” amesema Kuruthum

Aidha, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kampeni na kusikiliza sera za wagombea ili waweze kuchagua viongozi sahihi kwa kuwa tayari wagombea wameleta ratiba zao.

“Kwa hiyo mimi nitaomba kwa vyama vyote Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), niombe waweze kufuata utaratibu wa ratiba ambayo walijiwekea ili kuweza kufanya kampeni zao kwa amani,” amesisitiza Kuruthum.

Nao baadhi ya wananchi mjini Njombe, akiwemo Mary Mligo amesema wamejiandaa vizuri kushiriki na kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika nchini kote tarehe 27 Novemba mwaka huu licha ya wachache kuona suala hilo halina umuhimu.

Soma, Pia: Yanayojiri kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoa wa Njombe
 
Waombea wote wa chadema wameenguliwa, sasa hofu ya nini tena?
 
Back
Top Bottom