The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 2,471
- 3,768
Nimekutana na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji wa mwaka 2024 ambaye ni mkuu wa shule mojawapo katika mkoa wa tabora, kwa masikitiko makubwa ameeleza namna viongozi wa serikali walivyowalazimisha kujaza form za wagombea wote wa ccm ambazo zote zilikosewa kujazwa.
Anasema walipigiwa simu na kuitwa usiku na viongozi wao wa kata wakaambiwa kuna bahati mbaya imetokea wagombea wetu wa ccm wamekosea kujaza form hivyo chukueni form zote mzichane alafu wajazieni upya.
Mkuu huyu ambaye alikuwa akiongea kwa hofu sana anasema mbali ya kuwajazisha form za wanaccm pia waliamriwa kuharibu form za wapinzani ambazo zote zilikuwa zimejazwa kwa usahihi.
Haya mambo ndiyo humfanya kila mwenye mapenzi mema na nchi atamani mabadiliko ili mifumo ya uchaguzi isidhibitiwe na serikali wala chama tawala.