Msimamo: Napinga Mkapa kupongezwa kwa kuandika kitabu kinachoeleza makandokando yake

Msimamo: Napinga Mkapa kupongezwa kwa kuandika kitabu kinachoeleza makandokando yake

Laiti kama Mzee huyu angeandika kitabu cha kufundishia watoto shuleni cha alphabet kama 'a e i o u' au cha hesabu ama kiswahili sanifu basi nisingetia neno lolote, lakini kwa kitabu hiki alichoandika sitathubutu kumpongeza hata chembe.

Benjamini Mkapa mtu aliyeingia madarakani baada ya kuapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Tanzania, huku akiwa na akili timamu hawezi kupongezwa na yeyote mwenye akili timamu kwa kuandika kitabu kinachoelezea namna alivyofanya madudu yake ikiwa ni pamoja na mauaji ya wapemba akiwa madarakani jambo ambalo ni kinyume cha Katiba aliyoapa kuilinda, nani aliyekuwa hajui kuhusu yeye kufanya biashara Ikulu, nani hakufahamu kuhusu wizi wa kienyeji wa EPA uliokuja kunufaisha chama chake?

Alipokuwa madarakani mbona hatukumsikia akipigia chapuo Tume huru ya uchaguzi, why now? Amelenga kumdanganya nani na kwanini, ni hofu ya uzee?

Mtu ambaye miaka michache iliyopita aliwaita wapinzani wapumbavu leo amepata wapi huruma ya kuomba washirikishwe kwenye michakato ya nchi?

Ikiwa kama lengo la Mkapa lilikuwa ni kutubu basi ni vema angekutumia njia ya madhabauni lakini si ghiliba hii ya kitabu, ikiwa kama tutamsifia huyu basi bila shaka na hawa wengine watatumia njia hii hii kuja kutung'ong'a ili nao wahurumiwe.

Siungi mkono kitabu cha Mkapa na makandokando yaliyo ndani yake na naomba msimamo wangu uheshimiwe.

Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko.
Kupongeza au kuponda ni haki yetu kikatiba ambayo wewe Erythrocyte huwezi kuipokonya. Ungetutendea haki kama na wewe ungeandika kitabu chako kuponda other wise acha kulia Lia hapa.

BWM ndiye baba wa uchumi wa wa kisasa Tanzania. Misingi aliyoiweka ndiyo JK, JPM na Samia wanatembelea
 
Angalau Nyerere hawa wengine ni balaa tupu na aibu hakuna cha maana walichofanya zaidi ya kutafuna mali za nchi
 
Mimi sitalishangaa bandiko hili maana baadhi ya Watanzania wenzetu wao kazi ni pinga pinga tuu kila kitu, kiwe kizuri, kiwe kibaya wao watapinga tuu.

Watu wa aina hii, niliwazungumza hapa

P
Huna mvuto tena
 
Back
Top Bottom