Msimamo: Napinga TBC kurusha Live Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea Urais wa CHADEMA

Msimamo: Napinga TBC kurusha Live Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea Urais wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Kitakachofuata ni kuzima zima mitambo hata yatakayoongelewa yasieleweke na inawezekana inawekwa hivyo ili upande wa pili wapate point za kujipigia nikienda mbali zaidi naweza ona mtu akiwekewa sumu kwenye mic..nukta naomba niishie hapo
 
Chief sasa iv TBC ndio talk of the town, habar zao wana andaa kwa kiwango cha juu sanaa yaan ITV siku izi kwa TBC ni teke la mtu mzimaa na teke la mtoto. ...
nani anaangalia TBC nchi hii , umewahi kufanya utafiti wowote , unadhani wafanyabiashara kutopeleka matangazo ya biashara zao TBC ni wajinga ? mtabaki kutangaza dawa za nguvu za kiume za kigogo mbuyuni tu .
 
Chadema ni mali ya umma lazima tbc warushe matukio yenu, wakicover matukio yenu mnalalamika wasipocover mnalalamika sasa tuwaeleweje?
 
nani anaangalia TBC nchi hii , umewahi kufanya utafiti wowote , unadhani wafanyabiashara kutopeleka matangazo ya biashara zao TBC ni wajinga ? mtabaki kutangaza dawa za nguvu za kiume za kigogo mbuyuni tu .

Itisha poll hapa JF uone mwenyewe maana tusiandikie mate wakat wino umejaa tele
 
Wanakwepa dhambi nyingine yakufungia kituo kingine cha habari siku saba hahahhah, hapo akienda Tbc wajue wamepoteza ushindi TBC watacheza figisu kwenye hizo video ziwe hazina rangi wala kusikika halafu ndo mjue bao la mkono linapotokea
 
Chadema inafahamika na ina nguvu kubwa kuliko TBC
Nguvu gani wakati mmeshindwa kupata coverage yoyote, mnajipiga vifua halafu mfukoni watupu, kwa ujinga huu CCM watawacharaza sana, ni sawa na anafurahia alimsumbua bwana wake kabla ya kuvuliwa chupxx.
 
Tbc siyo kwa ajili ya wanasiasa tu, hata wasio wanasiasa wanalipa kodi na wana haki ya kuwasikiliza wagombea wote ili wafanye maamuzi sahihi.

Cha kufanya wewe pinga nyumbani kwako kutazama TBC, usiwaze kichadema chadema muda wote.

Hata mimi binafsi nasubili kwa hamu nifuatilie mkutano huo kupitia TBC.

Wenzenu ccm wana Channel ten nyinyi sijui mtaamka lini kujuwa umuhimu wa kumiliki tv station yenu, yani mnazidiwa maarifa hatanna wahuni tu kama kina Majizo?
Ni msimamo wangu , hayo mengine sijayasema , wakati ukilaumu Chadema kutokuwa na Channel yake jiulize walikopotelea Tanzania Daima , Mawio na MwanaHalisi
 
Huu ndio unyumbu sasa, CDM iwe kiki kwa TBC wakati hamna hata channel moja inayo onyesha matukio yenu live, huu ujinga unapatikana Ufipa tu.

Wewe "ni kina nani" kwani? Ni CCM siyo?

Nyie mnayo TV Channel ya kurusha matangazo "live?"

Inaitwaje? Iko wapi?
 
Tbc siyo kwa ajili ya wanasiasa tu, hata wasio wanasiasa wanalipa kodi na wana haki ya kuwasikiliza wagombea wote ili wafanye maamuzi sahihi.

Cha kufanya wewe pinga nyumbani kwako kutazama TBC, usiwaze kichadema chadema muda wote.

Hata mimi binafsi nasubili kwa hamu nifuatilie mkutano huo kupitia TBC.

Wenzenu ccm wana Channel ten nyinyi sijui mtaamka lini kujuwa umuhimu wa kumiliki tv station yenu, yani mnazidiwa maarifa hatanna wahuni tu kama kina Majizo?
Shwain wewe ,

Huoni magazeti , blogs na redio zenye affiliation na upinzani zinavyokula Ban.

Kwa akili zako za kuvukia Barabara unadhani upinzani ikiwa na TV station ndio haiwezi kufungiwa!


Halafu ukute wewe ni baba mtu mzima bichwa kubwa la kufugia nywele badala ya kufugia Ubongo.


Punda wewe.
 
😀😀😀😀
Ni wewe au!! Viongozi wako wapo upande wako!!! 😀😀😀
Mliwasema sana.. sasa wamewasikia.. si mufurahie mnasaidiwa kupata wapiga kura au!!.. TCRA nayo inawasaidia kwa wale wanyonge.. wasio weza kusikiliza tena vipindi vyao kwenye radio yao pendwa.. wamekasirika.. na wanafikiria wali wa Rungwe na wengine.. wawape kura.. kisa TCRA kuruka wengine na kuadhibu Clouds Media.
umefanya ile kitu lakini?
 
Duh, sijaelewa bado...kwani kubadilika in dhambi?
Kwanini wabadilike wakati huu wa kampeni? wanatafuta kura za huruma wale, kama sio hivyo TBC wakimaliza kuonesha huo mkutano nao wafungiwe kama wengine wanavyofanyiwa.
 
Kwa miaka mingi sana tangu kuondolewa kwa Tido Mhando kwenye uongozi wa TBC , Channel hii imejipambanua bila kificho wala uoga wowote kama channel ya ccm , kwa kuonyesha kila kinachofanywa na ccm hata mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa Taifa hili , imewapuuza wapinzani katika kipindi chote hicho huku ikiwanyima hata nafasi ya kukohoa tu kwenye mic zao , Watangazaji wake wamekuwa makada halisi wa ccm wenye kusifia hata ukandamizaji , hoja zote zenye tija hazijawahi kupewa nafasi kwenye TV hii .

Kwa tabia hii TBC imepoteza kabisa watazamaji katika nchi hii baada ya wananchi kwa umoja wao kuidharau moja kwa moja , nini kimetokea leo kwa TBC kutangaza mkutano wa Chadema , Je TBC inatafuta umaarufu kupitia mgongo wa Chadema baada ya wananchi kuipuuza ?

Napinga jambo hili na sitakubali Chadema itumike kama ngazi , waendelee kuifagilia ccm sisi tutapita nyumba kwa nyumba .

Naomba kuwasilisha .
Waliona wamekosa watazaamaji, sasa wanataka kunyanyua namba ya watazamaji wake, na njia pekee ya kunyanyua namba ya watazamaji ni Lissu na Chadema
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom