Kwa miaka mingi sana tangu kuondolewa kwa Tido Mhando kwenye uongozi wa TBC , Channel hii imejipambanua bila kificho wala uoga wowote kama channel ya ccm , kwa kuonyesha kila kinachofanywa na ccm hata mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa Taifa hili , imewapuuza wapinzani katika kipindi chote hicho huku ikiwanyima hata nafasi ya kukohoa tu kwenye mic zao , Watangazaji wake wamekuwa makada halisi wa ccm wenye kusifia hata ukandamizaji , hoja zote zenye tija hazijawahi kupewa nafasi kwenye TV hii .
Kwa tabia hii TBC imepoteza kabisa watazamaji katika nchi hii baada ya wananchi kwa umoja wao kuidharau moja kwa moja , nini kimetokea leo kwa TBC kutangaza mkutano wa Chadema , Je TBC inatafuta umaarufu kupitia mgongo wa Chadema baada ya wananchi kuipuuza ?
Napinga jambo hili na sitakubali Chadema itumike kama ngazi , waendelee kuifagilia ccm sisi tutapita nyumba kwa nyumba .
Naomba kuwasilisha .
[/QUOT
Cjajua Sana commitment ya TBC juu ya kurusha mkutano huo mwanzo Mwisho. Nina wasiwasi matangazo yanaweza katwa ghafla kwa sababu uzoefu unaoonyesha hapa kwetu hatuna uwezo wa kuckia Mambo magumu na hasa yanapogusa high profile people. Nijuavyo kampeni kwa namna yoyote ina Mambo magumu. Je watarusha mpaka Mwisho kweli?