Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Umeona ya Mbowe, ya Magufuli na kuua demokrasia huyaoni ukayesemea.
Bila shaka hujamuelewa Mwanakijiji. Yeye keshasema kuwa huyo Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala anakandamiza na kuharibu demokrasia.

Lakini amesisitiza kwamba demokrasia ni sawa na haki ambayo haipaswi "kuombwa" kama anavyofanya Mbowe kuomba usawa. Mbowe kama kiongozu mkuu wa chama tena chama kikuu cha upinzani alitakiwa kuchukuwa hatua "ngumu" kulinda demokrasia na siyo kumlamba miguu mwenyekiti wa chama tawala atoe "usawa".

Maana yake ni kwamba Mbowe ni dhaifu na kwahiyo hafai tena kuongoza chama badala yake awaachie wengine walete mikakati na mipango mipya.
 
liwalo na liwe , Mwanakijiji ni mfuasi wa Dr Slaa kama vile unavyoweza kuwa wewe na mfanyakazi wako wa ndani , hakuna asichojua kwamba Slaa alijiuza kwa udalali
wa mkewe lakini anataka kuaminisha watu humu kama Slaa aliondoka kumkimbia Lowassa , alipitishwa mlango wa chooni pale Kilimanjaro kwa udhamini wa Mwakyembe , akamtukana Sumaye leo yuko chama kimoja na Sumaye na lowassa mbona hakujiuzulu ubalozi ? haya yote Mnafiki Mwanakijiji anajua leo anakuja na ujinga wake hapa ! kachokoza nyuki .
Huyu Mzee anaendesha propaganda tu humu.
 
HAKUNA
Tatizo, miaka yote ya chama inamaana hakuna mbadala wa mbowe?
Kutokuwa na wigo mpana wa kiuongozi ni Tatizo kwa chama, Mbowe amefikia mwisho wake, alifaa chama kwa wakati wake, kwa sasa angeingia mtu mbadala aliye andaliwa na chama, kuliko Haya yanayo endelea kutokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli kwenye suala zima la INTELLIGENCE ya udukuzi ndani ya chama, CHADEMA mko vizuri saaana.Nimefurahishwa saaana na intellijensia yenu.Watu sasa wanaanza kuwaelewa.
 
Mfano mzuri aliegombea uenyekiti na aliekuwa Katibu Mkuu Leo wote wamevalishwa kijani manake ingekuwa wamechaguliwa hao kuwa viongozi manake chadema ndio ingekuwa mwisho

That is not Africa man! Nikisema Afrika (SA excluded) hakuna wa kujiudhulu kisa mikakati ya chama haifanikiwi. Kwa Mh. Mbowe mikasa anayoipata si kwa sababu ya chama chake kukosa mikakati mizuri bali dola imetumika kumdhoofisha. Hata akijiudhulu atakayeingia hawezi kuleta jipya - sana sana atakiangusha chama shimoni labda awe tayari kulamba viatu vya watawala. Kama kungekuwa na siasa safi CDM wangekuwa imara zaidi na hawa hama-hama wasingekuwepo. Hatujawahi kushuhudia katika Tanzania wabunge na madiwani wengi kuhama chama kisa - KUUNGA MKONO JUHUDU....

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanaofikiri kwa kutumia utumbo badala ya ubongo ni hasara kwa vyama vya upinzani hao jamaa wangekuwa na uwezo bila team work ya chama ilipaswa waanzishe vyama vyao tuone! yaani kwa mambo uliyoandika umedhihirisha uko kwenye mkakati wa jiwe HUTAFANIKIWA
Watu wanafikiria kuwapoteza watu kama Kitila, Mwigamba, ni jambo dogo... wengine tuna maslahi zaidi na CHADEMA kuliko watu wanavyofikiria. Tungeshindwa uchaguzi fair and square 2015 leo tungekuwa kwingine kabisa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Komredi Mbowe, usiwasikilize hawa 'MANYANG'AU' komaa, yanakuja yakiwa na mission zao yakishindwa yanarudi jehenam yalikotokea! una mtaji wa maelfu nyuma yako kamwe usigeuke nyuma ukawa mnara wa chumvi kama hao vibaraka.
 
Endeleza ukabila!!

Tunajua uko mlengo gani kwa faida ya nani.

Wewe ni sawa na zilpendwa,hakuna wa kukuamini tena.

Uliheshimika kwa hoja zako na si kwa jina lako unalotaka kuendelea kulitumia kwa faida ya unaowatumikia.

Mapandikizi yenu yamefeli sasa mnatapata!!

Wewe na Dr.Mihogo wote wanafiki.
Ila Salary Slip, nafikiri inawezekana MMM ana hoja inayotakiwa kufanyiwa kazi. Mbowe tayari ni Mwenyekiti kwa muhula mwingine lakini anafanya kazi katika mazingira magumu sana ya kisiasa. Katika mazingira ya awamu hii chama kinahitaji kiongozi mjeshi jeshi (Militant leader). Kiongozi atakayeweza kuendana na ‘kupambana’ vema na uongozi uliopo kwa kuhamasisha wanachama na wafuasi kuushinda woga hasa mwaka huu ambapo CCM wamejipanga kupoka ushindi wowote ambao upinzani wa kweli utaipata kwenye uchaguzi ujao.

Binafsi, namuona Mh Mbowe kama dhaifu na ni vema baadhi ya maoni ya wadau, wakiwemo wale wanaokihama chama, yakafanyiwa kazi ili kama si Mbowe kuondoka basi namna ya utendaji ibadilike na kufanya siasa ambazo ni za kimkakati zaidi ya kuwania kushika dola.

Lazima kitu kifanyike, vinginevyo Chadema na upinzani kwa ujumla utaambilia viti vitatu tu bungeni (huo ni utabiri tu). Mapendekezo yangu ya msingi ni kwa Mbowe kuanzisha mchakato wa kuunda coalition kama iliyokuwa ‘Ukawa’! Natamani kiongozi wa CDM awe proactive na aggressive kama Zitto Kabwe, awe vocal zaidi!

Natamani upinzanibuwe na vyombo vya habari kwa ajili ya ptopaganda kutoa elimu na kufanya propaganda ‘chanya’ hasa kipindi cha mwaka huu.

Mbowe anahitaji kubadilika au kujiuzulu kwa manufaa ya chama!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa haki na kwa kulinda heshima ya chama, Mbowe hakutakiwa kugombea uenyekiti wa chama, kwa maana nyakati zilizopo zimebadirika zinahitaji mbinu nyingine ili kuuvusha upinzani kwenye huu mkwamo uliopo.
Wapya Kama Wakina Cecil Mwambe?
 
Wenye akili ni hao wanaohama vyama kwenda kufeed familia !!! daah wadanganyika sijui mnaakili gani
Mzee mwanakijiji umekuwa ukitoa ushauri mzuri kila mara kwa hiki chama mfu.wenye chama Chao wameziba macho na masikio hawaishi kejeli na matusi.
Wenye akili wameondoka wamewaachia mazuzu na manyumbu chama Chao. Sikio la kufa halisikii dawa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ingetokea viongozi wa Chadema, wabunge na madiwani wanajitoa Chadema na kujiunga na vyama vingine kama ACT, CUF, NCCR nk ambavyo vinapigania haki dhidi ya ukandamizaji wa chama tawala CCM na kuendeleza ile misimamo yao nje ya Chadema hakika hoja yako ingekuwa fikirishi.
Tungejiuliza sana Mbowe anakosea wapi? Jee anafaa au aondoke? nk.
Lakini viongozi hao wameondoka kwenda CCM na kutuachia maswali jee yale waliyokuwa wakipigania yamefanyika? Kuna tuhuma za chama tawala kuhonga ili kuyumbisha upinzani nalo vipi?
Ukifika hapo unapata jibu kuwa Mbowe hana sababu ya kuondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.

Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.

India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.

Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.

Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.

Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT

Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!

Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.

Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.

Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!

Binafsi naamini kuondoka kwa Kashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.

Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.

Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.

MM. Mwanakijiji
Mimi sijui wasomi wetu wanakosea wapi, wewe unanaona tatizo Ni mbowe? Ebu FIKIRI KIDOGO KWA UBONGO. mazingira ya siasa ya TZ unayajua? Watu wananunuliwa na ushahidi upo TAKUKURU wameshi dwa kufanya kazi. Unataka mbowe awambue watu wapambane na polisi? Hapana hizo siasa za fujo hatuzutaki sisi anafanya kwa kiwango Cha JUU kabisa. Tana HEKIMA ikiwa imetawala. Wewe unakuja na maandishi yako mengiii unaki ganisha naxingira ya siasa za USA na tz my bro MUMEFAIL VIBAYA MNO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma bila kuweka hisia zilizoumizwa. Unaona bado anastahili kuongoza CHADEMA kuelekea kushindwa tena? Hadi nini kitokee ndio utajua upinzani unahitaji kiongozi mwingine?
Kwa wakati huu Sana tu, sasa hivi sio CCM dhidi ya upinzani bali ni dola dhidi ya wapinzani, ndio maana wanna CCM wana uwezo wa kutoa hukumu za vifo kwa wapinzani wao hadharani bila hata uoga. Jabari Kama Mbowe ndio anaweza kuivusha CDM
 
Back
Top Bottom