Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

So ulitaka Sumaye ndio awe Mwenyekiti? poor reasoning.
 
Mwanakijiji mwenzangu, Mimi ni Mwanakijiji kutoka Nshara Wilayani Hai kata ya Machame ,Mbowe n Mbunge wangu Kwa Nyumbani. Lakini Kwa aina ya siasa zake si Za kwenda mbali. Nimemshauri Kwa kinywa changu ajitathimini kama bado anafaa. Nilimwambia atoe nafasi Kwa nguvu mpya wakati anakubalika
 
Huyu Mzee anaendesha propaganda tu humu.
analipwa , kuna wakati alipendekezwa na Mwakyembe apewe UDC lakini utata ulijitokeza kidogo upande wa elimu na mashambulizi yake kwa ccm na Magufuli siku za nyuma kabla ya kukengeushwa na Dr Slaa akapigwa chini .
 
Kama ingetokea viongozi wa Chadema, wabunge na madiwani wanajitoa Chadema na kujiunga na vyama vingine kama ACT, CUF, NCCR nk ambavyo vinapigania haki dhidi ya ukandamizaji wa chama tawala CCM na kuendeleza ile misimamo yao nje ya Chadema hakika hoja yako ingekuwa fikirishi.
Tungejiuliza sana Mbowe anakosea wapi? Jee anafaa au aondoke? nk.
Lakini viongozi hao wameondoka kwenda CCM na kutuachia maswali jee yale waliyokuwa wakipigania yamefanyika? Kuna tuhuma za chama tawala kuhonga ili kuyumbisha upinzani nalo vipi?
Ukifika hapo unapata jibu kuwa Mbowe hana sababu ya kuondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Cha kushangaza zaidi ni kuwa wote wanaohama kutoka CHADEMA kwenda CCM wanapokelewa na kupewa nyadhafa chamani na serikalini! Hii ni rushwa moja kwa moja.
 
Kwa haki na kwa kulinda heshima ya chama, Mbowe hakutakiwa kugombea uenyekiti wa chama, kwa maana nyakati zilizopo zimebadirika zinahitaji mbinu nyingine ili kuuvusha upinzani kwenye huu mkwamo uliopo.
Ilitakiwa mwenyekiti awe sumaye au mwambe?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.

Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.

India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.

Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.

Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.

Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT
Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!

Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.

Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.

Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!

Binafsi naamini kuondoka kwa Mashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.

Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.

Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.

MM. Mwanakijiji
Uko sahihi kabisa! Mbowe kuwa m/kiti au la, haikuhitaji muda wote huu utadhani ni africa ya miaka ya 70. Tatizo liko kichwani. Malengo ya Mbowe ni yapi ktk siasa? Huyu anafanya siasa ya kibiashara. Kwa kuwa anapata pesa hajali. Wote waliotoka ni watu waliotumainiwa lakini yeye anajidai CHADEMA haiteteleki.

Lipo tatizo la ukabila ambalo ukilitaja wanazizima kama nyuki. Ukweli ni kwamba Wachaga wanaiona CHADEMA kama chama chao. Mbali na walioko ktk uongozi, walioko nje wakiona kabila jingine linasogelea hiki 'chama chao' wanapata taabu na lazima wakupe taabu. Sioni taabu kumuondoa katibu huyu na kuingiza yule, lakini kuna taabu kubwa ukiona katibu mstaafu anahamia chama kingine.
 
Mmmmmmh bado Mbowe anahitajika sana, tatizo mfano yote uliyoitoa ni ya dunia ya kwanza na ya pili anbayo mazingira yako ni tofauti kabisa na mazingia na siasa zetu. Hapa unazungumzia chama ambaçho hakijapewa kufanya mikutano ya hadhara kwa miaka 4 au mitano haha unamaanisha mashinji ambaye hafahamiki kwa watanzania hajawahi kufanya mkutano wowote wa hadhara na sidhani kwamba tangia achaguliwe amewahi kujitambulisha. Madhingira ya sasa ya siasa ni tofauti sana bado Mbowe anahitajika kwa kweli
 
Mbowe haondoki CDM kwa kelele za wajinga, mmemkosa risasi anadunda, mmempachika kesi za ajabu ajabu, mmeharibu mali zake bado hatishiki, mmemtungia mpaka sheria ya kijinga ya vyama inayompa msajili madaraka ya ajabu bado Mbowe yupo tu.

Wote wanaokimbilia CCM sasa ni njaa tu, wanafuata opportunities, hamumdanganyi mtu mwenye kujielewa, ENDELEENI KUPIGA KELELE.

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM ni waoga wa tume huru ni sawa na mtoto kumtishia kwa kitu anacho ogapa ukiwambia tume huru hiyoo! wanakimbia
 
Endeleza ukabila!!

Tunajua uko mlengo gani kwa faida ya nani.

Wewe ni sawa na zilpendwa,hakuna wa kukuamini tena.

Uliheshimika kwa hoja zako na si kwa jina lako unalotaka kuendelea kulitumia kwa faida ya unaowatumikia.

Mapandikizi yenu yamefeli sasa mnatapata!!

Wewe na Dr.Mihogo wote wanafiki.
Kamanda kaguswa Mbowe mnang'aka, mtaendelea kulialia mfululizo, wananchi wamepuuza ajenda yenu ndio maana wanaendelea na yao.
 
Naomba unisaidie jambo.. Alipoondoka Lowasa CCM na kujiunga na CHADEMA, MWENYEKITI wa CCM ALIPASWA KUJIUZULU?

Alipoondoka Sumayi, Nyalandu, Dr. Slaa na wengineo kujiunga na CHADEMA,MWENYEKITI WA CCM ALIPASWA KUJIUZULU? Kwa nini kuondoka kwa Mashinji kuwe sababu ya Mbowe kujiuzulu?

Umetolea mfano wa baadhi ya Viongozi waliojiuzulu sababu ya vyama vyao kushindwa chaguzi, je hakuna ambao waliendelea kubakia na madaraka yao baada ya vyama vyao kushindwa uchaguzi?

Huwa wanasema wewe ni mwelewa wa mambo, hivi kwa uelewa wako umeshindwa kuyatambua mafanikio ya Mbowe kwenye siasa za upinzani katika Taifa hili?

Ni uchaguzi gani CHADEMA chini ya Mbowe imepoteza ushindi? Unataka kumlaumu Mbowe kwa Wabunge, Madiwani na Viongozi wengine wa CHADEMA kujiunga na CCM kwa madai ya kumuunga mkono Kiongozi wa Nchi?

Kwa akili zako unahisi Kiongozi wa Nchi hastahili kuungwa Mkono?

Unadhani kwa nini ni Mbowe ndiye anaestahiki kujiuzulu Uongozi wa CHADEMA na sio Lipumba, Maalim Seif, Zitto Kabwe, Augustino Mrema na wengineo ambao nao vyama vyao havijawahi kupata ushindi pengine kuliko CHADEMA?


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unapima joto?
Kwa kifupi Mbowe is not for sale,is the die hard leader.
Na kwakuwa hatanunuliwa na hao wasiothamini utu wa mtu,bado ana nguvu na hari ya kujenga chama chake.
Wala usiwe na wasiwasi kama atakiongoza maisha,utafika muda nae atangatuka.
Je hujiulizi kwanini Nyerere aliongoza TANU hadi CCM akiwa Mwenyekiti zaidi ya miaka 40 wewe unamkomalia Mbowe mtoto wa jana?
Chadema kina mfumo wake wa uongozi.
 
Huyu tokea aliposikia neno "immediate family members" kutoka kwa Pompeo bàsi anahangaika kwa kila mwanasheria anaulizia kama na yeye yumo. Atakufa kwa stress na pressure!
 
Umepita mulemule
I agree Mwanakijiji...

Kwa kasi ya CHADEMA inavyopoteza members wake especially wa juu...

I guess inatakiwa short term stratergy ya kugeuza upepo ...

Kitu cha tofauti kitakachowavuta Members wapya na Kuretain Members wa zamani...

Nachokifikiria mimi ni Safu ya uongozi kubadilishwa..

Waje watu charismatic,wanaoeza kuinfluence..waje na mawazo Mapya!...

Kukiwa na viongozi wapya na Vision mpya,clear mission..stratergies...

Hapo mta attract Attention kutoka kwa watu wa kawaida...

Otherwise ni sawa na kusuburi embe chini ya mti wa mnazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waongezee sauti hao nguchiro
Mkuu unapima joto?
Kwa kifupi Mbowe is not for sale,is the die hard leader.
Na kwakuwa hatanunuliwa na hao wasiothamini utu wa mtu,bado ana nguvu na hari ya kujenga chama chake.
Wala usiwe na wasiwasi kama atakiongoza maisha,utafika muda nae atangatuka.
Je hujiulizi kwanini Nyerere aliongoza TANU hadi CCM akiwa Mwenyekiti zaidi ya miaka 40 wewe unamkomalia Mbowe mtoto wa jana?
Chadema kina mfumo wake wa uongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
liwalo na liwe , Mwanakijiji ni mfuasi wa Dr Slaa kama vile unavyoweza kuwa wewe na mfanyakazi wako wa ndani , hakuna asichojua kwamba Slaa alijiuza kwa udalali
wa mkewe lakini anataka kuaminisha watu humu kama Slaa aliondoka kumkimbia Lowassa , alipitishwa mlango wa chooni pale Kilimanjaro kwa udhamini wa Mwakyembe , akamtukana Sumaye leo yuko chama kimoja na Sumaye na lowassa mbona hakujiuzulu ubalozi ? haya yote Mnafiki Mwanakijiji anajua leo anakuja na ujinga wake hapa ! kachokoza nyuki .
Kumbe hilo analijua huyu Mzee.. 🙂 ..ndio maana ana chuki na Mbowe..
 
Back
Top Bottom