Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Hapo ndio utaona Kuwa sio Mbowe Tatizo
Tatizo lipo kwa hawa Kibendera wake wasio jua kukosoa
Wameona Mbowe mungu mtu asie kosea wala kukosolewa
Ccm itaondolewa na Kizazi kijacho sio hiki cha Wapuuzi
 
Hapo ndio utaona Kuwa sio Mbowe Tatizo
Tatizo lipo kwa hawa Kibendera wake wasio jua kukosoa
Wameona Mbowe mungu mtu asie kosea wala kukosolewa
Ccm itaondolewa na Kizazi kijacho sio hiki cha Wapuuzi
Kwani na wewe unataka ccm iondolewe !
 
Mkuu naheshimu mawazo yako,ila kama hali iko mnavotuaminisha unadhani ni kipi kinacho muogofya jiwe hadi anahangaika kuzuia mikutano,anawabambika kesi kila uchao wapinzani,wanabaka mchakato wa uchaguzi kama ilivyotokea kwenye serikali za mitaa, anatangaza hadharani kuwa ole wake mkurugenzi amtangaze mpinzani kushinda, utekwaji wa wakosoaji wake na mengine mengi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unadhani jiwe kuzuia mikutano na mbowe kuufyata ndio kuimarika kwa upinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee mwanakijiji umekuwa ukitoa ushauri mzuri kila mara kwa hiki chama mfu.wenye chama Chao wameziba macho na masikio hawaishi kejeli na matusi.
Wenye akili wameondoka wamewaachia mazuzu na manyumbu chama Chao. Sikio la kufa halisikii dawa!

Mwanakijiji angepeleka huo ushauri vyama kama TLP, Chauma, UPDP nk hivyo ndio vinahitaji ushauri ili vinyanyuke. Hao unaosema wana akili kimewashinda nini kuanzisha vyama vyao ili viendelee, wamebaki kuhamia vyama walivyoanzisha wanaume wengine?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.

Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.

India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.

Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.

Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.

Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT
Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!

Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.

Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.

Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!

Binafsi naamini kuondoka kwa Mashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.

Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.

Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.

MM. Mwanakijiji
Ni bahati mbaya conclusion yako inapishana na ukweli katika hoja zako.
 
Uko sahihi kabisa! Mbowe kuwa m/kiti au la, haikuhitaji muda wote huu utadhani ni africa ya miaka ya 70. Tatizo liko kichwani. Malengo ya Mbowe ni yapi ktk siasa? Huyu anafanya siasa ya kibiashara. Kwa kuwa anapata pesa hajali. Wote waliotoka ni watu waliotumainiwa lakini yeye anajidai CHADEMA haiteteleki.

Lipo tatizo la ukabila ambalo ukilitaja wanazizima kama nyuki. Ukweli ni kwamba Wachaga wanaiona CHADEMA kama chama chao. Mbali na walioko ktk uongozi, walioko nje wakiona kabila jingine linasogelea hiki 'chama chao' wanapata taabu na lazima wakupe taabu. Sioni taabu kumuondoa katibu huyu na kuingiza yule, lakini kuna taabu kubwa ukiona katibu mstaafu anahamia chama kingine.
Nilisema wakafuta.
Nahii watafuta
Ila uzuri kabla yakufuta watakuwa wamesoma.
Nihivi Chadema ni chama cha wachaga.
Cyo chama cha siasa.
Ova.
 
Hapo ndio utaona Kuwa sio Mbowe Tatizo
Tatizo lipo kwa hawa Kibendera wake wasio jua kukosoa
Wameona Mbowe mungu mtu asie kosea wala kukosolewa
Ccm itaondolewa na Kizazi kijacho sio hiki cha Wapuuzi
Onyesheni makosa ya Mbowe ili vibendera waone. Upuuzi wenu mnajenga hoja za kipumbavu lengo lenu Chadema isambaratike baada ya mabwana zenu kushindwa kutimiza kile mlichotaka watimize. Ili mjue kama Mbowe akili kubwa Sumaye akawekwa na jiwe ili asikilaumu chama, bado akapigwa chini. Mashinji angepewa ukatibu mkuu alikuwa anakipeleka chama choo cha kike asubuhi tu, wajanja wakamshtukia, mkamtuma Mwambe achukue fomu katika kipindi ambacho mlimpaka mavi Mbowe lakini bado mkapigwa chini na wafia Chadema. Mbinu zenu zote zimeshindwa kwa Mbowe sasa mnaanza kuja na upupu wa akina Mwanakijiji ambao waliishajichokea wanatafuta shibe kwa hata mbinu za kudhoofisha demokrasia nchini. Ni nani aliwahi kuwadanganya kwamba demokrasia na mageuzi ya kweli katika nchi hii yataletwa na chama cha siasa na sio wananchi? Hiyo mifano aliyoitoa Mwanakijiji ni kwa nchi ambazo wananchi ndio wenye maamuzi. Nyie mtu mmoja mmoja mnafanya nini kwa ajili ya maslahi ya nchi hii zaidi ya kudaka makombo mnayorushiwa? Mara ngapi Mbowe ameibua mambo ambayo yalihitaji ushiriki wa wananchi katika kuiadabisha serikali mnanyuti? Mbowe sasa anafanya siasa zenye akili zinazoungwa mkono na wengi kuanzia ndani ya serikali, CCM yenyewe, dini na kwenye jamii. Ukitaka kuamini, subiri watakaporuhusiwa kufanya siasa na hawa wababe wa nchi hii. Wiki moja tu inatosha kuwavuruga. Unapoona tuliowapa dhamana ya kutuongoza wanawazuia wengine kufanya siasa ili wao pekee waonekane kwenye TV usifikiri ni mchezo mchezo..acheni ungese!
 
Hivi ni nini kimeikumba hii akili ya huyu jamaa Mwanakijiji. Sijui amekuwaje siku hizi. He cant think normally. Tatizo kubwa wala hapa home hakai ajue kwa undani mambo yanakwenda vipi. Hoja ya ovyo kabisa kuwahi kutolewa naye.
 
.....alitakiwa kuchukuwa hatua "ngumu" kulinda demokrasia na siyo kumlamba miguu mwenyekiti wa chama tawala atoe "usawa".

Toa mfano wa hiyo hatua ngumu ili ueleweke.
 
Endeleza ukabila!!

Tunajua uko mlengo gani kwa faida ya nani.

Wewe ni sawa na zilpendwa,hakuna wa kukuamini tena.

Uliheshimika kwa hoja zako na si kwa jina lako unalotaka kuendelea kulitumia kwa faida ya unaowatumikia.

Mapandikizi yenu yamefeli sasa mnatapata!!

Wewe na Dr.Mihogo wote wanafiki.
Kumuona mwanakijiji kwamba ni munafiki, hakuondoi ukweli kwamba Mbowe ameharibu CHADEMA na upinzani kwa ujumla. Kwa nini ang'ang'anie nafasi ya m/kiti kwa kisingizio eti amekitoa mbali. Mbali wapi na sasa yuko wapi? Huo ndo mwendo pekee wa CHADEMA na kwamba sasa hakuna nguvu nyingine? Akishabikiwa ki-ukabila anajiona anafaa sana, ukweli unabaki kwamba ni sifa za kijinga kusifiwa na kabila lako, nawe unaamini unaweza ongoza chama kushika nchi ya makabila 120.
 
Hii Chadema acheni kuhangaika nayo zaidi utaambulia matusi. Nafikiri maonyo yametosha, tubakie wapenzi watazamaji hadi tutakapokuja kupata watu serious.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kinachouma ni kwamba tuliihitaji sana CHADEMA ili hata kama CCM wako madarakani, CHADEMA wawe ni darubini yetu. Sasa urafi wa kuiba pesa wanajiona wanafanya vizuri, na kusingizia wanabinywa kisiasa. Huyu akiguswa tu, mijitu inapiga kelele kumulinda kiukabila.
 
Back
Top Bottom