Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Mwizi kabla hujamuita mwizi, yeye ndiye anayekuita mwizi. SS leo wewe wewe unamuita mleta mada mnafiki......!!!!!!, ama kweli tukiwa hai tutaona mengi.

Kibaraka kama wewe Bendera, unayepangiwa la kusema, unapata wapi ubavu wakuweza kumsema mleta mada.

Ni msomi kukushinda, mwanasiasa mpevu, ni mtu inteligent aliyekuzidi wewe na hao wanaokuendesha kwa remote. Hufikii hata kiatu chake

Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseee!!!
Unamjua Mwanakijiji!?
Pole sana kwa kuabudu watu.
 
Dada,huyo mzee mchango wake uko wapi? Labda kumdalalia Slaa.
Hao vijana wa Bavicha hawajui kwamba 2005-2010 Mzee Mwanakijiji ana mchango mkubwa kwenye ukuaji wa CHADEMA akiwa ameshiriki kuandika ilani zote za CHADEMA.

Na ndio awamu hiyohiyo vijana wengi walivutiwa na siasa za upinzani hasa CHADEMA kwa kiasi kikubwa.
 
Onyesheni makosa ya Mbowe ili vibendera waone. Upuuzi wenu mnajenga hoja za kipumbavu lengo lenu Chadema isambaratike baada ya mabwana zenu kushindwa kutimiza kile mlichotaka watimize. Ili mjue kama Mbowe akili kubwa Sumaye akawekwa na jiwe ili asikilaumu chama, bado akapigwa chini. Mashinji angepewa ukatibu mkuu alikuwa anakipeleka chama choo cha kike asubuhi tu, wajanja wakamshtukia, mkamtuma Mwambe achukue fomu katika kipindi ambacho mlimpaka mavi Mbowe lakini bado mkapigwa chini na wafia Chadema. Mbinu zenu zote zimeshindwa kwa Mbowe sasa mnaanza kuja na upupu wa akina Mwanakijiji ambao waliishajichokea wanatafuta shibe kwa hata mbinu za kudhoofisha demokrasia nchini. Ni nani aliwahi kuwadanganya kwamba demokrasia na mageuzi ya kweli katika nchi hii yataletwa na chama cha siasa na sio wananchi? Hiyo mifano aliyoitoa Mwanakijiji ni kwa nchi ambazo wananchi ndio wenye maamuzi. Nyie mtu mmoja mmoja mnafanya nini kwa ajili ya maslahi ya nchi hii zaidi ya kudaka makombo mnayorushiwa? Mara ngapi Mbowe ameibua mambo ambayo yalihitaji ushiriki wa wananchi katika kuiadabisha serikali mnanyuti? Mbowe sasa anafanya siasa zenye akili zinazoungwa mkono na wengi kuanzia ndani ya serikali, CCM yenyewe, dini na kwenye jamii. Ukitaka kuamini, subiri watakaporuhusiwa kufanya siasa na hawa wababe wa nchi hii. Wiki moja tu inatosha kuwavuruga. Unapoona tuliowapa dhamana ya kutuongoza wanawazuia wengine kufanya siasa ili wao pekee waonekane kwenye TV usifikiri ni mchezo mchezo..acheni ungese!
Hao wote ukiowataja walikuja chadema kwa kuletwa kuoewa madaraka na nani?

Usichokijua ni kwamba Mbowe akisoma coment kama hii yako anafurahi sana kwa kutawala mazuzu kama wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I agree Mwanakijiji...

Kwa kasi ya CHADEMA inavyopoteza members wake especially wa juu...

I guess inatakiwa short term stratergy ya kugeuza upepo ...

Kitu cha tofauti kitakachowavuta Members wapya na Kuretain Members wa zamani...

Nachokifikiria mimi ni Safu ya uongozi kubadilishwa..

Waje watu charismatic,wanaoeza kuinfluence..waje na mawazo Mapya!...

Kukiwa na viongozi wapya na Vision mpya,clear mission..stratergies...

Hapo mta attract Attention kutoka kwa watu wa kawaida...

Otherwise ni sawa na kusuburi embe chini ya mti wa mnazi
Hebu eleza sifa za viongozi hao wapya! Hivi kwa mazingira ya sasa ya kisiasa upinzani unawezaje ku-grow! Ni dola vs Upinzani siyo CCM. Hata leo hii CDM M/Kiti akiwa JPM bado kwa ukandamizaji wa sasa wa demokrasia haiwezi kuperform. Muhimu kwa sasa ni kwamba upinzani unabaki unamea moyoni kwa wananchi, siku watasema inatosha basi ndiyo hii nchi itaandika historia. CCM wanapambana wabaki pekee yao katika ulingo wa siasa, wanaminya mawazo mbadala, hili ni [emoji378].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.

Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.

India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.

Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.

Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.

Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT
Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!

Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.

Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.

Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!

Binafsi naamini kuondoka kwa Mashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.

Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.

Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.

MM. Mwanakijiji
Kule Twitter UN's Tunis kina gani?
 
Wale wote waliowahi kuipenda CHADEMA na wanataka mabadiliko ya kweli...waliokataa kuuziwa mbuzi kwenye kiroba.
Kama bado mpo chadema ni sawa. Lakini endapo mko kwingine mfano ccm, je unadhani maoni yako yatachukuliwaje zaidi ya kuwa na madhara na kunufaisha ccm?
 
Mangi cha hangs kulikoni ccm kwa kununua hao jamaa waliosoma bila kuelimika
 
Kati ya mada zilizokosa hoja, mojawapo ni hii. Mwanakijiji analinganisha embe na karanga. Mazingira ya siasa ya Uingereza yanashabihiana na mazingira haya ya kidikteta ya Tanzania ya sasa? Kwa nini Mwanakijiji usimwambie Rais au CCM waige mazingira ya kidemokrasia na uchaguzi huru kama yale ya Uingereza au India? Hapa ndipo inafanya hoja yote ya Mwanakijiji ionekane ni ya kipuuzi.

Hivi utawala huu wa kwetu unaweza kulinganisha na utawala wowote wa watu waliostaaribika Duniani?

Leo hii kama Mbowe angesikiliza maneno yale ya wapuuzi waliokuwa wanamtaka asigombee, tayari muuaji wa demikrasia angekuwa amefanikiwa kama alivyofanikiwa kwa CUF. CHADEMA tayari ingekuwa ni CCMB.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.

Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.

India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.

Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.

Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.

Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT
Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!

Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.

Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.

Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!

Binafsi naamini kuondoka kwa Mashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.

Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.

Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.

MM. Mwanakijiji

Wakati pia umefika kwa serikali kuacha kufanya siasa za kujificha , CCM lazima iweke usawa sababu yenyewe ina tumia vyombo vya serikali kufanya siasa zamani ilikuwa kwa siri lakini sasa hivi ni dhahiri shairi.

Upinzani unausingizia sababu serikali inapambana mno kuua upinzani ili CCM ipate ushindi wa chee hata Mbowe akitoka bado tatizo la msingi liko pale pale. Kwa zaidi ya miaka 7 serkali imepambana kuua CUF kwa kuibeba chadema sasa mission complete inachukua watu wake.

Siasa za Tanzania ni fake na ulaghai mwingi wa CCM kutengeneza upinzani wa uongo ili iendelee kutawala. Upinzani wa kweli unataka palling mtu mbili juu juu hakuna kushikana, upinzani wa bongo TISS, Bunge, Polisi, Mahakama, Jeshi vyote vimekushika na CCM anarusha ngumi za uso
 
Lengo la chama cha upinzani ni kupata wabunge wengi ambao hawana athari zozote kwa chama tawala? Yaani ukipata wabunge 40 au 60 bado unafikiri umefikia lengo... labda uliangalie lengo hasa ni nini.
Mzee Mwanakijiji;
Punguza ujuha kidogo. Unadhani lengo la upinzani ni kupata wabunge 40??!!! Upinzani unajua kuwa kama wangepata wabunge 50/50 ndipo hicho chama dola kingeiona homa ya manjano.
Unaonaje jinsi halmashauri zinazoongozwa na upinzani zilivyopiga hatua hadi mkawanyang'anya mapato?? We kweli umezeeka achana na siasa tu ukale viazi kolomije
 
Huyu nae hana tofauti na Sumaye, Mwambe na Dr. Mashinji. Kuutangazia umma tu kuwa Makonda alijinufaisha na TASAF wakati yeye sio masikini na kumtaka arudishe wakati bado anamkumbatia kwenye nchi ulizofanya reference ilikuwa tayari amejiuzulu!! Hii ni kwa maslahi mapana zaidi ya taifa sio kakikundi ka watu- CDM!!
 
Back
Top Bottom