Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiendelea na operesheni +255 Katiba Mpya katika Kanda ya Kaskazini, kauli kinzani zimeibuka kati ya viongozi wa juu wa chama hicho Mwenyekiti Freeman Mbowe na makamu wake, Tundu Lissu.
Viongozi hao wanaoongoza timu mbili zinazoshiriki operesheni hiyo wamekuwa na kauli tofautikuhusu suala la maridhiano baina ya chama hicho, Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kutofautiana huko kumeibua mijadala ndani na nje ya chama na kuwaacha baadhi ya wanachama wasijue la kufanya.
“Unajua maridhiano yana faida, hata hii mikutano ya hadhara ambayo Lissu anaitumia kusema maridhiano hayajaonyesha matokeo, msingi wake ni maridhiano, wanachama wetu wenye kesi mbalimbali wameachiwa, kesi zenyewe za Lissu zimefutwa,” alisema kiongozi mmoja wa kamati kuu ya chama hicho.
Wakati kigogo huyo akieleza hayo, aliyewahi kuwa mbunge kupitia chama hicho aliyeomba jina lihifadhiwe alisema “maridhiano haya yanaturudisha nyuma sisi. Yanatufanya tuonekana kama tumesalimu amri, ni bora tuendelee na ujenzi wa chama, hawa tunaoridhiana nao si wa kuwaamini sana.”
Hata hivyo, Mbowe kwenye moja ya mikutano wa hadhara ya operesheni +255 mkoani Kigoma alisema wanaodai yeye (Mbowe) na Lissu hawaelewani wanakosea, hilo halipo na wanaendelea kuchapa kazi kama kawaida.
Awali, akiwa Singida, katika mwendelezo wa mikutano yake ya hadhara, Lissu alisema, “kuna maneno mengi ya upatanisho, lakini maridhiano pekee ni upatikanaji wa Katiba mpya, tusipokuwa na Katiba mpya tumeliwa. Maridhiano ambayo hayana ukweli, watu waliumizwa sana lakini hawajaambiwa kwa nini waliumizwa, wala nani aliyeamuru waumizwe wala kufidiwa,” alisema.