PreGE2025 Msimamo wa CHADEMA wa “No reform, no election”, nani yuko nyuma yao anayewapa ujasiri na kusonga mbele?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Aiseee, nani wa kulaumiwa? Viongozi wa dini au waasisi wa Taifa?
 
Jibu ni moja tu, ni wananchi waliochoshwa na serikali ya CCM iliyojaa ghilba,hadaa,ulaghai,ufisadi na ubabe. Hii nyomi inayojitokeza kupokea elimu ya No Reform No Election ni ushahidi wa sababu hiyo.
Je wananchi hao kwa kiasi gani unafikiri wataweza kuzuia uchaguzi kufanyika Oct 2025?
 
Wao ndio wapo mbele na nyuma ni wao wenyewe. Wao ndio wa kwanza wao ndio wenye mbiu yao
 
Kama una connection na mtu yeyote mkubwa TISS mwambie akupe matokeo ya kura ya maoni kuhusu Samia anavyokubalika nchini. Utashangaa. Ndiyo maana hata yeye ana wasiwasi sana, hajiamini.
 
Kama una connection na mtu yeyote mkubwa TISS mwambie akupe matokeo ya kura ya maoni kuhusu Samia anavyokubalika nchini. Utashangaa. Ndiyo maana hata yeye ana wasiwasi sana, hajiamini.
Mkuu sina connection.
Je kwa Tanzania sanduku la kura hutoa rais?
Ingawa kwa asilimia 1,000 naunga mkono katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
NB; sina chama.
 
Unaongelea umma upi?
Uliokacha maadamano kadhaa?
Uliomvunja moyo Mange Kimambi na maandamano ya kipindi kile?
Vitisho tu vya CCM na vyombo vyao vya ulinzi kutishia watu kuandamana lakini katika mioyo ya watanzania chama pendwa ni CHADEMA Hilo halina ubishi
 
Nguvu ya umaaaaaaa! Hakuna kurudi nyuma. NO REFORM NO ELECTION, NO REFORM NO ELECTION AND NO REFORM NO ELECTION.
 
Mm nadhani CHADEMA watashiriki kwenye uchaguzi hata kama Serikali itapuuzia No reform no Election..lkn sasa unajua watakachokisema kwenye kampeni...nikushawish umma kususia kupiga kura..mwanzo mwisho wa kampeni..mpaka kieleweke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…