The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
Hata wewe huna tofauti na hao unaowasema. Ujenzi wa hoja zako tu unaashiria kuwa hujui chochote na unaogelea ktk wimbi la ujinga uleule wa ki - CCM....Wanajukwaa bila shaka ni wa zima wa afya njema.
Wahenga walisema "kuuliza si ujinga"
Hivi msimamo wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wa No Reform No Election ni kitu gani kinawapa nguvu, ujasiri na morali ya kuendelea nao mbele wasibadili gear angani?
Je nani yuko nyuma yao?
Upande wa pili yaani CCM wana vyombo vyote vya dola wana haja gani baadhi yao kuwahofia Chadema?
Maana nikimwangalia Makamu mwenyekiti na Katibu wa Itikadi na Uenezi namna wanavyojibu hoja za Chadema ni kama vile wako katika hali ya kupanic, kwa nini wapanic wakati vyombo vya dola viko chini yao na upinzani hauwezi kuzuia uchaguzi kwa maandamano na Watanzania ni waoga si rahisi kuwaingizia barabarani kwa maandamano kwa asilimia kubwa?
Soma Pia: Tundu Lissu na John Heche watangaza kuipeleka ajenda yao ya "No Reform No Election" nje ya nchi
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Je Chadema awaogopi kwamba wasiposhiriki uchaguzi huu kuanzia mwakani watajikuta si chama kikuu cha upinzani tena?
Ruzuku watakuwa hawapati tena?
Je Chadema kama chama wamefanya tathimini vya kutosha faida za kutokushiriki na kushiriki?
Mimi ni Mtanzania nisiye na chama chochote.
Aidha u - mjinga kwa sababu ni wazi kabisa kuwa huelewi hata maana tu ya "NO REFORMS, NO ELECTION" achilia mbali hoja zinazoibeba na kuitetea kauli mbiu hii ambazo wenzako hawa (i.e CCM na serikali yao) unaowananga wanazijua, wanazielewa na kutambua kwa hakika kabisa kuwa MADAI YA CHADEMA sambamba na HOJA ZAO NI ZA KWELI ZISIZOKUWA NA HATA CHEMBE MOJA YA SHAKA....!
Bahati mbaya tu kwao ni kuwa, wanaogopa kuutazama na kuukabili ukweli ulio mbele ya nyuso zao badala yake wanahangaika na kuteseka hovyo na mwisho wa siku ndiyo maana wanaropoka ropoka hovyo kama njia ya kujilinda...
Sikiliza bwana, ujasiri wa CHADEMA na kusonga kwao mbele, it's simply tu kwa sababu wameishika kweli na YESU KRISTO ktk mafundisho ya Neno lake anasema MKIIJUA KWELI NA KUIKUMBATIA, BASI HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU, TENA SI TU HURU, BALI MTAKUWA HURU KWELIKWELI...!
Wenzako CCM na serikali yao wanatembea ktk UONGO na ULAGHAI mtupu matokeo yake wamekuwa watumwa ktk uongo na ulaghai wao....
Wenzao CHADEMA wanatembea ktk KWELI na HAKI na kwa hiyo nguvu ya Mungu imewafunika na kuwalinda huku wenzao wakihaha na kulemewa na zigo la UONGO na UDANGANYIFU mwingi...!