PreGE2025 Msimamo wa CHADEMA wa “No reform, no election”, nani yuko nyuma yao anayewapa ujasiri na kusonga mbele?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Baada ya katiba mpya kupatikana ndio Hilo litafanyika !Kwa mfumo wa katiba hii lazima kupambana ukuu ubaki kwenye taasisi salama kama CCM!

Ccm inajua namna ya ku regulate mambo yanapoharibika japo sometimes sio kwa njia demokrasia Bali dark arts!!

Nawaza
 
Kweli wewe ni msalaba !!
 
Nadhani ni wao pekee..ni viongozi tu wapo committed na suala la Uchaguzi huru na wa haki ..

Hilo la Mzee wa Anga kuhama, sina taarifa ila ni HAKI yake
 
Ccm wanajua cdm hawawezi kuzuia uchaguzi maana watanzania wanaogopa kipigo cha dola. Ila wanajua uchaguzi utakuwa na wapiga kura wachache, jambo ambalo litaanika ukweli wa kuwa ccm haina uungwaji mkono mkubwa wa wananchi. Wanataka cdm washiriki ili watu wajae vituoni, ili hata wakiiba ionekane wao ndio wanakubalika na watu wengi. Lakini watu wakiwa wachache vituoni, inapunguza hata uhalali wao kwa umma na dunia.
 
Mimi kama mwananchi nipo nyuma yao
 
Sawa mkuu, lakini mara gapi imesemwa kuandikishwa hadi watoto wasio na sifa za kuwa wapiga kura au sehemu nyingine marehemu, je kwenye matokeo watashindwa nini kuzidisha namba za waliopigia kura ccm?
 
Sawa mkuu, lakini mara gapi imesemwa kuandikishwa hadi watoto wasio na sifa za kuwa wapiga kura au sehemu nyingine marehemu, je kwenye matokeo watashindwa nini kuzidisha namba za waliopigia kura ccm?
Kuzidisha idadi wanaweza sana, ukweli vituoni uko wazi watu watakuwa wachache. Ukweli una nguvu kuliko hizo data za kupika.
 
Lakini mkuu wakati wa kampeni nani huamuru askari kufanya ulinzi na usalama kwenye mikutano ya kampeni?
Nani huamuru askari kuzunguka kipindi cha zoezi la upigaji wa kura na hata wakati wa kuhesabu kura?
2020 kabla ya kutangazwa Kura za urais bara na visiwani mbona viongozi wa upinzani Km hayati Maalim Sharif Hamad Seif, Jusa, Mazrui, Mhe Mbowe si walikamatwa na baadhi yao kupigwa na kuteswa na Jusa alipata ulemavu wa muda na wengine kutekwa, je askari walipewa amri kutoka kwa nani?

Magari ya kijeshi na mengine ya JWTZ nasikia Unguja yalikuwepo kila kona hadi huko Tarime je yaliigizwa mtaani kwa amri ya Rais aliye mgombea au IGP au CDF nani?

 
Mfumuko wa bei za bizaa utaleta hili jambo
Wana wasomi watajitahidi kuwatumia ili kudhibiti au?
Vipi bajeti ya mwaka huu maana Trump kawafungia vioo wale wapenda kuzungusha mabakuli na Uingereza inaweza kuwa je bajeti ya mwaka huu 2025/2026 haitakuwa bajeti ya kufunga mkanda kwa raia? Kodi mpya, tozo zaidi, ongezeko la bei fulani kwenye vitu vya msingi?
Ni mwaka wa uchaguzi je bajeti ikiwa ni ya kufunga mkanda raia wataelewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…