Butola
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 2,290
- 758
Kwahiyo wananchi wasubiri mikutano ya hadhara kujua ACT ni chama kikuu mbadala cha upinzani?
Tanzania itakujaje kwanza Kabla ya Tanganyika? Huo Ndio muungano imara kwa maoni na mtazamo wa ACT? Hakika hii ni failure at launch.
Tanzania kwanza, Tanganyika Kabla, nje ya hapo hakuna muungano imara wala legelege.
Again, hizi ni pro active politics, not pre emptive. Mmesubiri miezi Sita kusoma upepo wa Tanganyika, Leo Ndio mnakuja na hoja za serikali Tatu baada ya kuona maoni ya wananchi. Katika mchango wake ndani ya BLK, zitto hakugusia suala la serikali Tatu Bali alikwepa hoja kwa kusema Kwamba haijalishi kuna serikali Ngapi huku akimaanisha Kwamba hata Mbili za sasa zinaweza kudumisha muungano. Huyu ni Mwenyekiti mtarajiwa wa ACT ambae sasa amebadili msimamo na kuegemea kwenye msimamo wa vyama Vinginevyo vyote vya upinzani.
Hoja ya ukawa kufa baada ya katiba mpya pia imewahi jadiliwa na zitto. Ni Kama vile chadema kiliundwa na kufanikiwa kwa misingi ya serikali Tatu. As long as chadema kinaendelea kupigania maslahi ya wananchi, kitaendelea kuwepo na kuzidi kufanikiwa. Ni mafanikio haya Ndio mnataka kubomoa huku Mkiwa hamna lolote kwa wananchi Kama mbadala zaidi ya ombwe lenye faida kwa CCM.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mchambuzi...sikuhizi huoni wala husikii juu ya Chadema...ni haki yako ya msingi kufanya hivyo.
Kwangu mie usinitafutie upande, mie sio mwanachama wala mpenzi wa chama chochote kwa sasa.Sipo ACT na sipo Chadema sio kwa karatasi wala kwa mahaba pia.Hivyo kauli yoyote yangu ni kwa kadri nilivyoisoma mitazamo yao juu ya Muungano na sio kama msemaji wala mwakilishi wa yeyote zaidi ya Butola.
Yawezekana kwako ni kweli kuwa ni Tanzania Kwanza na Tanganyika Kabla, lakini kwa wengi wetu na kwa muundo wautakao UKAWA (ambao kimsingi na mie nautaka) ni Tanganyika na Zanzibar huru kwanza Tanzania shauri yake.Na ninakubali sana hili, kwa lugha ya sasa hakuna namna ya kistaarabu ya kusema sitaki Muungano zaidi ya kuunga mkono serikali tatu kama zilivyo kwenye rasimu, ndio maana ata wanaohitaji Zanzibar huru hawana shida na hilo kwa sababu wanajua kwa kupitia Tanganyika huru na Zanzibar huru automaticaly Tanzania inakufa.
Mie sio msemaji wa Zitto, lakin hujamtendea haki kwa kumwekea maneno ambayo hakuyasema. Zitto hakujadili mfumo gani unafaa bungeni bali alitoa maoni juu ya maridhiano na watu kujiridhisha juu ya wanayoyajadili. Na hakuishia kwenye idadi ya serikali akaenda pia kwenye uhai wa Tanzania ambapo alikiri kuwa ikibaki kama ilivyo kwenye rasimu Tanzania haiwezi kuexist, nukuu isiyo rasmi alisema "ndio maana tupo hapa, tuiboreshe hiyo rasimu kwenye hili".
Na kabla ya bunge lile alishatoa mtazamo wake juu ya muundo wa muungano ambao upo sawa na huu wa ACT, magazeti kadhaa yalitoa ile makala ya Zitto juu ya muundo wa Muungano.So hujamtendea haki kwenye "kufuata upepo wa UKAWA baada ya Bunge la Katiba".
Wananchi wasubiri mikutano kujua kama ACT itakuwa chama kikuu cha upinzani?exactly. Kumbuka Chadema ilikuwepo toka 1992, lakini ilikuwa underground kwa miaka karibu 13 wakati nchi ikiwa chini ya vyama vikuu vya upinzani vya TADEA, DP, NCCR, TLP na baadae CUF. Ni mpaka mwaka 2005 ndipo ilipoanza kuchomoza na kuwa kwenye peak kati ya 2007 na 2012. Hivyo sio ajabu kwa ACT iliyoanza mwaka 2014 kuchukua muda ku take off.
Nakumbuka Mwalimu Nyerere alipata kusema mwaka 1995 kuwa "Chadema ni chama kizuri na kina watu makini lakini viongozi wake si wanasiasa" akirefer Mtei na akina Bob Makani.Lakini ilipopata wanasiasa wakiongozwa na Mbowe Chadema ili take off, vivyovivyo mpaka sasa ACT wanasiasa wake kama wapo basi bado hawajaingia uwanjani rasmi, ebu tuwape muda na muda ndio utaongea kama kinaweza kuja kuwa chama kikuu cha upinzani au la.