Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,193
Nimelisoma tamko nakubaki kujiuliza maswali mengi, kama kuna umakini wa aina yoyote.
1. Tamko hili ni mwendelezo wa matamko waliyotoa UKAWA, CCM(Lembeli, Miwgulu) na wazee (Mark Boman), waandishi wa habari na wanajamii.
Hakuna walichokiongelea ACT kigeni zaidi ya kunukuu watu bila acknowledgement.
2. ACT wameorodhesha matatizo ya BMK. ACT hawajaweka wazi tatizo ni nini.
Wame epuka kusema rasimu ya kujadiliwa ni ya Warioba.
Wamekwepa kusema maoni ya tume ili kutowaudhi CCM kwa kujificha.Hilo ni kuwachanganya watu na wala si kuonyesha njia.
3. Suala la umri si agenda ya ACT. Tumejadiliana jamvini na akina Ben Saanane, MWANAKIjiji, JokaKuu, Jasusi, Mchambuzi , Bongolander, Mag3 n.k. muda mrefu
Tumepingana na akina Ben, leo tunaaminishwa ni jambo geni kabisa eti lina umakini. Mnachokifanya ni kujificha nyuma ya kundi la January na Zitto na agenda yao.
Hatutengenezi katiba ya watu wawili, tunatengeneza katiba ya nchi.
4. Mchambuzi anauliza, iwapo CUF, CDM, NCCR kila mmoja atakuja na madai yanayofanana kuna ulazima wa kufanya hivyo? Nami nauliza, kama ACT wana madai yanayofanana na UKAWA kuna ulazima wa kuja na kitu kile kile.
5. Hoja ya Kitila Mkumbo kuhusu S3 ni mfu.
Kinachojadiliwa ni muundo wa muungano kwanza, ndilo tatizo la kukwama BMK.
Namna gani serikali 3 zitakuwa imara au dhaifu hilo ndilo lipo mbele ya BMK.
Hoja ya msingi ni S3 kwanza. Hayo ya lege lege na imara ni mambo baada ya hoja kuu.Kusema ACT ina hoja imara tusizozijua na tusizozifahamu ni ad hominem
6. Tamko la ACT lilikusudia kueleza msimamo kuhusu BMK na mtafaruku unaoendelea.
Ukiliangalia ni tamko la jumla na hilo halina tatizo hata kama wanadurusu ya wenzao.
Tatizo ni pale Kitila anapoingia katika mkumbo usiolingana naye.
Kitila, katika tamko la jumla ni aibu kuongelea vipengele visivyohusika
Hili tamko, Dr, ni la kiwango kisicholingana na hadhi yako, nakuthibitishia hapa chini.
Soma kifungu hiki
Hadi hapa Kitila na ACT, wanatoa mapenekezo haya Anachronism! Tatizo ni kukwama kwa mchakato si vipengele husika. Mumedai mnapendekeza kukwamua mchakato.
Hili lina uhusiano gani na tatizo lililopo? Irrelevant, tumekwama mchakato hili linahusiana vipi na sehemu ya 7 ya mapedekezo yenu! Here we go! BMK limejadili kanuni, na muundo ndipo lilipokwama.
Halijajadili kiengele hata kimoja kinachohusu mambo ya muungano.
Wapi mnaona suala la gesi na mafuta ni sehemu ya tatizo tulilo nalo?
Hii haina maana yoyote kufuatana na kipengele namba 7 cha tamko lenu.
Tamko ni kukwamua mchakato si mafuta na gesi
Lakini pia mumeshindwa kuelewa.
Tume imeorodhesha matatizo mengi kuhusu muungano kwa pande zote.
Katiba tunayotaka kutengeneza si ya mafuta na gesi, na wala si katiba ya zanzibar.
Kuna matatizo ya Tanganyika.
Mnapochagua kipengele kama na kukifanya sehemu ya kukwamua mchakato, inasikitisha Kitila.
Zaidi ya hapo, gesi na mafuta si mambo ya muungano tena. Zanzibar walishaondoa.
Ningaliwaelewa kama mngeongele uvunjwaji wa katiba, na si ku-appease wznz kwa cheap politics za kitoto namna hii. Hakuna uhusiano na kukwama kwa BMK.
Mnachomeka vipengele kufurahisha watu, Kitila anasema ni tamko makini. Real ! This one!
Na mwisho, Kitila, ukiangalia lugha tu inatia shaka kama unapitia na kuhakiki matamko makubwa 'makini'. Kitila usijeniambia ni typo error!
Ndio maana nakusihi uangalie matamko kama haya, hayalingani na hadhi yako.
Ahsante
Nguruvi3,
Asante sana sana .Yale niliyotarajia kuandika umeniwahi kabisa.
Nakumbuka tulipingana sana kwenye suala la umri na thread zipo na msimamo wangu ukaendelea kubakia ule ule hadi leo
Nimeshangazwa sana idadi ya midahalo eti itajwe kwenye katiba badala ya kuwa suala la kutungiwa sheria au kanuni zitakazoeelekeza tume huru ya uchaguzi iandae midahalo
Last edited by a moderator: