Hoja Hapa sio Kujiunga na ukawa Bali kuunga Mkono msimamo wa ukawa. Ni busara kuacha duplicate resources and efforts Katika suala Zima la kudai katiba itokanayo na wananchi. Tayari vyama vya upinzani vina msimamo wa pamoja juu ya Hilo, sasa ukawa ni upinzani wa wapi, je ni mpinzani wa vyama vya upinzani? Mnachanganya sana wananchi, Kaeni vijiweni msikie mnavyokoroga wananchi.
Msimamo wa ACT sasa unatafsiriwa na wengi Kwamba ni sawa na kuunga Mkono UKAWA. Kinachochanganya na pia kushangaza wananchi Wengi ni je, kwanini ACT wanaendelea kuhangaika kujitofautisha na chadema Katika suala husika Wakati kimsingi Madai ya ukawa (chadema) ni Yale Yale Kama ya ukawa - katiba itokanayo na wananchi hasa Mfumo wa muungano?
Hizi hoja na juhudi za
Kitila Mkumbo kutofautisha msimamo wa ACT vis a vis Chadema kwa hoja Kwamba chadema wanapendekeza serikali Tatu Zenye muungano legelege Wakati ACT wanapendekeza serikali Tatu Zenye muungano imara ni hoja ya kitoto sana. Msingi wa hoja Hapa ni muungano wa serikali Tatu, period. Hayo Ndio wamesema wananchi, Hayo mengine juu ya uimara na ulegelege wa muungano wa serikali Tatu ni masuala ya kujadiliwa bungeni, na hiyo Ndio kazi ya BLK - kuboresha rasimu itokanayo na wananchi.
Cc
Nguruvi3,
Mag3,
JokaKuu,
Jasusi
Sent from my iPhone using JamiiForums