Msimamo wa chama cha ACT-Tanzania na katiba mpya


Mchambuzi...sikuhizi huoni wala husikii juu ya Chadema...ni haki yako ya msingi kufanya hivyo.

Kwangu mie usinitafutie upande, mie sio mwanachama wala mpenzi wa chama chochote kwa sasa.Sipo ACT na sipo Chadema sio kwa karatasi wala kwa mahaba pia.Hivyo kauli yoyote yangu ni kwa kadri nilivyoisoma mitazamo yao juu ya Muungano na sio kama msemaji wala mwakilishi wa yeyote zaidi ya Butola.

Yawezekana kwako ni kweli kuwa ni Tanzania Kwanza na Tanganyika Kabla, lakini kwa wengi wetu na kwa muundo wautakao UKAWA (ambao kimsingi na mie nautaka) ni Tanganyika na Zanzibar huru kwanza Tanzania shauri yake.Na ninakubali sana hili, kwa lugha ya sasa hakuna namna ya kistaarabu ya kusema sitaki Muungano zaidi ya kuunga mkono serikali tatu kama zilivyo kwenye rasimu, ndio maana ata wanaohitaji Zanzibar huru hawana shida na hilo kwa sababu wanajua kwa kupitia Tanganyika huru na Zanzibar huru automaticaly Tanzania inakufa.

Mie sio msemaji wa Zitto, lakin hujamtendea haki kwa kumwekea maneno ambayo hakuyasema. Zitto hakujadili mfumo gani unafaa bungeni bali alitoa maoni juu ya maridhiano na watu kujiridhisha juu ya wanayoyajadili. Na hakuishia kwenye idadi ya serikali akaenda pia kwenye uhai wa Tanzania ambapo alikiri kuwa ikibaki kama ilivyo kwenye rasimu Tanzania haiwezi kuexist, nukuu isiyo rasmi alisema "ndio maana tupo hapa, tuiboreshe hiyo rasimu kwenye hili".

Na kabla ya bunge lile alishatoa mtazamo wake juu ya muundo wa muungano ambao upo sawa na huu wa ACT, magazeti kadhaa yalitoa ile makala ya Zitto juu ya muundo wa Muungano.So hujamtendea haki kwenye "kufuata upepo wa UKAWA baada ya Bunge la Katiba".

Wananchi wasubiri mikutano kujua kama ACT itakuwa chama kikuu cha upinzani?exactly. Kumbuka Chadema ilikuwepo toka 1992, lakini ilikuwa underground kwa miaka karibu 13 wakati nchi ikiwa chini ya vyama vikuu vya upinzani vya TADEA, DP, NCCR, TLP na baadae CUF. Ni mpaka mwaka 2005 ndipo ilipoanza kuchomoza na kuwa kwenye peak kati ya 2007 na 2012. Hivyo sio ajabu kwa ACT iliyoanza mwaka 2014 kuchukua muda ku take off.

Nakumbuka Mwalimu Nyerere alipata kusema mwaka 1995 kuwa "Chadema ni chama kizuri na kina watu makini lakini viongozi wake si wanasiasa" akirefer Mtei na akina Bob Makani.Lakini ilipopata wanasiasa wakiongozwa na Mbowe Chadema ili take off, vivyovivyo mpaka sasa ACT wanasiasa wake kama wapo basi bado hawajaingia uwanjani rasmi, ebu tuwape muda na muda ndio utaongea kama kinaweza kuja kuwa chama kikuu cha upinzani au la.
 

Moja ya kasoro kubwa kwenye mambo yetu ya kisiasa ni kujenga hoja kabla ya jambo na kuishikilia hiyo hoja hata baada ya kupewa hoja mbadala, bila kui-counter hikyo hoja mbadala.

Yaani mnaweza kusema mko serious mnapoleta maoni yenu juu ya ACT kufuata upepo? So what if they are!!!!
Kwa jinsi tamko hilo linavyosema na hasira za wana- CHADEMA juu ya ACT ni wazi kuwa ACT imeleta alternative nzuri kwenye siasa za Tanzania. We call this alternative, INDEPENDENCE.

Angalia maana ya independent parties halafu utuambie kama huwa vinakuja na sera tofauti au a "HYBRID" of policies
Mchambuzi.

KUFUATA UPEPO SIO JAMBO BAYA, NI JAMBO ZURI NA NDIYO WANANCHI WENGI WANAVYOTAKA ..(Rejea maneno ya Prof. Kabudi)
Pre-emptiveness is not necessarily smart. And sidhani kama tunahitaji bogus pre-emptive,top-down, politically motivated and central committee dictated parties like CHADEMA, CUF and CCM anymore.

Mbona nyinyi UKAWA mnasisitiza kufuatwa kwa maoni ya wananchi? What does that mean ? Chama kinachofuata upepo na wanasiasa wanaofuata upepo ndiyo tunaowataka, na siyo chama kinachowatungia sera wananchi na kujiita centrist/leftist/liberals .... who cares??

We want a socialist state, period. How socialist, we can talk about it but that should come from the people and not some power hungry big-bellies calling themselves "central committees". That thing is played-out.

Good job ACT, naipitia katiba yenu and it looks like you got a member over here!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kobello.

Niseme wazi ya kwamba nakubaliana na hoja zako moja kwa moja.

Na ukiwafuatilia vizuri ACT kama chama hawana shida na sera za vyama vingine.

Mfano kama chadema tukichukulie kama kilinganishi chake...act hawana shida wala criticisms za kupingana na chama hiko moja kwa moja...thats why tumeona pale juu kitila mkumbo karespond kwamba kisera vyaweza kulandana ingawa wao wamejaribu kuboresha zaidi.

Kilichowafanya wao kama wao kuamua kutoka ndani ya chama hiko na kuasisi act ni ubakaji wa demokrasia unaofanyika ndani ya chadema na uuungu mtu ndani ya chama hiko huku wakijizatiti katika kufanya demokrasia magilini.

So far sion kwa nin uwepo wa act as a political party uwanyime usingiz hawa ndugu wa upande wa pili.

Kama ni kweli wao wanaamin ya kwamba act ni kibaraka wa ccm kama walivyokatuaminisha ya kwamba cuf ni ccm b ambayo leo hii hawa hawa chadema wameungana nao hawa cuf bila hata ya kutujuza ni lini cuf hii iliacha kuwa ccm b...au ni lin ndoa baina ya cuf na ccm ilivunjika...so wauache muda wenyewe utaamua??hofu yao ya nin..

Kwann act iwanyime usingiz.

Kama wana uhakika ya kwamba hawa act ni vibaraka waachane nao waendelee kujenga chama chao.

Kila mtu awe huru kunadi sera na kufanya siasa zake.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi...sikuhizi huoni wala husikii juu ya Chadema.Ni uchaguzi wako.
Mwananchi yoyote mtaka mabadiliko appreciates the role of chadema towards that end. Chadema imerudisha sana CCM Katika Mstari, chama kilijisahau sana na athari zake kwa wananchi zikawa wazi. For the past 5 years, msimamo wangu ni Kwamba bila ya chadema madhubuti, CCM makini haiwezekani. Umakini wa CCM umeongezeka Katika suala Zima la kuangalia maslahi ya umma ingawa bado kuna kazi kubwa sana ya kufanyika. All in all, credit goes to chadema iliyokuwa ni ya kina kitila, zitto, mwigamba et al.

Butola yeye sio mwanachama wa ACT Wala CCM Wala chadema Bali yeye ni "independent" ambae anavutiwa na siasa za ACT, siku akiamua kutumia Haki yake ya kikatiba Kupiga kura, ataipigia ACT, je Nipo sahihi Katika hili?

Mbona kimsingi unaegemea kwenye "Dhana ya Tanzania kwanza? Tanganyika Kabla"?


Msingi na Malengo ya hoja ya zitto ilikuwa kukwepa kuji commit Katika suala la serikali Tatu, that's the bottom line.

Nikuulize, je hii kauli yako Kwamba zitto alitoa mtazamo wake binafsi muda mrefu Kabla ya BLK Kuanza, mtazamo ambao ni sawa na wa ACT miezi sio chini ya saba baadae, inatueleza wananchi kitu gani?

Sijaelewa msingi wa hoja yako Hapa ni nini, je ni ACT kujifananisha na chadema au? Ndio haya haya nayo sema Kwamba ACT is nothing than a hybrid party.

Kitila alishamteua zitto kuwa Mwenyekiti wa ACT nje ya utaratibu, na kwa njia Ile Ile ambayo yeye kitila na wenzake walikuwa wakilalamika kwenye waraka wao wa Siri Kwamba uongozi chadema ni wa kuchaguana, Nguruvi3 alijadili Hilo suala kwa kina. Ni Jambo lililo wazi Kwamba zitto ndiye Mwenyekiti mtarajiwa wa ACT, Kabla hata ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa chama hicho kutangazwa na wanachama kuchukua fomu za kugombea.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Jamani,huu mjadala ni mzuri sana...wale wenzangu na mimi ukiona hauna cha kuchangia ni bora uwe msomaji kama mimi.

Maana ukileta viroja vyako badala ya hoja basi ujuwe hawa magwiji tunaowasoma hapa wote wataondoka na thread yenyewe itajifia. Huu ni mtizamo wangu.. Mzeemwanakijiji na Pasco tunasubiri maoni yenu.
 
Last edited by a moderator:
I hear you !
Ndipo hasa hoja ilipo, kuwa S3 zimeongelewa na Zitto hapa JF na magazetini 3 years ago. Zimekuwa ni sera ya CDM chini ya ushauri wa Kitila Mkumbo zaidi ya miaka 10.

Leo Kitila anaposema UKAWA wanataka S3 legelege, na ACT wana proposal ya S3 imara, proposal tusiyoijua inashangaza.
Hawana katiba wala sera, bado wanaongozwa na ad hoc committee.

Ukisoma tamko, proposal yao ya S3 ni kuondoa gesi na mafuta katika muungano. Ni kuruhusu ZNZ ijiunge na mashirika ya kimataifa.
Tujiulize hayo ndiyo matatizo ya muungano?

Wanajribu cheap politics za kuwapendeza wznz na si kutoa ufumbuzi wa tatizo.
Sisi tunasema, Hell no! Kikwete amewafariji wazanzibar hadi wamevunja katiba.

Kila wanachotaka wanapewa, na bado kuna matatizo ya muungano. ACT wanasema tatizo ni mafuta na gesi, ambayo Kikwete ameruhusu kupitia katiba ya 2010 na si suala la muungano tena.

Unaweza kuona jinsi walivyo opportunists wa kutumia hali iliyopo katika publicity zao. Na juu ya hilo, bado publicity yao ni hovyo.
Huwezi kusema eti suluhu ya BMK ni kuruhusu znz kuwa na mafuta na gesi, au kushiriki katika taasisi za kimataifa.

Kwamba ACT wameliangalia tatizo zima la BMK na kuja na suluhu flimsy kama hiyo.
Sababu kkubwa ya kuwa rampant and erratic ni kutokana na ukweli kuwa wao ni opportunists tu, nothing more nothing less

Ni hawa walituaminisha katika waraka kuwa wao wana akili kubwa na wanaongozwa na akili ndogo hivyo walitaka mabadiliko.real!
 
Nakubaliana na wewe kwenye hili, japo ni muhimu kutambua kuwa Chadema nayo kama ilivyo CCM inaweza kupoteza umadhubuti, hivyo kuilea kama mtoto anayedekezwa ni kuiua.


Butola yeye sio mwanachama wa ACT Wala CCM Wala chadema Bali yeye ni "independent" ambae anavutiwa na siasa za ACT, siku akiamua kutumia Haki yake ya kikatiba Kupiga kura, ataipigia ACT, je Nipo sahihi Katika hili?
Ni independent, na siamini kwenye kupiga "kura" kwa "mafungu" hivyo hupiga kura kwa "mtu zaidi" kuliko "chama" nikitambua kuwa kama nchi tuna uhaba mkubwa wa "viongozi makini na wa kweli" katika siasa zetu. Hii ni kwa vyama vyote, sio CCM tu.Ni tatizo la kitaifa.

Mbona kimsingi unaegemea kwenye "Dhana ya Tanzania kwanza? Tanganyika Kabla"?
Unless kama Tanzania Kwanza ina maana ata ikifa shauri yake ilmuradi ilishawahi kuwepo.


Hapana, hujamtendea haki kutafsiri hivi. Labda kama una tatizo na yeye mwenyewe na sio alichokiongea.

Kwa mtu asiye bias angetambua kuwa alichofanya Zitto haikuwa kukwepa hoja bali kuonyesha "uongozi" pale ambapo Bunge lilikosa uongozi wa kulirudisha kwenye mstari. Wakati wabunge wengi na viongozi wa makundi yaliyopo bungeni wakijiingiza kwenye malumbano na kutoyapa maridhiano nafasi, Zitto alichofanya ni kujaribu kuwarudisha kwenye njia sahihi, na ndio busara ya uongozi inavyotaka hasa wakati wa utengano. Na hiki ndicho tunachomlaumu leo Kikwete kwenye hotuba yake ya ufunguzi. Hivyo tumpongeze na sio kumkebehi kwa kuyafanya ambayo wakubwa wale walishindwa kufanya.
Sijaelewa msingi wa hoja yako Hapa ni nini, je ni ACT kujifananisha na chadema au? Ndio haya haya nayo sema Kwamba ACT is nothing than a hybrid party.

Sababu ya kurefer historia ya Chadema ilikuwa kujibu hoja yako hii
Mwananchi Kwahiyo wananchi wasubiri mikutano ya hadhara kujua ACT ni chama kikuu mbadala cha upinzani? .
Wananchi wataipaje nafasi ACT kuwa chama kikuu cha upinzani kabla hakijafanya mikutano na kuonana na wananchi??ni wananchi ndio watakaoamua baada ya kuwasikiliza, muda utaongea.

Umeendelea kutoitendea haki ACT, last time I checked Kitila alikuwa ni mmojawapo tu wa wanachama wa ACT na hana mamlaka ya kumteua mtu kuwa Mwenyekiti, sasa ni lini Zitto amekuwa Mwenyekiti wa ACT??kwenye hili labda tuupongeze tu uongozi wa sasa wa ACT kwa kulinda na kuheshimu maoni ya wanachama wake ata kama yanahatarisha nafasi ya viongozi waliopo madarakani. Maana kwenye vyama vingine vya upinzani kauli hiyo ingetafsiriwa kuwa ni usaliti na adhabu yake pamoja na kupakwa matope na kuzushiwa kashfa ingekuwa ni kufukuzwa uanachama.
 
Well, in some cases it is better that we agree to disagree. Sikubaliani na hoja ya Profesa Kabudi ya siasa za msimu, yaani upepo ukivuma kinakuja chama kinapata umaarufu na upepo ukiisha chama kinakuwa useless. Moja kati ya ukosaaji wangu mkubwa wa CHADEMA at some point ni kuona kuwa kilikuwa ni kama anti corruption, ambacho msingi wake ni scandal za CCM. Lakini baadae labda wenyewe walijua kuwa chama cha siasa ni zaidi ya upinzani na ukosoaji, ni kujiandaa kutawala pia.Unasema we want to be a socialist country?....mkuu hapa ungejisemea mwenyewe, mimi kwa mazingira ya Tanzania sioni kama hiyo kitu inafaa.Nataka kujua ACT ni alternative kivipi? what does the party stands for, what are policies of ACT, long term policies not hand to mouth approach that they have started with, what is their principle ideology? Sidhani kama tutakuwa tunajitendea haki kama chama hiki kitakuwa cha wenye njaa na uchu wa madaraka tu, na hakina lolote jipya kinacholeta kwa Tanzania. Nauliza maswali haya ili kujua kama kweli hiki ni chama halisi ay ni scum tuSo inawezekana kuwa ACT ni scum, au itakuwa ni chama kama Sasa mkuu unanishangaza unaposema ndio unasoma katiba yao, halafu unakipongeza ACT, unakipongeza kwa lipi?Who are the founders of this party? ni wale rejects wa CCM, CUF na CDM? wanatuletea nini kipya kwenye siasa za Tanzania,m kama sio makapi kutoka kwenye vyama hivyo? Mkuu naomba unelewe vizuri sio kama nakishambulia ACT nataka tuangalie picha kubwa, na tujue kama kweli ACT ni Chama au ndio yale yale vya vyama ambavyo ni miradi ya watu.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna kitu kama siasa za msimu, labda sielewi unachomaanisha. kuhusu Chadema kuwa anti-corruption, hiyo pia ni sera ya CCM,NCCR na CUF na sidhani kama kuna chama ambacho siyo anti-corruption. All they did was get the inside scoop on some dirt that politicians tend to cover. Once the government took care of some agents, the flow of information kinda stopped and the "nzi's" sopped buzzing. Thats common, mabbe you got hyped but I knew it was gonna end soon.

Kwani watanzania tunataka kujenga taifa gani? Si taifa ambalo rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi equally? Now what u call that? ... Nisingependa sana twende huko kwa sababu haya mambo ya left and Right are so overrated. But watanzania tunataka kujenga taifa la kisoshalisti, tuna asili hiyo kwa hiyo hilo halina ubishi. Ila unaweza bisha ukitaka, but you will be wasting your time.

ACT ni alternative nzuri kwa sababu inafuata upepo kama ulivyosema. Wanataka serikali tatu, lakini yenye powerful central government. Hii ndiyo issue inayozungumziwa, prove kwamba serikali ya muungano itakuwa na nguvu kama ambavyo Warioba alivyowaomba CCM wa-prove kwamba wataondoaje Tanganyika kuvaa "Kanzu" ya muungano. Let's discuss this na siyo kushikilia tu serikali tatu.


Speaking of the founders, (hehehe). All the rest are CCM "Rejects" as yo'd like to call'em. So whats your point brah?
If I differ with let's say CUF on mkataba and got expelled from it, will that mean my point is not benign among Tanzanians? Can't I find Tanzanians who will join me and start an anti-mkataba party for instance? ... You really need to straighten this up cos ... you know, I don't get it.


Naipongeza ACT for the style of leadership that they have shown. A brand new-party that took a stance based on what other parties and the citizenry as a whole stood for and came up with a couple of fine-tuned points. Whats wrong with that? You don't have to pick your "Extreme" in politics. Sometimes politics is just compromising.
Give us Three governments, with a strong central government siyo hii iliyopendekezwa. Hivi ukiwaambia wazanzibari wasianzishe ubalozi somewhere halafu wakakataa utawafanya nini? How can you lobby the permanent members of the security council when you don't have anything. No gas, no oil, no grip on international trade .... shoosh, you won't even own highways!! and you call yourself a central government? Trying to control a big ass country like Tanganyika? ... You gotta be kidding me mayn!

Kuhusu kuishambulia ACT, I REALLY WOULDN'T BE SUPRISED, kwa sababu inaonyesha ni watu ambao mnatofautiana nao kisiasa, giving yourselves high fives while making bogus points on this forum. But thats cool, ila tu ujue kuwa hoja hujibiwa kwa hoja na mimi sijaona hoja inayokufanya uwaone majamaa kuwa ni matapeli. Points wamezimwaga ila tu, nataka nijue wataiimarishaje serikali ya muungano? Kwa sababu there's a lot of people who can't wait to see Tanzania gone.

Mwisho, ndiyo kwanza nimeanza kuisoma katiba ya ACT leo, baada ya Mchambuzi kuni-tag kwenye hii thread na kwa sababu nam-respect na kumu-admire jamaa ikabidi niitupie (Pia ina heading nzuri, siyo ya kimipasho) na nimependa sana jinsi walikvyojieleza. I can't believe that I didn't see it when it came.
 
Last edited by a moderator:
Sikubaliani na uhuru wa kukatisha kabeti,ukiwa ubunge wako umedhaminiwa na chama cha siasa basi ubunge wako utakoma pale ambako chama hicho kitakuchanganya uanachama.Hii itasaidia sana kuleta discipline kwenye vyama na kuzuia kuzalisha watu kana zito
Hilo wazo najua limetoka kwa zitto bila shaka! hii ni njaa tu za wabunge wetu wanaondekeza maslahi yao binafsi ! la msingi hapo ni wananchi kupewa rungu la kuwathibiti wabunge tu!full stop
 
Hilo wazo najua limetoka kwa zitto bila shaka! hii ni njaa tu za wabunge wetu wanaondekeza maslahi yao binafsi ! la msingi hapo ni wananchi kupewa rungu la kuwathibiti wabunge tu!full stop

Mkuu hii ndio point ninayoeleza hapa. Noana kuwa hatuna mfumo wenye nidhamu, sasa vyama vinaibuka tu kama uyoga. Ni ujinga kuanzisha chama kwa ajili ya mtu fulani kuwa mwenyekiti halafu agombee urais, chama cha namna hiyo ni ujinga tu. Ina maana kipo kwa ajili ya kukidhi matwkwa ya mwanasiasa mmoja au wawili.
 
Kitila Mkumbo, Mwl.Kaijage,

..mapendekezo ya tume ya Warioba ni kwamba mambo ya muungano yawe 7.

..sasa naomba kujua ACT inapendekeza mambo mangapi yawe ya muungano.

..pia ningefurahi kama mngetueleza ni mambo gani mnapendekeza yawe ya muungano.

..zaidi, ACT imependekeza kuwe na mawaziri wakuu wa Tanganyika na Zanzibar.

..ningependa kujua hao mawaziri wakuu wa watapatikana kwa utaratibu gani.

cc Mchambuzi, Kobello, Nguruvi3, Pasco, Bongolander
 

Mkuu hiki chama kwa maoni yangu it is just a scum. sidhani kama ni chama chenye sera na itikadi yoyote. Naona ni chama chenye lengo la kumpatika ZZK uenyekiti. Hiyo ndio sera na itikadi kuu ya ACT.

Kutokana na kuwa ni chama kilichoanzishwa hivi karibuni sidhani kama "wanachama" watakuwa wamekaa na kuwa na maoni ya chama kuhusu mambo hayo, sana sana atakuwa ni mtu mmoja anayetoa maoni kutokana na upepo unavyoenda.
 
Washauri act waungane na ukawa kudaikatiba mpya mkiwa pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…