Msimamo wa nchi za Afrika juu ya suala la Urusi na Ukraine ni jambo dogo sana linalopaswa kuongozwa na kanuni, sio maslahi ya nchi zetu

Hapana mkuu mimi nipo lingusenguse, Ruvuma ila ninasoma sana latest information za bara letu la Africa, yes Malema ni mwizi na mwanasiasa mbabaishaji tu,President H&H of Zambia ndio shining star ya sasa ,1ZWK =145TSHS,Ghana cedi yao inazidi kuporomoka against usd, it's only productivity, reform na max export tunayatakiwa kuyafanya nchi yetu ili nasi tununue diesel kwa 15BWP,just imagine unaenda Oil com na kutumia 15TSH kupata 1L of Diesel!sio 3300.00tshs
Na huyu president wa Zambia yuko makini sana. Atawafikisha Zambia mbali. Hafanyi mambo kwa kudanganya ili kusifiwa kama ilivyokuwa kwa yule wa kwetu hapa; mtanikumbuka, tunapigwa sana, kumbe yeye ndie anatupiga huku anapuliza!
 
Unajua kinachosikitisha sana ni nini? Unaweza kusikia Malema kachaguliwa kuwa Raisi wa Bondeni. Unaona signature yangu hapo chini? Ndio maana siku nyingi sana nimesema hili wazi; Changamoto kubwa sana inayoyakabili mataifa masikini duniani na kufanya washindwe kuendelea ni nyingi ya akili ndogo kupewa mamlaka makubwa, kwa njia ya kura au kuteuliwa.
Unfortunately ndio ukweli ambao umeuhitimisha hapo, viongozi wetu wengi hapa Africa wapo kwa masilahi yao, wengi wame take advantage baada ya kuvuruga mfumo wa elimu na kuingiza mifumo ya kuzalisha mazuzu, wapo tayari kuitisha chaguzi kuu ili kuonyesha kuwa wanaendesha demokrasia kumbe ni washenzi wakubwa, but it's not all lost hapo Lesotho kuna new sherrif in town, hope's naye huyu ata shake vitu pale Maseru
 
Na huyu president wa Zambia yuko makini sana. Atawafikisha Zambia mbali. Hafanyi mambo kwa kudanganya ili kusifiwa kama ilivyokuwa kwa yule wa kwetu hapa; mtanikumbuka, tunapigwa sana, kumbe yeye ndie anatupiga huku anapuliza!
Yes mkuu mwenyewe nimeitembelea sana hii nchi ,inabadilika na kuwa ya kidemokrasia zaidi na uchumi umekua, Ile brutality ya vyombo vya dola imepungua mno, kwenye barabara zao ni check points tu ndizo zilizobaki (Tanzania tulikua nazo hizi),na ndio pit stops za kupumzikia na kulala ,zipo safe kabisa (za jeshi na police),ningekua na uwezo ningechuka mazuzu wa humu hadi pale kapiri mposhi waone je ni trunks ngapi zinakuja nakonde na ngapi zinapitiliza na zimebeba nini
 
Nawashangaa sana viongozi wetu. Eti wengi wanasema hawataki kuchagua upande kati ya Urusi na Ukraine, hata kwenye mambo ya kura wanajitoa. Huu ni uoga na unafiki usiokubalika kwa viongozi wa nchi za Afrika.

Ndio maana nimesema siku zote Nyerere alikuwa mtu mwenye busara sana, alisimamia principles, sio urafiki au maslahi ya Tanzania

NInaamini kwa dhati katika hili Nyerere angemlaani Putin katika suala la hii vita. Alishasema, kwamba hii mipaka ya nchi zetu, japokuwa mara nyingine hatuipendi, lakini hatutalazimisha ibadilishwe. Kuwekwa kwake kwa sasa ni jambo la kihistoria na acha ibaki hivyo kwa ajili ya amani na ujirani mwema, japo labda hatuipendi.

Kwa hivyo basi, katika suala la vita kati ya Urusi na Ukraine, madai ya Putin kwamba Ukraine inawaonea watu wenye asili ya Urusi ndani ya Ukraine kwa hiyo wanavamia Ukraine kuwakomboa watu wenye asili ya Urusi, ni ujinga uliopita kikomo na usiopaswa kukubalika na kiongozi yeyeote mwenye akili timamu. Ni sawa na sisi Tanzania, leo hii tuwaambie Wakenya kwamba maeneo ya Kajiado wanayoishi Masai wa Kenya yako nyuma kimaendeleo kwa hiyo tutaingia Kenya kuchukua maeneo haya kwa kuwa Wamasai wa huko ni sehemu ya Wamasai wa Tanzania na wanapaswa kufikiriwa na kuendelezwa kama sehemu nyingine za Kenya, halafu tuivamie Kenya kijeshi. Unaona ujinga huo?

Sasa hapo ndipo Africa Union ilipaswa isimamie bila woga na kujali maslahi. Kina Malema kule South Africa wanasema tutam-support Putin na Warusi katika huu mgogoro kwa kuwa Urusi ilituunga mkono kwenye freedom strugle. Stupid stinking thinking! Kumbuka Nyerere alichosema pia, hatukuwaunga mkono ANC kwa sababu ni weusi kama sisi, bali kwa sababu walikuwa wanabaguliwa na hatupendi ubaguzi wa rangi kwa kuwa unakiuka haki za binadamu.

Sasa Nyerere alimaanisha nini? Kwamba itakuwa ujinga sana kwa Raisi wa Tanzania, siku ANC, chama cha weusi wengi kule South Africa, wakianza kunyanyasa wazungu na kuwabagua, Tanzania kuendelea kuwaunga mkono kwa sababu tu ANC ni chama cha weusi wenzetu. Ikiwa wazungu hao Afrika Kusini leo hii wakibaguliwa na haki zao za kibinadamu kukiukwa na ANC na watu weusi wa South Afrika, na wazungu hao wakaanzisha mapambano ya kujikomboa, itabidi Tanzania tuwa-support na kuwapa kambi zote hapa nchini zilizokuwa za ANC kuwa kambi zao za kupigania uaswa nchini Afrika Kusini.

Kumbuka pia, kwa nini Nyerere aliunga mkono Biafra kule Nigeria, japo tulikuwa marafiki wa serikali ya Nigeria? Kwa nini Nyerere alivunja uhusiano na Uingereza, Israel na Ujerumani wakati fulani licha ya misaada mikubwa tuliyokuwa tunapata toka kwao? NI suala la principles, sio maslahi ya nchi au urafiki. Haya ndio mambo yalifanya Nyerere aheshimike sana duniani. Rational and fairness principles.

Leo hii jirani yako anakupa lift kwenda kazini, siku akishutumiwa kuwafanyia unajisi watoto, utamtetea au kukaa kimya kwa sababu amekuwa akikupa msaada? Labda wewe kama una tatizo la mtindio wa ubongo.

Sasa hawa viongozi wetu hapa Afrika, kama wangejua jinsi ya kusimamia principles badala ya maslahi, hili suala la Urusi na Ukraine is a no brainer - wangetoa tamko la kumlaani Putin. Huwezi kusema mbona Marekani walivamia sijui Iraq, Libya nk. Utakuwa unatukumbusha tu jinsi usivyo na msimamo kwa sababu wakati Marekani wakivamia Iraq na Libya ulipaswa kulaani kwa nguvu zote pia. Na two wrongs do not make a right. So African leaders, stop your nonsensical approach to the Russia-Ukraine debacle. You are just proving what Trump is always accusing us of - something about shit hole countries!
Hii post imeandikwa vizuri na ukishawishika tu kwa namna tu ilivyo pangiliwa basi huna budi kushawishika. Ila mimi bado sijaweza kushawishika hata.

Kwa sababu mgogoro wa Urusi vs Ukraine ni tofauti sana na migogoro ya weusi na wazungu wakati wa S. Africa Apatheid, ni tofauti na mgogoro wa Biafra huko Nigeria, ni tofauti sana na mlinganisho ulioufanya wa wamasai wa Kenya vs wamasai wa Tanzania kwamba kama si sawa kwa Tanzania kuivamia kenya kukomboa wamasai wa Kajiado basi haiwezi kuwa sawa Urusi kuivamia Ukraine.

Ndiyo si sawa kwa Urusi kuivamia Ukraine iwapo tu utaisoma historia ya Urusi na Ukraines kuanzia mwaka 2022 vita ilipoanza. Ila huu mgogoro ni zaidi ya Urusi kuivamia Ukraine kwa lengo la "land grab" kama wamagharibi wanavyoubrand kwenye media. Lakini je makubaliano ya Urusi na NATO kuhusu usalama wa Urusi ilikuwa miaka ya 1990? Ilikuwa kwamba, yeah Urusi ipo radhi kuachia zile nchi zilizokuwa chini ya USSR "baltic states" kuwa huru lakini asingependa kuona zinakuwa militarized states armed with western weapons zinazotishia usalama wa Urusi yenyewe. Hapo ni baada ya figisu za Marekani kuhakikisha USSR inavunjika. Lakini nini kilichotokea baadaye? NATO kwa ulevi wao wa pesa wakazidi kuzimega nchi zilizokuwa sehemu ya USSR, na Putin akawa akiwacheki na kujesemea moyoni hiiii! Miaka ya 2000 minongono ilipoanza kwamba hata Ukraine ikikaa sawa kwenye mambo yake ya ndani ya kisiasa inaweza kujiunga na NATO Urusi ikasema sasa baasi.

Kwa background hii complicated sasa sisi waafrika tulaani nini hapa kati ya Ukraine na Mrusi? Sera ya kutofungamana na upande wowote ni sera baab kubwa kwenye situation kama hii.
 
Unfortunately ndio ukweli ambao umeuhitimisha hapo, viongozi wetu wengi hapa Africa wapo kwa masilahi yao, wengi wame take advantage baada ya kuvuruga mfumo wa elimu na kuingiza mifumo ya kuzalisha mazuzu, wapo tayari kuitisha chaguzi kuu ili kuonyesha kuwa wanaendesha demokrasia kumbe ni washenzi wakubwa, but it's not all lost hapo Lesotho kuna new sherrif in town, hope's naye huyu ata shake vitu pale Maseru
Tunafanya uchaguzi ili kuwaridhisha wakubwa kuwa tuna utawala wa kidemokrasia, lakini ukweli ni kwamba chaguzi zetu huwa si za kidemokrasia wala za haki, ni show off tu zinazotumia advantage ya wapiga kura wetu ambao asilimia kubwa ni semi-illiterates wa mambo ya siasa na uongozi bora. Tukimaliza uchaguzi walioshinda wanajipongeza kwa kushinda kwa asilimia kubwa huku wakijua wazi kwamba ushindi wao haukuwa halali hata kidogo, lakini hilo haliwanyimi usingizi!
 
Hii post imeandikwa vizuri na ukishawishika tu kwa namna tu ilivyo pangiliwa basi huna budi kushawishika. Ila mimi bado sijaweza kushawishika hata.

Kwa sababu mgogoro wa Urusi vs Ukraine ni tofauti sana na migogoro ya weusi na wazungu wakati wa S. Africa Apatheid, ni tofauti na mgogoro wa Biafra huko Nigeria, ni tofauti sana na mlinganisho ulioufanya wa wamasai wa Kenya vs wamasai wa Tanzania kwamba kama si sawa kwa Tanzania kuivamia kenya kukomboa wamasai wa Kajiado basi haiwezi kuwa sawa Urusi kuivamia Ukraine.

Ndiyo si sawa kwa Urusi kuivamia Ukraine iwapo tu utaisoma historia ya Urusi na Ukraines kuanzia mwaka 2022 vita ilipoanza. Ila huu mgogoro ni zaidi ya Urusi kuivamia Ukraine kwa lengo la "land grab" kama wamagharibi wanavyoubrand kwenye media. Lakini je makubaliano ya Urusi na NATO kuhusu usalama wa Urusi ilikuwa miaka ya 1990? Ilikuwa kwamba, yeah Urusi ipo radhi kuachia zile nchi zilizokuwa chini ya USSR "baltic states" kuwa huru lakini asingependa kuona zinakuwa militarized states armed with western weapons zinazotishia usalama wa Urusi yenyewe. Hapo ni baada ya figisu za Marekani kuhakikisha USSR inavunjika. Lakini nini kilichotokea baadaye? NATO kwa ulevi wao wa pesa wakazidi kuzimega nchi zilizokuwa sehemu ya USSR, na Putin akawa akiwacheki na kujesemea moyoni hiiii! Miaka ya 2000 minongono ilipoanza kwamba hata Ukraine ikikaa sawa kwenye mambo yake ya ndani ya kisiasa inaweza kujiunga na NATO Urusi ikasema sasa baasi.

Kwa background hii complicated sasa sisi waafrika tulaani nini hapa kati ya Ukraine na Mrusi? Sera ya kutofungamana na upande wowote ni sera baab kubwa kwenye situation kama hii.
Unaona basi, na wewe unafanya kosa lile lile.

NI hivi, twende kwenye basics. Mpaka kati ya Urusi na Ukraine umekuwa wapi siku zote? Na je huu mpaka unakuwa sio halali kwa kuwa tu Ukraine anataka kujiunga na NATO?

Achilia mbali ubabe wa NATO sijui, hilo ni suala jingine halihusiki hapa. Issue ni kwamba siku zote Urusi anatambua mpaka kati yake na Ukraine, hadi siku Ukraine anapoonyesha interest na NATO. Kabla ya Raisi wa sasa wa Ukraine, kulikuwa na Raisi wa Ukraine kipenzi wa Putin. Kwa nini Putin hakuongelea juu ya mipaka wakati huo ambapo ilikuwa rahisi zaidi kwake? Ndio maana nimekwambie tungalie principles, mipaka tunaweza kuwa hatuipendi lakini ipo ilipo.

Ni sawa na Malawi kusema mpaka kati yake na Tanzania ni ukingo wa Ziwa Nyasa, baada ya mafuta kuonekana yapo Ziwa Nyasa. Huo ni upuuzi.
 
Tunafanya uchaguzi ili kuwaridhisha wakubwa kuwa tuna utawala wa kidemokrasia, lakini ukweli ni kwamba chaguzi zetu huwa si za kidemokrasia wala za haki, ni show off tu zinatotumia advantage ya wapiga kura wetu ambao asilimia kubwa ni semi-illiterates wa mambo ya siasa na uongozi bora. Tukimaliza uchaguzi walioshinda wanajipongeza kwa kushinda kwa asilimia kubwa huku wakijua wazi kwamba ushindi wao haukuwa halali hata kidogo, lakini hilo haliwanyimi usingizi!
Kwa sababu pia hata hao unaowaita "wakubwa" tunaotaka kuwaridhisha kwenye chaguzi zetu siyo watu innocent, hawana clean agenda kwenye hizo democracy shows, na wanapotaka jambo lao lifanikiwe watalifanikisha hata bila kuheshimu hizo kanuni za demokrasia. Tunalazimisha kuishi kwa kanuni walizoweka watu wengine?
 
Umaskini wa akili umefanya viongozi wa Afrika kuwa waoga.
 
Kwa sababu pia hata hao unaowaita "wakubwa" tunaotaka kuwaridhisha kwenye chaguzi zetu siyo watu innocent, hawana clean agenda kwenye hizo democracy shows, na wanapotaka jambo lao lifanikiwe watalifanikisha hata bila kuheshimu hizo kanuni za demokrasia. Tunalazimisha kuishi kwa kanuni walizoweka watu wengine?
Lakini sisi ndio tunawapa sababu. Kama Nyerere alivyosema, ni watu wenye akili chafu wanageuka kumwangalia mwanamke alievaa nusu uchi. Sasa kwa nini katika tawala zetu tunakuwa tumevaa nusu uchi? Tunaponyanyasa watu, tunapokuwa mafisadi wa kupokea rushwa kwenye mikataba, ni wazi tutawavutia hawa wakubwa kwa kuwa wanaona fursa katika namna ya ovyo ovyo tunavyoendesha nchi zetu. Unavaa nusu uchi halafu wanaume wenye akili chafu wakikufuata unalalamika, eboo!
 
Unaona basi, na wewe unafanya kosa lile lile.

NI hivi, twende kwenye basics. Mpaka kati ya Urusi na Ukraine umekuwa wapi siku zote? Na je huu mpaka unakuwa sio halali kwa kuwa tu Ukraine anataka kujiunga na NATO?

Achilia mbali ubabe wa NATO sijui, hilo ni suala jingine halihusiki hapa. Issue ni kwamba siku zote Urusi anatambua mpaka kati yake na Ukraine, hadi siku Ukraine anapoonyesha interest na NATO. Kabla ya Raisi wa sasa wa Ukraine, kulikuwa na Raisi wa Ukraine kipenzi wa Putin. Kwa nini Putin hakuongelea juu ya mipaka wakati huo ambapo ilikuwa rahisi zaidi kwake? Ndio maana nimekwambie tungalie principles, mipaka tunaweza kuwa hatuipendi lakini ipo ilipo.

Ni sawa na Malawi kusema mpaka kati yake na Tanzania ni ukingo wa Ziwa Nyasa, baada ya mafuta kuonekana yapo Ziwa Nyasa. Huo ni upuuzi.
Unadhani mambo ni black.and white kama unavyotaka yawe? Katika mgogoro kati ya Israeli na Palestina principle inasemaje na Marekani yupo upande upi? Kama tukifata kanuni na basics, kanuni ni kutofungamana na upande wowote kwenye migogoro isiyotuhusu. Nyerere alijihusisha sana kwenye migogoro inayotuhusu.

Of course hakuna kiongozi wa Tanzania ya sasa mwenye calibre ya Nyerere lakini walau kwenye hili la Ukraine na Mrusi - aidha kwa woga au kwa sababu zinginezo -- wapo sahihi kutojihusisha kwenye mgogoro usiotuhusu.
 
Ndio, mambo yanatakiwa kuwa black and white. Kwani tulipovunja uhusiano na Israel hatukuona USA wako wapi? Sasa tutamlaani USA kwa kupendelea upande wa Israel, lakini haina maana hatutashirikiana na USA katika mambo ambayo anafanya sawa. Kumlaani Urusi kwa kuvamia Ukraine sio maana kwamba tumsuse. Kwa nini watu hamuelewi haya mambo rahisi hivi? Tatizo ni nini hasa?

Yaani wewe umesoma hapa ulichoelewa ni kwamba tukimlaani Putin tunamuunga mkono USA ambae anamuunga mkono Israel katika kuwanyanyasa Wapelestina? Hee, imbombo ilipo jifo na lori na mafikifiki kuelewesha watu

Mgogoro wa ubaguzi South Afrika ulituhusu kwa kuwa waliobaguliwa walikuwa weusi kama sisi? Pole sana.
 
Tunafanya uchaguzi ili kuwaridhisha wakubwa kuwa tuna utawala wa kidemokrasia, lakini ukweli ni kwamba chaguzi zetu huwa si za kidemokrasia wala za haki, ni show off tu zinazotumia advantage ya wapiga kura wetu ambao asilimia kubwa ni semi-illiterates wa mambo ya siasa na uongozi bora. Tukimaliza uchaguzi walioshinda wanajipongeza kwa kushinda kwa asilimia kubwa huku wakijua wazi kwamba ushindi wao haukuwa halali hata kidogo, lakini hilo haliwanyimi usingizi!
Hilo haliwanyimi using izimwe kwa sababu hakuna push back kutoka kwa hawa illiterate waliotawaliwa na uzuzu mwingi, na huhitajiki kwenda mbali humu kwenye JF mada za ngono, udaku na mpira (unaoshangiliwa kwa mafanikio mfu),wengi watachangia na kuusoma ila ukiongelea kuwa after more than 60yrs ya kujitawala kuna mikoa lami bado ni ndoto kubwa kwao,maji Safi pale mpwapwa ni shida, maji Safi na salama pale Ilemela ni shida wakati few meters kuna ziwa kubwa lenye fresh water
 
Nawashangaa sana viongozi wetu. Eti wengi wanasema hawataki kuchagua upande kati ya Urusi na Ukraine, hata kwenye mambo ya kura wanajitoa. Huu ni uoga na unafiki usiokubalika kwa viongozi wa nchi za Afrika.

Ndio maana nimesema siku zote Nyerere alikuwa mtu mwenye busara sana, alisimamia principles, sio urafiki au maslahi ya Tanzania

NInaamini kwa dhati katika hili Nyerere angemlaani Putin katika suala la hii vita. Alishasema, kwamba hii mipaka ya nchi zetu, japokuwa mara nyingine hatuipendi, lakini hatutalazimisha ibadilishwe. Kuwekwa kwake kwa sasa ni jambo la kihistoria na acha ibaki hivyo kwa ajili ya amani na ujirani mwema, japo labda hatuipendi.

Kwa hivyo basi, katika suala la vita kati ya Urusi na Ukraine, madai ya Putin kwamba Ukraine inawaonea watu wenye asili ya Urusi ndani ya Ukraine kwa hiyo wanavamia Ukraine kuwakomboa watu wenye asili ya Urusi, ni ujinga uliopita kikomo na usiopaswa kukubalika na kiongozi yeyeote mwenye akili timamu. Ni sawa na sisi Tanzania, leo hii tuwaambie Wakenya kwamba maeneo ya Kajiado wanayoishi Masai wa Kenya yako nyuma kimaendeleo kwa hiyo tutaingia Kenya kuchukua maeneo haya kwa kuwa Wamasai wa huko ni sehemu ya Wamasai wa Tanzania na wanapaswa kufikiriwa na kuendelezwa kama sehemu nyingine za Kenya, halafu tuivamie Kenya kijeshi. Unaona ujinga huo?

Sasa hapo ndipo Africa Union ilipaswa isimamie bila woga na kujali maslahi. Kina Malema kule South Africa wanasema tutam-support Putin na Warusi katika huu mgogoro kwa kuwa Urusi ilituunga mkono kwenye freedom strugle. Stupid stinking thinking! Kumbuka Nyerere alichosema pia, hatukuwaunga mkono ANC kwa sababu ni weusi kama sisi, bali kwa sababu walikuwa wanabaguliwa na hatupendi ubaguzi wa rangi kwa kuwa unakiuka haki za binadamu.

Sasa Nyerere alimaanisha nini? Kwamba itakuwa ujinga sana kwa Raisi wa Tanzania, siku ANC, chama cha weusi wengi kule South Africa, wakianza kunyanyasa wazungu na kuwabagua, Tanzania kuendelea kuwaunga mkono kwa sababu tu ANC ni chama cha weusi wenzetu. Ikiwa wazungu hao Afrika Kusini leo hii wakibaguliwa na haki zao za kibinadamu kukiukwa na ANC na watu weusi wa South Afrika, na wazungu hao wakaanzisha mapambano ya kujikomboa, itabidi Tanzania tuwa-support na kuwapa kambi zote hapa nchini zilizokuwa za ANC kuwa kambi zao za kupigania uaswa nchini Afrika Kusini.

Kumbuka pia, kwa nini Nyerere aliunga mkono Biafra kule Nigeria, japo tulikuwa marafiki wa serikali ya Nigeria? Kwa nini Nyerere alivunja uhusiano na Uingereza, Israel na Ujerumani wakati fulani licha ya misaada mikubwa tuliyokuwa tunapata toka kwao? NI suala la principles, sio maslahi ya nchi au urafiki. Haya ndio mambo yalifanya Nyerere aheshimike sana duniani. Rational and fairness principles.

Leo hii jirani yako anakupa lift kwenda kazini, siku akishutumiwa kuwafanyia unajisi watoto, utamtetea au kukaa kimya kwa sababu amekuwa akikupa msaada? Labda wewe kama una tatizo la mtindio wa ubongo.

Sasa hawa viongozi wetu hapa Afrika, kama wangejua jinsi ya kusimamia principles badala ya maslahi, hili suala la Urusi na Ukraine is a no brainer - wangetoa tamko la kumlaani Putin. Huwezi kusema mbona Marekani walivamia sijui Iraq, Libya nk. Utakuwa unatukumbusha tu jinsi usivyo na msimamo kwa sababu wakati Marekani wakivamia Iraq na Libya ulipaswa kulaani kwa nguvu zote pia. Na two wrongs do not make a right. So African leaders, stop your nonsensical approach to the Russia-Ukraine debacle. You are just proving what Trump is always accusing us of - something about shit hole countries!
Hao NATO Us-led walivyovamia LIBYA na kumtoa Ghadafi ni haki? Siwalaumu viongozi wa Africa kuwa kimya ni vyema wakakaa kimya kwa sababu hata kipindi cha Nyerere Waziri Mkuu Kawawa, tulikuwa Non Allied, unalikumbuka hilo?
 
Umeisoma vizuri Minsk Agreement? Kufeli kwake? Na hii hali inayoendelea kwa sasa?
Kwa kifupi, Putin ndio rightful leader kwenye hii dunia iliyojaa udhalimu, udanganyifu wa kimawazo na kimtazamo na utegemezi wa Magharibi, vikwazo vya kiuchumi alivyowekewa Urusi ni elimu tosha kwa sisi tuliopo barani Afrika (achana na viongozi) kujitafakari juu ya rasilimali tulizonazo kwenye kuzalisha na kuacha rushwa. Tuna Gas tuna makaa ya mawe nk
 
Hao NATO Us-led walivyovamia LIBYA na kumtoa Ghadafi ni haki? Siwalaumu viongozi wa Africa kuwa kimya ni vyema wakakaa kimya kwa sababu hata kipindi cha Nyerere Waziri Mkuu Kawawa, tulikuwa Non Allied, unalikumbuka hilo?
Nimeshasema, Afrika tulipaswa kulaani kwa nguvu zote uvamizi wa USA na NATO wa Libya, Iraq nk. lakini tutakuwa wajinga na walevi ikiwa hatutalaani uvamizi wa Urusi kwa Ukraine kwa kuwa USA nao walivamia Libya na Iraq. Na kama unasema tusiwalaani Urusi kwa sababu hiyo na wewe ni mjinpa kama hao viongozi wa Afrika kama kina Malema. Hamjui mnachokisema. Jirani yako atakupa lift kwenda Kariakoo, na hilo litafanya umtetee au usilaani matendo yake ya kunajisi watoto mtaani kwako siku akikamatwa kwa hilo kosa, au ukiona amenajisi mtoto wa mtu ambae huko nyuma nae alinajisi mtoto wa mtu mwingine. Sasa huo ni mtindio wa ubongo
 
Nawashangaa sana viongozi wetu. Eti wengi wanasema hawataki kuchagua upande kati ya Urusi na Ukraine, hata kwenye mambo ya kura wanajitoa. Huu ni uoga na unafiki usiokubalika kwa viongozi wa nchi za Afrika.

Ndio maana nimesema siku zote Nyerere alikuwa mtu mwenye busara sana, alisimamia principles, sio urafiki au maslahi ya Tanzania

NInaamini kwa dhati katika hili Nyerere angemlaani Putin katika suala la hii vita. Alishasema, kwamba hii mipaka ya nchi zetu, japokuwa mara nyingine hatuipendi, lakini hatutalazimisha ibadilishwe. Kuwekwa kwake kwa sasa ni jambo la kihistoria na acha ibaki hivyo kwa ajili ya amani na ujirani mwema, japo labda hatuipendi.

Kwa hivyo basi, katika suala la vita kati ya Urusi na Ukraine, madai ya Putin kwamba Ukraine inawaonea watu wenye asili ya Urusi ndani ya Ukraine kwa hiyo wanavamia Ukraine kuwakomboa watu wenye asili ya Urusi, ni ujinga uliopita kikomo na usiopaswa kukubalika na kiongozi yeyeote mwenye akili timamu. Ni sawa na sisi Tanzania, leo hii tuwaambie Wakenya kwamba maeneo ya Kajiado wanayoishi Masai wa Kenya yako nyuma kimaendeleo kwa hiyo tutaingia Kenya kuchukua maeneo haya kwa kuwa Wamasai wa huko ni sehemu ya Wamasai wa Tanzania na wanapaswa kufikiriwa na kuendelezwa kama sehemu nyingine za Kenya, halafu tuivamie Kenya kijeshi. Unaona ujinga huo?

Sasa hapo ndipo Africa Union ilipaswa isimamie bila woga na kujali maslahi. Kina Malema kule South Africa wanasema tutam-support Putin na Warusi katika huu mgogoro kwa kuwa Urusi ilituunga mkono kwenye freedom strugle. Stupid stinking thinking! Kumbuka Nyerere alichosema pia, hatukuwaunga mkono ANC kwa sababu ni weusi kama sisi, bali kwa sababu walikuwa wanabaguliwa na hatupendi ubaguzi wa rangi kwa kuwa unakiuka haki za binadamu.

Sasa Nyerere alimaanisha nini? Kwamba itakuwa ujinga sana kwa Raisi wa Tanzania, siku ANC, chama cha weusi wengi kule South Africa, wakianza kunyanyasa wazungu na kuwabagua, Tanzania kuendelea kuwaunga mkono kwa sababu tu ANC ni chama cha weusi wenzetu. Ikiwa wazungu hao Afrika Kusini leo hii wakibaguliwa na haki zao za kibinadamu kukiukwa na ANC na watu weusi wa South Afrika, na wazungu hao wakaanzisha mapambano ya kujikomboa, itabidi Tanzania tuwa-support na kuwapa kambi zote hapa nchini zilizokuwa za ANC kuwa kambi zao za kupigania uaswa nchini Afrika Kusini.

Kumbuka pia, kwa nini Nyerere aliunga mkono Biafra kule Nigeria, japo tulikuwa marafiki wa serikali ya Nigeria? Kwa nini Nyerere alivunja uhusiano na Uingereza, Israel na Ujerumani wakati fulani licha ya misaada mikubwa tuliyokuwa tunapata toka kwao? NI suala la principles, sio maslahi ya nchi au urafiki. Haya ndio mambo yalifanya Nyerere aheshimike sana duniani. Rational and fairness principles.

Leo hii jirani yako anakupa lift kwenda kazini, siku akishutumiwa kuwafanyia unajisi watoto, utamtetea au kukaa kimya kwa sababu amekuwa akikupa msaada? Labda wewe kama una tatizo la mtindio wa ubongo.

Sasa hawa viongozi wetu hapa Afrika, kama wangejua jinsi ya kusimamia principles badala ya maslahi, hili suala la Urusi na Ukraine is a no brainer - wangetoa tamko la kumlaani Putin. Huwezi kusema mbona Marekani walivamia sijui Iraq, Libya nk. Utakuwa unatukumbusha tu jinsi usivyo na msimamo kwa sababu wakati Marekani wakivamia Iraq na Libya ulipaswa kulaani kwa nguvu zote pia. Na two wrongs do not make a right. So African leaders, stop your nonsensical approach to the Russia-Ukraine debacle. You are just proving what Trump is always accusing us of - something about shit hole countries!
Usihadaike na hao Magharibi wanaokuambia Hashimu kumuoa Juma ni haki na ni sawa ila Hashimu kumuoa Husna na Halima ni haramu.
 
Nimeshasema, Afrika tulipaswa kulaani kwa nguvu zote uvamizi wa USA na NATO wa Libya, Iraq nk. lakini tutakuwa wajinga na walevi ikiwa hatutalaani uvamizi wa Urusi kwa Ukraine kwa kuwa USA nao walivamia Libya na Iraq. Na kama unasema tusiwalaani Urusi kwa sababu hiyo na wewe ni mjinpa kama hao viongozi wa Afrika kama kina Malema. Hamjui mnachokisema. Jirani yako atakupa lift kwenda Kariakoo, na hilo litafanya umtetee au usilaani matendo yake ya kunajisi watoto mtaani kwako siku akikamatwa kwa hilo kosa, au ukiona amenajisi mtoto wa mtu ambae huko nyuma nae alinajisi mtoto wa mtu mwingine. Sasa huo ni mtindio wa ubongo
Ndugu kabla ya hiyo Operation Zelenskky kaitwa wazungumze kashupaza shingo, anafanya makosa ya wazi wazi na kama Mrusi asingemuwahi 24/02 mambo yangekua tofauti
Amini nakwambia Putin ni raisi mzuri, mwenye moyo safi ila Zelenskky na hao mshirika wake hasa USA wanaisogeza hii operation mbele zaidi.
Kaka hukatazwi kumkanya mdogo wako akishupaza shingo.
 
Usihadaike na hao Magharibi wanaokuambia Hashimu kumuoa Juma ni haki na ni sawa ila Hashimu kumuoa Husna na Halima ni haramu.
Hilo ndilo ninalosema ni lojiki ya watu wenye mtindio wa ubongo. Kama Magharibi wakisema Hashimu kumuoa Juma ni haki wakati sio haki, sema hivyo. Na kama Husna kumuoa Halima sio haki, sema hivyo pia. Sasa kama wewe utasema Hashimu kumuoa Husna si haramu kwa kuwa Magharibi walisema Hashimu kumuoa JUma ni haki wakati sio haki, una tatizo kichwani.
 
Si ndio wanachokuambia kila siku na kufundisha watoto darasani, mzee mimi ndio nina mtindio au wao...
Kaka soma Minsk Agreement uje hapa bhana achana na longolongo za BBC, Washington Post.
 
Ndugu kabla ya hiyo Operation Zelenskky kaitwa wazungumze kashupaza shingo, anafanya makosa ya wazi wazi na kama Mrusi asingemuwahi 24/02 mambo yangekua tofauti
Amini nakwambia Putin ni raisi mzuri, mwenye moyo safi ila Zelenskky na hao mshirika wake hasa USA wanaisogeza hii operation mbele zaidi.
Kaka hukatazwi kumkanya mdogo wako akishupaza shingo.
Hapa hatupo kuangalia uzuri wa Putin au Zelenshhy. It does not matter kama raisi wa Urusi ni Lenin au Putin au Gorbachev, na yule wa Ukraine ni Zelenckky au sijui nani. Ndio maana nikasema ni suala la kanuni. Sasa kama huelewi maana ya kanuni, au principles kwa kiingereza, basi kaa kimya. Kaongeze elimu.
 
Back
Top Bottom