Nawashangaa sana viongozi wetu. Eti wengi wanasema hawataki kuchagua upande kati ya Urusi na Ukraine, hata kwenye mambo ya kura wanajitoa. Huu ni uoga na unafiki usiokubalika kwa viongozi wa nchi za Afrika.
Ndio maana nimesema siku zote Nyerere alikuwa mtu mwenye busara sana, alisimamia principles, sio urafiki au maslahi ya Tanzania
NInaamini kwa dhati katika hili Nyerere angemlaani Putin katika suala la hii vita. Alishasema, kwamba hii mipaka ya nchi zetu, japokuwa mara nyingine hatuipendi, lakini hatutalazimisha ibadilishwe. Kuwekwa kwake kwa sasa ni jambo la kihistoria na acha ibaki hivyo kwa ajili ya amani na ujirani mwema, japo labda hatuipendi.
Kwa hivyo basi, katika suala la vita kati ya Urusi na Ukraine, madai ya Putin kwamba Ukraine inawaonea watu wenye asili ya Urusi ndani ya Ukraine kwa hiyo wanavamia Ukraine kuwakomboa watu wenye asili ya Urusi, ni ujinga uliopita kikomo na usiopaswa kukubalika na kiongozi yeyeote mwenye akili timamu. Ni sawa na sisi Tanzania, leo hii tuwaambie Wakenya kwamba maeneo ya Kajiado wanayoishi Masai wa Kenya yako nyuma kimaendeleo kwa hiyo tutaingia Kenya kuchukua maeneo haya kwa kuwa Wamasai wa huko ni sehemu ya Wamasai wa Tanzania na wanapaswa kufikiriwa na kuendelezwa kama sehemu nyingine za Kenya, halafu tuivamie Kenya kijeshi. Unaona ujinga huo?
Sasa hapo ndipo Africa Union ilipaswa isimamie bila woga na kujali maslahi. Kina Malema kule South Africa wanasema tutam-support Putin na Warusi katika huu mgogoro kwa kuwa Urusi ilituunga mkono kwenye freedom strugle. Stupid stinking thinking! Kumbuka Nyerere alichosema pia, hatukuwaunga mkono ANC kwa sababu ni weusi kama sisi, bali kwa sababu walikuwa wanabaguliwa na hatupendi ubaguzi wa rangi kwa kuwa unakiuka haki za binadamu.
Sasa Nyerere alimaanisha nini? Kwamba itakuwa ujinga sana kwa Raisi wa Tanzania, siku ANC, chama cha weusi wengi kule South Africa, wakianza kunyanyasa wazungu na kuwabagua, Tanzania kuendelea kuwaunga mkono kwa sababu tu ANC ni chama cha weusi wenzetu. Ikiwa wazungu hao Afrika Kusini leo hii wakibaguliwa na haki zao za kibinadamu kukiukwa na ANC na watu weusi wa South Afrika, na wazungu hao wakaanzisha mapambano ya kujikomboa, itabidi Tanzania tuwa-support na kuwapa kambi zote hapa nchini zilizokuwa za ANC kuwa kambi zao za kupigania uaswa nchini Afrika Kusini.
Kumbuka pia, kwa nini Nyerere aliunga mkono Biafra kule Nigeria, japo tulikuwa marafiki wa serikali ya Nigeria? Kwa nini Nyerere alivunja uhusiano na Uingereza, Israel na Ujerumani wakati fulani licha ya misaada mikubwa tuliyokuwa tunapata toka kwao? NI suala la principles, sio maslahi ya nchi au urafiki. Haya ndio mambo yalifanya Nyerere aheshimike sana duniani. Rational and fairness principles.
Leo hii jirani yako anakupa lift kwenda kazini, siku akishutumiwa kuwafanyia unajisi watoto, utamtetea au kukaa kimya kwa sababu amekuwa akikupa msaada? Labda wewe kama una tatizo la mtindio wa ubongo.
Sasa hawa viongozi wetu hapa Afrika, kama wangejua jinsi ya kusimamia principles badala ya maslahi, hili suala la Urusi na Ukraine is a no brainer - wangetoa tamko la kumlaani Putin. Huwezi kusema mbona Marekani walivamia sijui Iraq, Libya nk. Utakuwa unatukumbusha tu jinsi usivyo na msimamo kwa sababu wakati Marekani wakivamia Iraq na Libya ulipaswa kulaani kwa nguvu zote pia. Na two wrongs do not make a right. So African leaders, stop your nonsensical approach to the Russia-Ukraine debacle. You are just proving what Trump is always accusing us of - something about shit hole countries!
Kwanza, maamuzi, hasa ya kisiasa siyo rahisi kama tunavyofikiria. Mimi ninachojuwa maamuzi ya namna hiyo kuna wakati yanafuata principle kuna wakati hayafuati kabisa principle. Kwa maana nyingine tusikimbilie kuilaani Urussi kwa principle peke yake.
Ni kweli Urussi ni kama amevamia Ukraine, lakini kila mtu anajuwa kisa na chanzo cha hili. Wafuasi wa siasa za dunia wanajuwa wazi, baada ya kusambaratika Urrusi kulikuwa na makubaliano yenye nia ya kuhakikisha Urussi haizungukwi na NATO hii ikiwa na maana nchi yoyote inayoingia NATO/EU inahatarisha usalama wa Urussi. Sote tunajuwa bifu kati ya Magharibi na Urussi.
Msimamo wa TZ kuhusu hili mimi nauafiki. Huko nyuma msimamo huu ulikuwa wa nchi zisizofungamana na upande wowote (East or West).
Ningependa kukubali kufuata principle ni kitu kizuri, lakini usiwe wewe tu unakuwa principled wengine hawaishi hivyo. Nitoe mfano kwa nchi ya Marekani. Marekani wao hawako principled na hawafuati principle isipokuwa pale tu principles zinainufaisha. Marekani kila siku inapiga kelele juu ya haki za binadamu za nchi zingine, lakini wao hawajioni kama wakiukaji wa haki hizo nyumbani kwao na nje. Na kila mahali Marekani imejiwekea kinga. Kwa mfano Mmarekani, wanasiasa wao, askari wao hawawajibiki kwenye mahakama ya "The Hague", lakini wakati huohuo wanataka nchi zingine zote ziwajibike isipokuwa wao. Hasa hapo wanafuata principle gani.
Kila mara tunasikia kelele zao kuhusu ukiukwaji haki za binadamu kwa mataifa ya nje, kitu ambacho ni kizuri, lakini ingekuwa vizuri zaidi wawe principled, kwa maana nao wanapokuwa na matatizo kama hayo wawajibike. Chukuwa mfano wa Iraqi, Afghanistan, Palestine ambako kumekuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu nyingi, lakini askari wao wana kinga. Kilichotokea au kinachotokea Ukraine ni sawa na yale yaliyotokea Palestine, Lebanon, Vietnam, Korea, Iraqi, Afghanistan, na kwingineko ambako Marekani iliyenda kupigana na kukimbia kwa aibu maana hakuna sehemu yoyote waliposhinda, mara nyingi kwenda kwao huko kulizigawa nchi hizo kuwa nchi mbili au tatu bila ridhaa.
Mmarekani siku zote anaamini kwenye interest zake at the expense of interest za nchi nyingine. Kwao kama kitu kina maslahi kwao basi hapo hakuna cha principle. TZ nayo inatakiwa iangalie ni wapi kuna faida kwetu sisi kama TZ, siyo kufuata principle kama vipofu. Hata kuendesha na kuisimamia familia yako, panapokuwa na tatizo siku zingine unatakiwa kwenda nje ya box, na hapo ndiyo unaweka principle pembeni na kuangalia kipi chenye maslahi kwa familia.
Maisha yetu binadamu tunakumbwa na kitu kama "kuchukuwa maamuzi magumu" na wakati mwingine maamuzi magumu ni pamoja na maamuzi yanayokinzana na convetional wisdom au principle. Najuwa wengi wetu humu JF tuna dini tunazofuata, uwe wislamu, mkristo, dini asilia, n.k. tuna misingi inayotukataza ushirikini na kuamini na kutumia njia au nguvu za giza. Ukweli ni kuwa hata hao staunch muslims, christians, born again kuna wakati wnapata shida au matatizo wanamuomba Mungu lakini hawapati majibu wanayotegemea. Ikifikia hapo wengi hukimbilia nguvu za giza kuona kama huko itawezekana! Wakristo, Waislamu, na walokole wangapi walikwenda kunywa kikombe cha babu Loliondo. Kwani hawa hawakuwa principled Christians/ Muslims. Mpaka rais wetu alienda kupata kikombe cha babu.
Kwa kifupi, binadamu hawezi kuishi na kutenda kwa principle peke yake. Principles zipo kufuatwa lakini siyo kuzifuata blindly. Msimamo wetu kuhusu Ukraine ni vizuri usifungamane na upande wowote. Kwanza hao Ukraine ni wabaguzi na vita ilipoanza wanafunzi wa Kitanzania walipata shida saana, sioni kwa nini tuwapige tafu. Hata Yesu alitumwa kutuokoa, lakini mateso yalimzidi akasahau kilichomleta duniani na kumuomba Mungu Baba ikiwezekana kikombe (mateso) kimpite.