Msimamo wa Polepole: Sitavaa barakoa hata kama nyie wote mnavaa barakoa

Msimamo wa Polepole: Sitavaa barakoa hata kama nyie wote mnavaa barakoa

Msimamo hadi raha!! Siyo yule akitishiwa kidogo analazimisha watu wote kwenye vikao vyake wavae barakoa!!. Kakuta waarabu hawavai naye anaacha kuvaa!!
Akirudi bongo anataka watu wavae ili wamuunge mkono kupata mikopo
 
Barakoa sio uoga, hata licha ya Covid kuna magonjwa ya kupumuliana kama Homa ya ini au kifua kikuu. Mbona wewe unatumia neti au Condom kwani ni muoga?? Kujikinga sio uoga ni kuwalinda wengine tu ambao unaweza waambukiza magonjwa.
Hayo magonjwa unayosema yalikuwepo siku zote. Kisha kuvaa kondom na kutumia neti ni uoga unaoletwa na maradhi husika, kama isingekuwa hivyo hizi net na condom zisingetumika.
 
Mbona alikua anatumia moyo wa bandia tena umetengenezwa na Beberu!! Kwanini asingeacha uoga na kutegemea moyo wake pekee ujisukume?
Ndio maana aliwagomea kwenda tena kubadilisha huko na akatengeneza kitengo kama hicho muhimbili.
 
Thubutu!! achanje nani? siyo Polepole ninayemfahamu!! Katikati ya watu wote wenye barakoa anadunda kwa uhuru bila barakoa na ana haki na uhuru wote!!
Wewe unakaa na polepole muda wote? Mnakula wote? Mnalala pamoja?
 
Barakoa sio uoga, hata licha ya Covid kuna magonjwa ya kupumuliana kama Homa ya ini au kifua kikuu. Mbona wewe unatumia neti au Condom kwani ni muoga?? Kujikinga sio uoga ni kuwalinda wengine tu ambao unaweza waambukiza magonjwa.

Elimu nchi hii inahitajika zaidi. Mtu anashangilia mtu mwingine kutovaa barakoa. Seriously…
 
Ukipewa jina basi linaathiri sana maisha yako. Huwezi mkuta mtu anaitwa TATU akawa wa kwanza hata siku moja.
Duuh jf Ina watu ..!!kwahiyo yeye anajifunza polepole ikifika 2030 ndo atagundua corona ipo na kuvaa barakoa sio suala la kuwa na msimamo wa kijinga..
 
Kwenye suala la kuvaa barakoa Balozi Polepole kashindwa kumwakilisha Mh Rais huko nchini Malawi.
 
Kuvaa au kutokuvaa ni uamuzi binafsi wa mtu
 
Polepole ni muumini mwenzangu wa kutokuvaa barakoa. Amenifurahisha kutunza msimamo wake mbele ya wenyeji wake wote waliovaa barakoa. Safi sana!!

View attachment 2263246
Huyu dogo umpende usimpende lakini calibre yake ndio inayomlinda. Vijana kama hawa wanatunzwa kwa kazi za baadae! Ukiona ukiharibu unatupwa hata machakani ujue you are not "one of them".

Huyu usikute hata wakubwa wakisema hawamtaki huko kwenye corridor wanaweka viunzi muacheni! Pamoja na spana zake lakini "hasugui benchi".
 
Hata mimi nashangaa balozi anavunja protokali za kidiplomasia. Inaelekea hajui wajibu na kazi za balozi.
Protokal ipi kavunja? Hebu iweke hapa!

Unafikiri Polepole ni ana ubongo wa kunguni kama nyie?
 
Watu wenye matatizo yakiafya yanayoweza kuathiri upumuaji kama vile asthma,selimundu (sickle cell),matatizo ya moyo n.k. hawatakiwi kuvaa barakoa 😷😷😷
 
Barakoa sio uoga, hata licha ya Covid kuna magonjwa ya kupumuliana kama Homa ya ini au kifua kikuu. Mbona wewe unatumia neti au Condom kwani ni muoga?? Kujikinga sio uoga ni kuwalinda wengine tu ambao unaweza waambukiza magonjwa.
Homa ya ini ni ugonjwa wa kupumuliana?
 
Back
Top Bottom