Msimamo wangu kuhusu Ongezeko la Posho kwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba - Makonda

Paul Makonda

Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
97
Reaction score
186
Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba ieleweke kwamba sijazungumza na chombo chochote cha habari wala kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho. Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa taifa na kwa watanzania wote katika mchakato huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya kiuchumi bali kushiriki katika kuamua mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga. Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho, huku tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia muda mwingi kuandaa majungu na fitina, tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mchango wangu ambao nimewahi kuchangia bungeni ni huu.
Sakata la posho kwa wajumbe wa bunge la katiba laundiwa kamati. - YouTube
 
nasubiri hiyo kamati ndogo iliyoundwa kuhusu suala hili. wewe nimekusikia ingawa umefichaficha maelezo yako.
 
....punguza porojo na ujielekeze kwenye hoja ya msingi,uko upande gani?
(a).upande wa wanaotaka posho iongezwe
(b).wanaopinga posho kuongezwa...
 
Mimi huwa simuamini mwanasiasa yeyote hasa wa ccm! Naamini siasa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine tu na wanasiasa wapo kazini,in exception of mwl nyerere and co.
 
Ccm wote ndivyo mlivyo,kwanini watu wakuseme wewe na isiwe kigwangala au mwingine?.Kama hiyo mnayoita posho wakati ni zaidi ya mshahala wa mtu haitoshi si uludi kwako?.Umepima hali ya upepo baada ya kuwa umeshalalamika alafu unakuja na single ya ajabu eti unatujari watanzania,Tangu lini watu wa Cccm mkatujari watanzania?
 
Simamia maslahi ya Taifa na siyo vinginevyo,

Ila next time anzisha uzi kwanini unamsema hovyo EL na siyo Membe,Makamba,Wassira etc,
 
Kijana ni vyema ungekaa kimya kuliko kuja hapa JF na andiko lako hili jepesi.

Ni nani asiyejua kuwa mmetumia nguvu nyingi kuzipata hizo nafasi za ujumbe kwa matarajio ya kuneemeka?, ila sasa imekuwa tofauti kabisa na matarajio yenu.

Sasa hivi ndivyo itakavyo kuwa, utaki laki 3 kama posho, basi funga virago uende zako. Hiyo kamati iliyoundwa itakuja na mapendekezo haya haya. Hakuna nyongeza ya posho hapa.

By the way; kama Lowassa angekuwa rais hata huu mzozo usingekuwepo, zamani angeshatolea maamuzi kuwa posho HAIONGEZWI. Period.
 
Makonda nini maoni yako juu ya 300,000 kwa siku. acha siasa na maneno mengi
 
Kijana ni vyema ungekaa kimya kuliko kuja hapa JF na andiko lako hili jepesi.

Ni nani asiyejua kuwa mmetumia nguvu nyingi kuzipata hizo nafasi za ujumbe kwa matarajio ya kuneemeka?, ila sasa imekuwa tofauti kabisa na matarajio yenu.

Sasa hivi ndivyo itakavyo kuwa, utaki laki 3 kama posho, basi funga virago uende zako. Hiyo kamati iliyoundwa itakuja na mapendekezo haya haya. Hakuna nyongeza ya posho hapa.

By the way; kama Lowassa angekuwa rais hata huu mzozo usingekuwepo, zamani angeshatolea maamuzi kuwa posho HAIONGEZWI. Period.
Duh,mkuu leo upo pamoja na wapenda haki..!? Salute kwako mkuu..!
 
  • Thanks
Reactions: G11
Naomba unieleze ni wapi nimesikika ama kunukuliwa nikiwa nasema kuwa laki tatu ni ndogo. Ni mahojiano kwenye redio, tv ama akaunti yangu kwenye mtandao wowote wa kijamii..?
Tafuta mwenyewe mahali ulipolopoka!mie siyo kazi yangu kutafuta uliropokea wapi.

Kijana jifunze siasa, jambo hili lipo toka juzi, Leo hii eti unaibuka kukanusha!?

Ukiona hivyo ujue mchawi ni wewe mwenyewe!

Toa msimamo wenu maccm maana mpaka leo mpo kimia kama hamjui, tunawazidi kuwalaani..
 
Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba ieleweke kwamba sijazungumza na chombo chochote cha habari wala kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho. Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa taifa na kwa watanzania wote katika mchakato huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya kiuchumi bali kushiriki katika kuamua mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga. Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho, huku tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia muda mwingi kuandaa majungu na fitina, tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mchango wangu ambao nimewahi kuchangia bungeni ni huu.
Sakata la posho kwa wajumbe wa bunge la katiba laundiwa kamati. - YouTube

hongera mzalendo
 
Simamia maslahi ya Taifa na siyo vinginevyo,

Ila next time anzisha uzi kwanini unamsema hovyo EL na siyo Membe,Makamba,Wassira etc,
Mkuu huo uzi utausubiri sana, maana hata yeye hajitambui, anatumiwa tu kama kifaa kutumana ili apate umaarufu wa harufu
 
Bw. Mdogo,watanzania wa leo siyo wa kudanganywa kwa maneno mazuri km unavyotuaminisha..! Umetumia muda mwingi kuandika porojo kwa watu wanaojitambua. Ungekuwa mzalendo wa kweli,ungesema hapa msimamo wako ni upi! Posho haitoshi iongezwe,inatosha au ni kubwa upunguzwe!?
 
Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba ieleweke kwamba sijazungumza na chombo chochote cha habari wala kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho. Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa taifa na kwa watanzania wote katika mchakato huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya kiuchumi bali kushiriki katika kuamua mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga. Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho, huku tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia muda mwingi kuandaa majungu na fitina, tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mchango wangu ambao nimewahi kuchangia bungeni ni huu.
Sakata la posho kwa wajumbe wa bunge la katiba laundiwa kamati. - YouTube

pole mkuu kwa majukumu ya kutunga sheria, binafsi siku nyingine nakushauri usilete mada ya kuchokozeka, yaani usiilete kama mtuhumiwa hata kama unajua unatuhumiwa then sisi ambao tulikuwa hatujasikia kuwa iunataka ziada then tujue kuwa unasimamia nini, ila mada za kulalamika sisi wengine tutaanzia apo apo kukurushia matusi wakati hata hatukuwahi kusikia izo tuhuma kwako....ingefaa ungeandika uzi kwa kukemea izo posho then sisi tungebeba msimamo wako...sana sana hata na wale makonda wenzangu wa daladala za mbagala ambao tuko bize ,once tukichunugulia apa ili tupate overview tutakachokiona ni kuwa unajitetea badala ya ungeweka kichwa cha habari kukemea then tungejua unakemea.

Mkuu posho ni ndogo kuliko ukubwa wa shughuli ya kuirudisha Tanganyika, ivo jielekeze kujadili iyo sheria bila kurudi nyuma...usianze kupanda mlima kisha ukarudi chini kuona nani alikuwa anakuvuta mguu wakati unapanda...hautafikia lengo....
 
Nilikipuuza tangu siku ile ulipomtukana matusi ya nguoni Edward Lowassa ambaye kiumri ni sawa na Baba yako.

Kweli Siasa tu ikufanye ukose utu kiasi hicho?
 
haipendezi kwa mtu wa hadhi yako kuwa mropokaji..!!
Kunya anye kuku akinya bata, kahara, sasa matamko uliyotoa hivi karibuni ukimshambulia mtu ambaye unaweza kuzama kabisa katika viatu vyake na bado akavivaa na isionekane kama umo ndani yake na akaendelea na safari zake ulikuwa unaongea au unaropoka?
,
 
Kijana ni vyema ungekaa kimya kuliko kuja hapa JF na andiko lako hili jepesi.

Ni nani asiyejua kuwa mmetumia nguvu nyingi kuzipata hizo nafasi za ujumbe kwa matarajio ya kuneemeka?, ila sasa imekuwa tofauti kabisa na matarajio yenu.

Sasa hivi ndivyo itakavyo kuwa, utaki laki 3 kama posho, basi funga virago uende zako. Hiyo kamati iliyoundwa itakuja na mapendekezo haya haya. Hakuna nyongeza ya posho hapa.

By the way; kama Lowassa angekuwa rais hata huu mzozo usingekuwepo, zamani angeshatolea maamuzi kuwa posho HAIONGEZWI. Period.
kijana haujui unachokizungumza..,ni bora ungekaa kimya tu.
 
makonda mimi nashauri posho ya laki3 yenyewe ni kubwa mno, hoteli ya southern sun iliyoko city cetre dar es salaam ni kuwa ina vyumba mpaka dola 55,apo breakfast bure , arusha naura spring hotel bei sh dola 90, je maisha ya dodoma ni ghali zaidi ya miji hii?je mnatafuta hela ya kuponda maisha? binafsi sitarajii kupata katiba bora kwa ufisadi wenu wa bunge ili...nasubiri tu muilete tuipigie kura ya kuikataa then tuendelee na ile yenye viraka.
Mwl na sekretari mnakula mshahara wake kwa siku,yeye anacheza na chaki mwezi mzima.,kweli jaman? hii katiba ni ya matajiri tu sisi maskini kuna siku tutaunda ya kwetu....cha ajabu aliyewachagua amesema wale walioajiriwa taasisi zao ziendelee kuwajali, je sheria za nchi yenu zinaruhusu double salary????
Yaani mimi najikunja mwezi mzima then nalipa PAYE ela iyo inachukuliwa anapewa Paul Makonda na Hamis Mgeja kwa ujira wa siku moja!!! Nadhani kama nyie kweli ni wazarendo ,tafadhari pendekeza iyo posho ipunguzwe walau iwe laki moja mpaka laki na sitini, tofauti nauko sisi tutawaona watunga katiba wote ni wezi tu!
 
Back
Top Bottom