Msimamo wangu kuhusu Ongezeko la Posho kwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba - Makonda

Msimamo wangu kuhusu Ongezeko la Posho kwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba - Makonda

Kunya anye kuku akinya bata, kahara, sasa matamko uliyotoa hivi karibuni ukimshambulia mtu ambaye unaweza kuzama kabisa katika viatu vyake na bado akavivaa na isionekane kama umo ndani yake na akaendelea na safari zake ulikuwa unaongea au unaropoka?
,
Nadhani sijakuelewa sawasawa nini nakimaanisha katika post yako hii.
Kama hoja ni kukosoa wale wanaoenda kinyume na taratibu na kanuni tulizojiwekea ndani ya nchi na Chama, sidhani kuwa hilo linakuwa justified kwa umri, kuwa kijana wa miaka 21 aliyeiba kuku anapaswa aambiwe na aadhibiwe kwa kosa hilo ila mzee wa miaka 61 aliyeiba kuku asifiwe na kupongezwa..???
 
makonda mimi nashauri posho ya laki3 yenyewe ni kubwa mno, hoteli ya southern sun iliyoko city cetre dar es salaam ni kuwa ina vyumba mpaka dola 55,apo breakfast bure , arusha naura spring hotel bei sh dola 90, je maisha ya dodoma ni ghali zaidi ya miji hii?je mnatafuta hela ya kuponda maisha? binafsi sitarajii kupata katiba bora kwa ufisadi wenu wa bunge ili...nasubiri tu muilete tuipigie kura ya kuikataa then tuendelee na ile yenye viraka.
Mwl na sekretari mnakula mshahara wake kwa siku,yeye anacheza na chaki mwezi mzima.,kweli jaman? hii katiba ni ya matajiri tu sisi maskini kuna siku tutaunda ya kwetu....cha ajabu aliyewachagua amesema wale walioajiriwa taasisi zao ziendelee kuwajali, je sheria za nchi yenu zinaruhusu double salary????
Yaani mimi najikunja mwezi mzima then nalipa PAYE ela iyo inachukuliwa anapewa Paul Makonda na Hamis Mgeja kwa ujira wa siku moja!!! Nadhani kama nyie kweli ni wazarendo ,tafadhari pendekeza iyo posho ipunguzwe walau iwe laki moja mpaka laki na sitini, tofauti nauko sisi tutawaona watunga katiba wote ni wezi tu!
hoja yako nimeipokea ingawa haijazingatia vigezo vingi katika ufikishaji wake, lakini ni hoja na nimeizingatia.
 
Kunya anye kuku akinya bata, kahara, sasa matamko uliyotoa hivi karibuni ukimshambulia mtu ambaye unaweza kuzama kabisa katika viatu vyake na bado akavivaa na isionekane kama umo ndani yake na akaendelea na safari zake ulikuwa unaongea au unaropoka?
,

duh mkuu, hii ni lugha ya sanaa ya hali ya juu, inanichukua muda kumfikiria mjumbe kafichwa kwenye kiatu bila madhara yoyote, mkuu namfikiria mjumbe kuwa mh Lowasa yuko pale anachangia hoja bungeni anasikia kajitu kanamtekenya, anajisemea nitamwambia mama regina aangalie viatu ivi kwa nini kuna kitu kinanigusa gusa, dah anafika nyumbani kuchomoa kiatu, laaah ulaah laah ulaah kumbe 'nilikavaliana' kajamaa, laah ulaa! mgemamkwezi, leo umeupa mtihani ubongo wangu kufikiria size ya uyu mjumbe, duh! Naomba kuuliza je, kweli haijamdhalilisha mjumbe wetu wa katiba????????????????????/
 
Mbona hata huo msimamo sijauona!? Nyie wanasiasa mna matatizo gani!? Hapa ulichokiandika ni porojo tu
 
Kijana ni vyema ungekaa kimya kuliko kuja hapa JF na andiko lako hili jepesi.

Ni nani asiyejua kuwa mmetumia nguvu nyingi kuzipata hizo nafasi za ujumbe kwa matarajio ya kuneemeka?, ila sasa imekuwa tofauti kabisa na matarajio yenu.

Sasa hivi ndivyo itakavyo kuwa, utaki laki 3 kama posho, basi funga virago uende zako. Hiyo kamati iliyoundwa itakuja na mapendekezo haya haya. Hakuna nyongeza ya posho hapa.

By the way; kama Lowassa angekuwa rais hata huu mzozo usingekuwepo, zamani angeshatolea maamuzi kuwa posho HAIONGEZWI. Period.

Siamini kama niwewe HAMY-D. Naona sasa umeanza kukomaa kiakili na kiuzalendo. Hongera sana kijana. Huyu makonda ni mjinga sana anataka kumalizia shda zake hapo.
 
Kijana ni vyema ungekaa kimya kuliko kuja hapa JF na andiko lako hili jepesi.

Ni nani asiyejua kuwa mmetumia nguvu nyingi kuzipata hizo nafasi za ujumbe kwa matarajio ya kuneemeka?, ila sasa imekuwa tofauti kabisa na matarajio yenu.

Sasa hivi ndivyo itakavyo kuwa, utaki laki 3 kama posho, basi funga virago uende zako. Hiyo kamati iliyoundwa itakuja na mapendekezo haya haya. Hakuna nyongeza ya posho hapa.

By the way; kama Lowassa angekuwa rais hata huu mzozo usingekuwepo, zamani angeshatolea maamuzi kuwa posho HAIONGEZWI. Period.

Kwa leo nimekukubali sana.
 
Mbona kila mtu anajifanya hajadai ongezeko la posh? Hata asubuhi Star Tv nimewaona Mnyika na Kigwangala akiruka kuhusu madai ya posho, sasa hiyo kamati imeundwa ya nini?

Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba ieleweke kwamba sijazungumza na chombo chochote cha habari wala kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho. Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa taifa na kwa watanzania wote katika mchakato huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya kiuchumi bali kushiriki katika kuamua mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga. Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho, huku tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia muda mwingi kuandaa majungu na fitina, tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mchango wangu ambao nimewahi kuchangia bungeni ni huu.
Sakata la posho kwa wajumbe wa bunge la katiba laundiwa kamati. - YouTube
 
hoja yako nimeipokea ingawa haijazingatia vigezo vingi katika ufikishaji wake, lakini ni hoja na nimeizingatia.

mkuu sitarajii kuandika au kukupata wazo langu likawa exact kama unavohitaji...ayo ni mawazo yangu...you can take the meat in it and throw the skin.
 
Mbona kila mtu anajifanya hajadai ongezeko la posh? Hata asubuhi Star Tv nimewaona Mnyika na Kigwangala akiruka kuhusu madai ya posho, sasa hiyo kamati imeundwa ya nini?

na ikipitiswa wanaigonga....ah aha ah hao ndo wanasiasa wetu mkuu
 
hoja yako nimeipokea ingawa haijazingatia vigezo vingi katika ufikishaji wake, lakini ni hoja na nimeizingatia.

Vigezo kama ada za watoto wako za shule kodi ya nyumba dereva ama kweli wewe jinga sana ulitegemea hapo ndio mahali pakuponea.
 
Kijana ni vyema ungekaa kimya kuliko kuja hapa JF na andiko lako hili jepesi.

Ni nani asiyejua kuwa mmetumia nguvu nyingi kuzipata hizo nafasi za ujumbe kwa matarajio ya kuneemeka?, ila sasa imekuwa tofauti kabisa na matarajio yenu.

Sasa hivi ndivyo itakavyo kuwa, utaki laki 3 kama posho, basi funga virago uende zako. Hiyo kamati iliyoundwa itakuja na mapendekezo haya haya. Hakuna nyongeza ya posho hapa.

By the way; kama Lowassa angekuwa rais hata huu mzozo usingekuwepo, zamani angeshatolea maamuzi kuwa posho HAIONGEZWI. Period.
Kwa mara ya kwanza nimeilike post yako!!!
 
Hata Mnyika na Kigwangala hawakukataa kuwa ikiongezwa watakataa kuchukua, ila niliona Mnyika akijipambanua kuwa huwa hachukui posho kwenye vikao vya halamshauri au baraza la madiwani, mwenziye akawa mpole hata hakutaka kuliongelea zaidi.

na ikipitiswa wanaigonga....ah aha ah hao ndo wanasiasa wetu mkuu
 
hoja yako nimeipokea ingawa haijazingatia vigezo vingi katika ufikishaji wake, lakini ni hoja na nimeizingatia.

hoja za msingi ni zile zilizoko kwenye rasimu ya tume ya Mh Warioba,, hoja iliyobeba mawazo ya wananchi juu ya katiba mpya,ila ndiyo hivyo munakwenda kuitupilia mbali na kuileta ile ya ya kwenu(ccm)muliyoihifadhi kabatini kusubiria muda mwafaka muihalalishe kwa kura za vidole!!! wewe kweli unaweza kuzingatia hoja ya kupunguza bakshishi hiyo ya ujumbe? mwanasiasa ni zaidi ya shetani!! anaweza kumchinja yeyote kwa kidole tu ili atimize tamaa yake na genge lake,ama akawapiganisha mkachinjana kama kuku ili tu yeye aendelee kuwa ikulu.
 
Makonda tunakusubiri je laki tatu a. Inatosha b. Haitoshi c. Ipunguzwe d. Hakuna jibu sahihi
Jibu ni..........
 
....punguza porojo na ujielekeze kwenye hoja ya msingi,uko upande gani? (a).upande wa wanaotaka posho iongezwe (b).wanaopinga posho kuongezwa...
Ahsante, tz inaangamizwa na wanafiki. Heading yake haiwiani na na hzo ndarandira alizoandika, otherwise anataka kutuambia kuwa ndio uzao wa shule zetu za kata. Thenk yu sana!
 
MJUMBE WA BUNGE LA KATIBA PAUL
MAKONDA, AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA
KUDAI POSHO.

"Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi
tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji
muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi
mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba
bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa
Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika
uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa
nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya
msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa
nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya
taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao
kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba
ieleweke kwamba sijazungumza na chombo
chochote cha habari wala kuandika kwenye
mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho.
Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa
taifa na kwa watanzania wote katika mchakato
huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania
na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa
kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya
kiuchumi bali kushiriki katika kuamua
mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga.
Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo
kati ya walionacho na wasionacho, huku
tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa
WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi
ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote
wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia
muda mwingi kuandaa majungu na fitina,
tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo
sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia
kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na
kijamii".

By
PAULMakonda​

Tamko hili la Makonda limekuja baada ya Jana Peter Dafi.com kuandika habari za Makonda kuwa kaunga hoja mchakato wa posho kuongezwa kwa wajumbe wa katiba mpya.​
 
Last edited by a moderator:
Huo unakuwa mzimu wa LOWASSA unamuandama....
 
Back
Top Bottom