Msimamo wangu kuhusu Ongezeko la Posho kwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba - Makonda

Msimamo wangu kuhusu Ongezeko la Posho kwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba - Makonda

MJUMBE WA BUNGE LA KATIBA PAUL
MAKONDA, AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA
KUDAI POSHO.

"Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi
tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji
muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi
mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba
bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa
Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika
uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa
nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya
msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa
nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya
taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao
kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba
ieleweke kwamba sijazungumza na chombo
chochote cha habari wala kuandika kwenye
mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho.
Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa
taifa na kwa watanzania wote katika mchakato
huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania
na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa
kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya
kiuchumi bali kushiriki katika kuamua
mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga.
Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo
kati ya walionacho na wasionacho, huku
tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa
WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi
ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote
wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia
muda mwingi kuandaa majungu na fitina,
tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo
sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia
kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na
kijamii".

By
PAULMakonda​

Tamko hili la Makonda limekuja baada ya Jana Peter Dafi.com kuandika habari za Makonda kuwa kaunga hoja mchakato wa posho kuongezwa kwa wajumbe wa katiba mpya.​
Its welcome news, wengine tulishaanza kurusha madongo tukijiuliza huyu Paul makonda ndiye, au siye?
Tunashukuru kwa ufafanuzi.
 
mbona mnaandika na kujijibu wenye makonda anatafuta cheap pop. kwa kick ya posho
 
Mi naona kunavijana wameenda kuleta comedy ndani ya Bunge, hawajui wajibu wa kilichowapeleka pale zaidi ya kutafta kick za kisiasa!
 
Huyu bwana amezoea kuhongwa na akina membe sasa anataka leta njaa zake huku kwenye umma kaumbuka sasa anakanusha..jambazi mkubwa huyu
 
Bora umewaeleza mwenyewe,kuna mtu anaitwa mussa Abdallah aliandika hiyo habari katika facebook nikamjibu kama ifuatavyo:najua paul makonda hawezi kusema hataki posho ya laki tatu(300,000/=),mleta mada najua ni mfuasi wa ....... ambaye makonda ameeleza ukweli wa utumbo anaoufanya. yeye akanijibu kwa kuniambia napiga ramli,nikamjibu tena:sijui ramli ni nini ila nimesema makonda hawezi kukataa posho hiyo,kama hiyo ni kupiga ramli basi sawa. napenda uhalisia zaidi ya ushabiki@Mussa Abdallah

RAI yangu: Fanya kazi kama unavyofanya.
 
Kijana ni vyema ungekaa kimya kuliko kuja hapa JF na andiko lako hili jepesi.

Ni nani asiyejua kuwa mmetumia nguvu nyingi kuzipata hizo nafasi za ujumbe kwa matarajio ya kuneemeka?, ila sasa imekuwa tofauti kabisa na matarajio yenu.

Sasa hivi ndivyo itakavyo kuwa, utaki laki 3 kama posho, basi funga virago uende zako. Hiyo kamati iliyoundwa itakuja na mapendekezo haya haya. Hakuna nyongeza ya posho hapa.

By the way; kama Lowassa angekuwa rais hata huu mzozo usingekuwepo, zamani angeshatolea maamuzi kuwa posho HAIONGEZWI. Period.

Chukua LIKE ya simu kiroho safi kabisa.
 
Pmakonda,
Hii post yako iko shallow sana, hujawa muwazi kana kwamba upo kambi ya fulani, hutaki kuwa muwazi zaidi kwakuwa unaweza kuwa kambi nyingine vile vile. Kuparaganyia kwa chama chako kunakunyima fursa ya kuwa huru
 
Last edited by a moderator:
Cheap politics,,, msimamo hapo ni nini? ? Unatafuta attention ya watu,,, kwan wew utakuwaje tofauti na wenzako? ??kama kwel ulikuwa na nia nzuri na hutaki posho kwa nini uanze kuzungumzia posho kabla ya Rasimu? ??

Uko hapo for posho,,, full stop!
 
Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba ieleweke kwamba sijazungumza na chombo chochote cha habari wala kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho. Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa taifa na kwa watanzania wote katika mchakato huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya kiuchumi bali kushiriki katika kuamua mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga. Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho, huku tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia muda mwingi kuandaa majungu na fitina, tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.


Mchango wangu ambao nimewahi kuchangia bungeni ni huu.
Sakata la posho kwa wajumbe wa bunge la katiba laundiwa kamati. - YouTube

Makonda nenda taratibu,,umechelewa kukanusha ulikua unasoma upepo hakuna atakae kuamini,,Rais atawaumiza wanyonge akikubali matakwa haya ya mbweha wasio na huruma kwa taifa,umemuangusha hata aliyekuamini na kukuteua,,,inashikitisha eti mada kuu kutaka posho,upumbavu huu hauvumiliki,wabunge wote mnaotaka kuongezewa posho peweni na mama zenu sio pesa za walipa kodi,msitake kumchonganisha Kikwete na umma,,manina
 
Ni yule wa ccj?
Mkuu unarudisha mapigo kutaka kumsaidia mzee mzima aliyeanza safari ya matumaini ya ndoto zake kutokana na sucker punch ya huyu kijana week chache zilizopita!.

Inavyoonekana mpaka tufike kwenye chaguzi za kitaifa mtakuwa mmeisha toana macho kwa sababu ya uongozi ambao pia hamfahamu kama wananchi watawapa ridhaa ya uongozi kitaifa.


Mtu unapotumia nguvu nyingi katika promotions lazima kuna malipo mazuri kwa sababu ukubwa wa investment unaendana na mtaji wake.

Kwa sasa makundi na uhasama umepelekwa mpaka kwenye Bunge la Katiba. Now things are getting serious!.

Huyu Makonda naye anakuja na andiko la kudonoa donoa kama wanasiasa wengine bila hata kusema msimamo wake halisi.

Wanasiasa wetu ni majanga tupu.

Mantiki inaniambia ukimuona mwanasiasa ameacha wazi katika maneno au maandishi yake upande wa hili sakata la posho, basi kuna uwezekano mkubwa anapenda posho ziongezwe.
 
Kuna mgombea mmoja ambae Makonda ni swshiba wake huyu ni Sitta,juzi anaomba kuungwa mkono ktika uenyekiti akiwaahidi wajumbe. Kuwa atapandisha posho hadi laki saba Makonda jitokeze ubishe nikupe za uso,nawewe kwa kuwa unatumikia tumbo ukawa unamuunga mkono...wote tuko dodoma hapa kawadanganye wajinga,..juzi kwa macho yangu nikiwa na waandishi wenzangu nimemsikia baba yako sitta akijigamba kupandisha posho,mnachoangalia ni maslahi yenu ya kisiasa hata kama taifa litaumia,mmesoma upepo mmeguguka hatutaki huu ushenzi.msimchonganishe Rais na wananchi manina kabisa.

mwalimu analipwa laki tatu kwa mwezi.anawstoto na anaishije,Udom watoto wetu wanapata 7500 manina.

Jana nimepita hotel zote nzuri 30000 unalala chumba cha heshima pumbafu zenu,ifike wakati tuwaheshimu wananchi
 
makonda mimi nashauri posho ya laki3 yenyewe ni kubwa mno, hoteli ya southern sun iliyoko city cetre dar es salaam ni kuwa ina vyumba mpaka dola 55,apo breakfast bure , arusha naura spring hotel bei sh dola 90, je maisha ya dodoma ni ghali zaidi ya miji hii?je mnatafuta hela ya kuponda maisha? binafsi sitarajii kupata katiba bora kwa ufisadi wenu wa bunge ili...nasubiri tu muilete tuipigie kura ya kuikataa then tuendelee na ile yenye viraka.
Mwl na sekretari mnakula mshahara wake kwa siku,yeye anacheza na chaki mwezi mzima.,kweli jaman? hii katiba ni ya matajiri tu sisi maskini kuna siku tutaunda ya kwetu....cha ajabu aliyewachagua amesema wale walioajiriwa taasisi zao ziendelee kuwajali, je sheria za nchi yenu zinaruhusu double salary????
Yaani mimi najikunja mwezi mzima then nalipa PAYE ela iyo inachukuliwa anapewa Paul Makonda na Hamis Mgeja kwa ujira wa siku moja!!! Nadhani kama nyie kweli ni wazarendo ,tafadhari pendekeza iyo posho ipunguzwe walau iwe laki moja mpaka laki na sitini, tofauti nauko sisi tutawaona watunga katiba wote ni wezi tu!

Mimi nilikuwa Dodoma kikazi hivi karibuni nilikuwa nalala hoteli moja nzuri self contained na huduma za kifungua kinywa kwa Sh. 15,000/= Hivyo hawa wajumbe hata wakikaa kwenye hoteli za 30,000/- inatosha waache tamaa. Kwa mahesabu rahisi kwa mtu asiyependa anasa kwa siku anaweza kutumia kati ya Sh. 45,000/= hadi 60,000/= kwa siku ikiwa ni pamoja na kulipia chumba. Kwa maana hiyo kwa wastani mjumbe anaweza kuwa anabaki na kati ya 230,000/= na 250,000/= kama net profit! Bado haziwatoshi? Mimi naona wote wanaopinga 300,000/= ni hayawani washindwe, walegee na wanyong'onyee kabisa. Lakini linalonishangaza mimi ni kuwa huko kwenye bunge la katiba kuna viongozi wa dini pia. Mbona hatuwasikii kututetea sisi wanakondooo wao? Au nao wanaona ni ndogo?
 
Kibaraka mkubwa wa riz huyu dogo, kati ya janga katika taifa ni huyu jamaa, alipoteuliwa tu juzi nilikuwa nae mlimani city hapo hapo akaongea na sita then sita akamuelekeza showroom ile ya karibu na shoperz kwenda kuchukua gari ya mkopo kwa makubaliano kuwa atakuwa analipa kila wiki kumbe ni ela za posho, pumba.........f kabisa
 
Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba ieleweke kwamba sijazungumza na chombo chochote cha habari wala kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho. Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa taifa na kwa watanzania wote katika mchakato huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya kiuchumi bali kushiriki katika kuamua mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga. Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho, huku tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia muda mwingi kuandaa majungu na fitina, tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.


Mchango wangu ambao nimewahi kuchangia bungeni ni huu.
Sakata la posho kwa wajumbe wa bunge la katiba laundiwa kamati. - YouTube

Yani we kiazi kweli haki ya Mungu!!!
Umeenda bungeni hujui hata ni rasimu ipi inaenda kujadiliwa?!
Bora usingeweka huo utumbo ulioongea kwenye youtube...
 
We makonda mnafiki mkubwa unazipenda saaana unajishaua tu hapa.
Ccj inaendeleaje?
 
Du!bora ungekaa kimya mkuu makondeko!nani asiejua jinsi makada wa CCM walivyo vigeugeu?
 
w99OGSIo25mMAAAAABJRU5ErkJggg==
 
Upuuzi wako uliozoea kuandika kwenye Uhuru na Startv leo umeuleta huku kwenye great thinkers,kijana mdogo unakuwa na siasa za kizee hivi ni aibu,JF sio hadhi yako tafuta pa kwenda kuandika huu ----- wako.
 
Back
Top Bottom