Msimamo wangu kuhusu Ongezeko la Posho kwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba - Makonda

Msimamo wangu kuhusu Ongezeko la Posho kwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba - Makonda

Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba ieleweke kwamba sijazungumza na chombo chochote cha habari wala kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho. Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa taifa na kwa watanzania wote katika mchakato huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya kiuchumi bali kushiriki katika kuamua mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga. Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho, huku tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia muda mwingi kuandaa majungu na fitina, tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.


Mchango wangu ambao nimewahi kuchangia bungeni ni huu.
Sakata la posho kwa wajumbe wa bunge la katiba laundiwa kamati. - YouTube

Hapa ndio umeandika nini sasa? Jikite kwenye point, acha Siasa Uchwara!
 
Kijana umejitahidi kupata ulichokua unakitafuta "umaarufu" kwani sikua nafahamu kama kuna mtu anaeitwa Paul Makonda dunia hii..sasa natambua
 
Achen kuwakandamiza wavuja jasho fanyen kilichowapeleka au ndio kusema mmepata ulaji huko na ndio maana kila kukicha kila mtu analalamika ooh mm nilipeleka jina langu kama mwakilishi fulan lkn halijatoka kuna hujuma. ..labda mtuambia mnawakilisha nn...kujaza matumbo? Au kero za wananchi..pigen kaz
 
Back
Top Bottom