Msimamo wangu kuhusu Ongezeko la Posho kwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba - Makonda

Nadhani sijakuelewa sawasawa nini nakimaanisha katika post yako hii.
Kama hoja ni kukosoa wale wanaoenda kinyume na taratibu na kanuni tulizojiwekea ndani ya nchi na Chama, sidhani kuwa hilo linakuwa justified kwa umri, kuwa kijana wa miaka 21 aliyeiba kuku anapaswa aambiwe na aadhibiwe kwa kosa hilo ila mzee wa miaka 61 aliyeiba kuku asifiwe na kupongezwa..???
 
hoja yako nimeipokea ingawa haijazingatia vigezo vingi katika ufikishaji wake, lakini ni hoja na nimeizingatia.
 

duh mkuu, hii ni lugha ya sanaa ya hali ya juu, inanichukua muda kumfikiria mjumbe kafichwa kwenye kiatu bila madhara yoyote, mkuu namfikiria mjumbe kuwa mh Lowasa yuko pale anachangia hoja bungeni anasikia kajitu kanamtekenya, anajisemea nitamwambia mama regina aangalie viatu ivi kwa nini kuna kitu kinanigusa gusa, dah anafika nyumbani kuchomoa kiatu, laaah ulaah laah ulaah kumbe 'nilikavaliana' kajamaa, laah ulaa! mgemamkwezi, leo umeupa mtihani ubongo wangu kufikiria size ya uyu mjumbe, duh! Naomba kuuliza je, kweli haijamdhalilisha mjumbe wetu wa katiba????????????????????/
 
Mbona hata huo msimamo sijauona!? Nyie wanasiasa mna matatizo gani!? Hapa ulichokiandika ni porojo tu
 

Siamini kama niwewe HAMY-D. Naona sasa umeanza kukomaa kiakili na kiuzalendo. Hongera sana kijana. Huyu makonda ni mjinga sana anataka kumalizia shda zake hapo.
 

Kwa leo nimekukubali sana.
 
Mbona kila mtu anajifanya hajadai ongezeko la posh? Hata asubuhi Star Tv nimewaona Mnyika na Kigwangala akiruka kuhusu madai ya posho, sasa hiyo kamati imeundwa ya nini?

 
hoja yako nimeipokea ingawa haijazingatia vigezo vingi katika ufikishaji wake, lakini ni hoja na nimeizingatia.

mkuu sitarajii kuandika au kukupata wazo langu likawa exact kama unavohitaji...ayo ni mawazo yangu...you can take the meat in it and throw the skin.
 
Mbona kila mtu anajifanya hajadai ongezeko la posh? Hata asubuhi Star Tv nimewaona Mnyika na Kigwangala akiruka kuhusu madai ya posho, sasa hiyo kamati imeundwa ya nini?

na ikipitiswa wanaigonga....ah aha ah hao ndo wanasiasa wetu mkuu
 
hoja yako nimeipokea ingawa haijazingatia vigezo vingi katika ufikishaji wake, lakini ni hoja na nimeizingatia.

Vigezo kama ada za watoto wako za shule kodi ya nyumba dereva ama kweli wewe jinga sana ulitegemea hapo ndio mahali pakuponea.
 
Kwa mara ya kwanza nimeilike post yako!!!
 
Hata Mnyika na Kigwangala hawakukataa kuwa ikiongezwa watakataa kuchukua, ila niliona Mnyika akijipambanua kuwa huwa hachukui posho kwenye vikao vya halamshauri au baraza la madiwani, mwenziye akawa mpole hata hakutaka kuliongelea zaidi.

na ikipitiswa wanaigonga....ah aha ah hao ndo wanasiasa wetu mkuu
 
hoja yako nimeipokea ingawa haijazingatia vigezo vingi katika ufikishaji wake, lakini ni hoja na nimeizingatia.

hoja za msingi ni zile zilizoko kwenye rasimu ya tume ya Mh Warioba,, hoja iliyobeba mawazo ya wananchi juu ya katiba mpya,ila ndiyo hivyo munakwenda kuitupilia mbali na kuileta ile ya ya kwenu(ccm)muliyoihifadhi kabatini kusubiria muda mwafaka muihalalishe kwa kura za vidole!!! wewe kweli unaweza kuzingatia hoja ya kupunguza bakshishi hiyo ya ujumbe? mwanasiasa ni zaidi ya shetani!! anaweza kumchinja yeyote kwa kidole tu ili atimize tamaa yake na genge lake,ama akawapiganisha mkachinjana kama kuku ili tu yeye aendelee kuwa ikulu.
 
Makonda tunakusubiri je laki tatu a. Inatosha b. Haitoshi c. Ipunguzwe d. Hakuna jibu sahihi
Jibu ni..........
 
....punguza porojo na ujielekeze kwenye hoja ya msingi,uko upande gani? (a).upande wa wanaotaka posho iongezwe (b).wanaopinga posho kuongezwa...
Ahsante, tz inaangamizwa na wanafiki. Heading yake haiwiani na na hzo ndarandira alizoandika, otherwise anataka kutuambia kuwa ndio uzao wa shule zetu za kata. Thenk yu sana!
 
MJUMBE WA BUNGE LA KATIBA PAUL
MAKONDA, AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA
KUDAI POSHO.

"Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi
tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji
muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi
mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba
bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa
Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika
uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa
nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya
msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa
nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya
taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao
kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba
ieleweke kwamba sijazungumza na chombo
chochote cha habari wala kuandika kwenye
mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho.
Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa
taifa na kwa watanzania wote katika mchakato
huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania
na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa
kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya
kiuchumi bali kushiriki katika kuamua
mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga.
Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo
kati ya walionacho na wasionacho, huku
tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa
WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi
ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote
wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia
muda mwingi kuandaa majungu na fitina,
tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo
sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia
kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na
kijamii".

By
PAULMakonda​

Tamko hili la Makonda limekuja baada ya Jana Peter Dafi.com kuandika habari za Makonda kuwa kaunga hoja mchakato wa posho kuongezwa kwa wajumbe wa katiba mpya.​
 
Last edited by a moderator:
Huo unakuwa mzimu wa LOWASSA unamuandama....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…