Msimhukumu Rais Samia pasipokuwa na uhakika

Ndio maana serikali duniani uwa zikishatoa elimu, asietaka kuelewa awamsubiri atawakuta wenzake mbele ya safari.
Kabisa! Kwa sababu wapo watakaokuelewa na wasiokuelewa hawatakosekana ! Thinking capacity siku zote haziko sawasawa baina ya watu na watu it’s normal in life !!
 
Wewe ndiyo unaleta vitu vya kichwani mwako.

Wenzio wanaongelea mambo ambayo yapo kwenye mkataba mama, wewe unaongelea hisia. Mkataba mama umekwishatamka kuwa mwisho wa mkataba ni pale ambapo mikataba midogo.midogo yote itakapoisha.

Na mkataba mama umekwishatamka kuwa hatutaruhusiwa kuwakaribisha wawekezaji wengine kwenye sekta ya bandari wakati IGA ikiwa hai. Unaelewa maana yake?

Maana yake ni kwamba, hata kama HGA ya Dar port ikawa imeisha muda wake, lakini mwaka huo inapoisha, kuna HGA nyingine bado ina miaka 5 kwisha, IGA itakuwa bado inafanya. Na IGA ina kipengere kinachokuzuia kualika wawekezaji wengine kuwekeza kwenye sekta ya bandari. Yaani mkataba wa HGA na hao DP umeisha, lakini bado unaendelea kulazimika kutii masharti ya IGA kwa sababu kuna miradi ambayo HGA zake bado zinaishi.

Ni mkataba wa kishenzi, wa kijinga na wa hovyo kupindukia.
 
Shida ni kwamba watu wametumia muda mwingi kuwaelezea sana maana ya hiyo IGA.

Mfano mkurugenzi wa sheria kutoka wizara ya uchukuzi amedadavua karibu kila kitu hapo kwa lugha nyepesi, ila watu bado tu; awataki kuelewa somo.
Tatizo kiongozi hujaelewa asietakiwa ni muarabu na sio mkataba na tena hawamtaki muarabu kwa maslah yao na sio ya taifa
 
Shida ni kwamba watu wametumia muda mwingi kuwaelezea sana maana ya hiyo IGA.

Mfano mkurugenzi wa sheria kutoka wizara ya uchukuzi amedadavua karibu kila kitu hapo kwa lugha nyepesi, ila watu bado tu; awataki kuelewa somo.
Hakuna mtu yeyote anayeweza kudadavua ujambazi halafu ugeuke kuwa ni wema.

Watu wengi wanaelewa ni nini kilichomo kwenye mkataba. Hatuhitaji ufafanuzi. Ufafanuzi wa nini kwenye kitu kinachoeleweka na kilicho wazi?
 
Kabisa! Kwa sababu wapo watakaokuelewa na wasiokuelewa hawatakosekana ! Thinking capacity siku zote haziko sawasawa baina ya watu na watu it’s normal in life !!
Na ata sababu pia zinaweza kuwepo za kutotaka kuelewa. Watu ambao maslahi yao yataguswa awawezi kuona bandari mtu atazuia ulaji wao.
 
Mbona kwenye kila pesa zikitolewa anatajwa yeye tu utasikia hizi pesa zimetolewa na mama Dr, hospitali ikijengwa utasikia hizi pesa zimetolewa na Dr( utadhani hizo unazitoa za kwakwe wakati ni kodi yetu) kama amekubali kusifiwa kwa mazuri yote basi na akubali kulaumiwa kwa mabaya yoote, yeye ndie kashika mpini hao wengine sisi hatuwajui!
 
Ww unauwakika unavyo tukataza. Na pia kama nivinginevyo mbona mama asemi? Acha shobo sw.
 
Hakuna mtu yeyote anayeweza kudadavua ujambazi halafu ugeuke kuwa ni wema.

Watu wengi wanaelewa ni nini kilichomo kwenye mkataba. Hatuhitaji ufafanuzi. Ufafanuzi wa nini kwenye kitu kinachoeleweka na kilicho wazi?
Sasa hapo ndio umeandika nini zaidi ya kupinga tu bila ya sababu za msingi.
 
Wewe na Prof. Shivji nani ana akili kujua mikataba, Toka hapa unatupigia kelele tu.
 
Huo Uhakika utapatikana lini na wapi..., Ukiwa kiongozi likiharibika lazima Ubebe lawama..., Ukiwa kiongozi mzuri yale mema yote na mazuri hata kama yote umeyafanya wewe unashare na wenzako.... (Take all the blame even if your not responsible and share all the credits)..,

Ila kipindi hiki cha UCHAWA hata jua likiwaka au mvua ikinyesha unaambiwa unaupiga mwingi..., Ukirikoroga hata kama ni wewe binafsi na kwa ubishi wako wa kutokusikiliza ushauri watasema ulishauriwa vibaya....

Kweli afadhali wajinga kuliko Chawa......
 
Wamepigwa upo na kiburi cha mamlaka ili washuhudie maanguko yao.
 
Wewe na Prof. Shivji nani ana akili kujua mikataba, Toka hapa unatupigia kelele tu.
Unatakiwa unikosoe kwa kanuni za sheria za mikataba na useme Shivji yupo sahihi kwa kanuni hizo hizo.

Kwa sababu huna ata abc za contract law, na unamwamini Shivji kwenye sheria siwezi kukulaumu kudhani yupo sahihi.

Lakini kwa anaejua contract law, Shivji ni mweupe.

Humu kuna wanasheria, mimi nimesema mara kadhaa UDSM awafundishwi ‘law of contract’ hakuna alienipinga mpaka sasa.

Unajua kwanini nimehitimisha hivyo, ukiwasikiliza arguments zao ni rahisi kubaini hawana foundation knowledge ya hayo mambo.
 
Ungetaja hivyo vifungu vinavyosema ivyo ili twende sawa.
 
Kiongozi haongozwi bali anaongoza. Ata kama kuna mashauriano, mwisho wa siku lazima aongoze kwa kuchukua maamuzi. Kabla ya kuchukua maamuzi lazima apime kila jambo aliloshauriwa na kuamua. Vinginevyo atakuwa si kiongozi anayejua anachotakiwa kufanya
 
Loh! 'Eti wataalam wa Serikali wakiwaeleza'. Serikali hii inayoshindwa kuendesha hata biashara ya genge la nyanya, eti ina wataalam wa kuwaelekeza watu.

Kwa Tanzamia, wataalam wapo kwenye sekta binafsi, siyo serikalini. Ndiyo maana baadhi ya multinational companies, ukiomba kazi halafu ukasema unafanya kazi Serikalini, inakuwa ni disqualification.
 
Tatizo kiongozi hujaelewa asietakiwa ni muarabu na sio mkataba na tena hawamtaki muarabu kwa maslah yao na sio ya taifa
Na hiyo ndio point yenye nguvu !!
 
Duh !
 
Ndio maana akatafutwa mwekezaji aende kuongeza ufanisi port.

Sasa kama unayajua yote hayo unachopinga ni nini?
 
Kwa hiyo argument yako, my learned friend, ni kuwa bila HGA hakuna IGA? Kama ni hivyo, IGA ni ya nini? Si wangeingia tu kwenye HGA baada ya MoU?
Unaweza kusema mimi sielewi legal meaning za maneno yaliyo katika IGA na hautakuwa umekosea. Lakini jopo la Tanganyika Legal Society nao hawaelewi isipokuwa legal officer wa wizarani? Na Professors Shivji na Lipumba nao hawaelewi legalese? Na Lissu na wale waliofungua kesi Mbeya, wote hawaelewi tofauti kati ya IGA na HGA? Please. Msitufanye wote wajinga. Jifunzeni kusikiliza.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…