Mmeshaambiwa zaidi ya mara mia hakuna mkataba wa kibiashara bado na ndio utakaopanga muda, lakini amtaki kusikia.
IGA ni mkataba wa mualiko kuja kuwekeza Tanzania na unao orodhesha taratibu kadhaa za kutengeneza mikataba ya kibiashara (framework).
Sasa nyie amtaki kuelewa.
Mkataba wa kibiashara lazima uwe na thamani ya kitu mnachobadilishana (consideration), lisipokuwepo hilo; hayo ni makubaliano tu mbele mahakama yoyote lakini sio mkataba wa kibiashara.
Mmeambiwa muda wa mkataba atakaopewa kuendesha bandari unategemea na thamani ya uwekezaji utakaofanywa.
Makubaliano yenyewe msingi wake ni muda wa kurudisha hela ya uwekezaji watakayo toa, kidogo kidogo kulinga na mapato ya maeneo watakayo pewa. Hayo mambo mawili ndio yatakayo amua miaka ya wao kuendesha hiyo bandari mpaka hela yao irudi.
Hayo yatapangwa watakapokutana kujadili mikataba ya concession. Hiyo IGA yenyewe inakwambia huko bado awajifika, serikali inakwambia huko bado awajifikia amtaki kuelewa. Ninyi mmekazana na vitu tu kutoka vichwani kwenu ata mueleweshwe vipi amtaki kusikia.
Dah kazi kweli kweli