Msimhukumu Rais Samia pasipokuwa na uhakika

Msimhukumu Rais Samia pasipokuwa na uhakika

Ndugu zangu mengi yameibuka tangu kusainiwa kwa mkataba wa DP World. Hii nchi haiongozwi na kiongozi mmoja. Kuna idadi kubwa sana ya viongozi kuanzia wastaafu na waliopo madarakani.

Uamuzi wa kuwakabidhi DP World hakuufanya mwenyewe, aidha alishinikizwa ama lah. Tunaweza kumnyooshea kidole kumbe wapo waliomsababishia hilo tatizo.

Nashauri badala ya kumtuhumu tumtafute na kushauriana naye pengine tutaweza kumsaidia kuondokana na kipindi hiki kigumu.
Kwahiyo akiupiga mwingi anaupiga na hao unaotaka kujifichia kwao?
 
Ndio maana serikali duniani uwa zikishatoa elimu, asietaka kuelewa awamsubiri atawakuta wenzake mbele ya safari.
Ni kweli, hata wakati wa ubinafshaji wa viwanda serikali iliamua na tukawakuta mbele tukiwa tumechoka sana. Kisha Mkapa ambaye ndio alikuwa kinara wa ule uwekezaji tena kwa jeuri, akakiri kwenye kitabu chake kuwa alifanya kosa kubwa kubinafsisha viwanda! Kibaya zaidi hakuna aliyeweza kumchukulia hatua huku tukiwa tumeumia vibaya.
 
Usichanganye mambo, shida unapenda ku complicate issues sana.

IGA imeenda bungeni ili iwe sheria, acha kufukiria vitu unavyotaka wewe.

Baada ya kuwa sheria inakuwa implied term kwenye mikataba ya utekelezaji.

Hayo mengine mnayalazimisha ndio maana mnachanganya mambo na conclusions zenu.
IGA sio sheria. Usitudanganye.

Amandla...
 
Sasa anamaana gani ya kua raisi wa nchi tena mwenye elimu ya udokta na anaitwa muheshimiwa kabisa kumbe muheshimiwa wa hovyo kama hawezi kusimamia misingi bora ya nchi anatofauti gani na baba mwenye familia asiejielewa. Kiufupi hatuna kiongozi hadi wanawake wenzake washamchoka maana wanaona wanaumia kuliko wanavyomsifia chawa wake wenyewe hawana la kusema sasa hivi

Kwanza yule ni felia elimu yake yenyewe yakuungauga kwa plasta,kaingizwa cha kike anakenua mimeno tu huku akiwapa waarabu hatmilik ya nchi,katiba ya hii nchi ya hovyo sana.
 
Mmeshaambiwa zaidi ya mara mia hakuna mkataba wa kibiashara bado na ndio utakaopanga muda, lakini amtaki kusikia.

IGA ni mkataba wa mualiko kuja kuwekeza Tanzania na unao orodhesha taratibu kadhaa za kutengeneza mikataba ya kibiashara (framework).

Sasa nyie amtaki kuelewa.

Mkataba wa kibiashara lazima uwe na thamani ya kitu mnachobadilishana (consideration), lisipokuwepo hilo; hayo ni makubaliano tu mbele mahakama yoyote lakini sio mkataba wa kibiashara.

Mmeambiwa muda wa mkataba atakaopewa kuendesha bandari unategemea na thamani ya uwekezaji utakaofanywa.

Makubaliano yenyewe msingi wake ni muda wa kurudisha hela ya uwekezaji watakayo toa, kidogo kidogo kulinga na mapato ya maeneo watakayo pewa. Hayo mambo mawili ndio yatakayo amua miaka ya wao kuendesha hiyo bandari mpaka hela yao irudi.

Hayo yatapangwa watakapokutana kujadili mikataba ya concession. Hiyo IGA yenyewe inakwambia huko bado awajifika, serikali inakwambia huko bado awajifikia amtaki kuelewa. Ninyi mmekazana na vitu tu kutoka vichwani kwenu ata mueleweshwe vipi amtaki kusikia.

Dah kazi kweli kweli
Inaonekana mkataba hujausoma au umeusoma ila hujauelewa. Unaposema mkataba hauna kipengere cha muda bali mikataba midogo ya kibiashara ndio itakuwa na muda hapo naona hujauelewa Mkataba huu. Mkataba huu ndio mama wa hiyo mikataba hiyo ya kibiashara. Huu mkataba umeshasema kabisa kuwa muda wake utaisha pale shughuli za bandari zitakapoisha sasa jiulize lini shughuli za bandari TZ sitaisha!!? Hii maana yake ni wa milele. Wanasheria wengi waliousoma wameutafasiri hivyo wakiwemo viongozi wastaafu.
 
Katika jambo la maana atakalo lifanyia Tanzania ni haya makubaliano na DPW yakitekelezwa yote phase 1 & 2, mungu awape akili tu TPA waingie concession agreement zenye maslahi ya taifa.

Watanzania mnaopinga amuoni tu picha kubwa ya huu uwekezaji kabisa.

Binafsi sio shabiki wa huyo mama kabisa, lakini kwenye ili la bandari wasirudi nyuma. Ni yale maamuzi ya watu wengi watamshukuru baadae wakishaanza kuona matokeo.

Mama asiangalie nyuma na kuwa jiwe kwenye hili; yupo sahihi 1000%.
Wakosoaji wamejikita hapa. 1. Kama jambo hili ni neema na litatuleletea faida, kwanini bandari za zanzibar hazijajumuishwa? Je, hawa wazanzibar wanaoamua kuingia mkataba na bandari za Tanganyika Je, wao hawayataki mapesa hayo kwao Zanzibar? 2. Kulikuwa na sababu gani kumpa mwarabu bandari zetu milele? Kwanini isiwe miaka kadhaa inapoisha wana-renew mkataba.
 
Ikulu sio mahali rahisi, utakuwa Raisi lakini utakuwa ukisemeshwa na viongozi wasiohesabika, huwezi kufanya uamuzi peke yako, wapo wengi watakusemesha kuanzia chama kilichokupa hicho kiti. Kumbuka chama hakina mtu mmoja, kina maelfu ya viongozi ambao lazima utawasikiliza ili wasikunyang'anye kiti. Kumbuka raisi yupo chini ya chama, anaweza kunyang'anywa madaraka na chama chake

Hivi kwa mfumo wa chama cha mapinduzi na katiba ya hii nchi,kuna mtu yuko above rais??wengi ni puppets hasa humo kwenye chama ndio vichwa maji wamejazana.
 
Wakosoaji wamejikita hapa. 1. Kama jambo hili ni neema na litatuleletea faida, kwanini bandari za zanzibar hazijajumuishwa? Je, hawa wazanzibar wanaoamua kuingia mkataba na bandari za Tanganyika Je, wao hawayataki mapesa hayo kwao Zanzibar? 2. Kulikuwa na sababu gani kumpa mwarabu bandari zetu milele? Kwanini isiwe miaka kadhaa inapoisha wana-renew mkataba.
Kwa uelewa wangu mdogo nilionao sehemu za bandari kati ya Tanzania bara na Zanzibar kwa sasa sio miongoni mwa vitu vya kimuungano.

Kama utakuwa na kumbukumbu mzuri mwezi uliopita tu katika harakati za kupunguza/kuondoa kero za Muungano bandari ilikuwa ni sehemu moja wapo iliyokuwa inatafutwa suluhu.
 
Ni kweli, hata wakati wa ubinafshaji wa viwanda serikali iliamua na tukawakuta mbele tukiwa tumechoka sana. Kisha Mkapa ambaye ndio alikuwa kinara wa ule uwekezaji tena kwa jeuri, akakiri kwenye kitabu chake kuwa alifanya kosa kubwa kubinafsisha viwanda! Kibaya zaidi hakuna aliyeweza kumchukulia hatua huku tukiwa tumeumia vibaya.
Wawekezaji wengi walioshindwa kuendeleza hivyo viwanda walikuwa wa ndani.

Ule aukuwa ubinafsishaji bali ufisadi.

Ukitaka mifano chanya angalia mabank angalia airtel. Fananisha faida zao na biashara hizo hizo zilizo chini ya serikali leo kwa asilimia 100.
 
Hivi kwa mfumo wa chama cha mapinduzi na katiba ya hii nchi,kuna mtu yuko above rais??wengi ni puppets hasa humo kwenye chama ndio vichwa maji wamejazana.
Anza kujipima ww kwanza
 
Inaonekana mkataba hujausoma au umeusoma ila hujauelewa. Unaposema mkataba hauna kipengere cha muda bali mikataba midogo ya kibiashara ndio itakuwa na muda hapo naona hujauelewa Mkataba huu. Mkataba huu ndio mama wa hiyo mikataba hiyo ya kibiashara. Huu mkataba umeshasema kabisa kuwa muda wake utaisha pale shughuli za bandari zitakapoisha sasa jiulize lini shughuli za bandari TZ sitaisha!!? Hii maana yake ni wa milele. Wanasheria wengi waliousoma wameutafasiri hivyo wakiwemo viongozi wastaafu.
Vizuri uvitaje ivyo vipengele unavyoviongelea ili twende sawa.

Maana hayo unayosema hayapo kwenye IGA.
 
Wakosoaji wamejikita hapa. 1. Kama jambo hili ni neema na litatuleletea faida, kwanini bandari za zanzibar hazijajumuishwa? Je, hawa wazanzibar wanaoamua kuingia mkataba na bandari za Tanganyika Je, wao hawayataki mapesa hayo kwao Zanzibar? 2. Kulikuwa na sababu gani kumpa mwarabu bandari zetu milele? Kwanini isiwe miaka kadhaa inapoisha wana-renew mkataba.
Swala la uendeshwaji wa bandari ni devolved matter toka mwaka 97, na Zanzibar wana mamlaka yao kuendesha bandari ambayo inasimamiwa na serikali ya mapinduzi.

Samia ni raisi wa muungano ata kama ni mzanzibari hana mamlaka ya kuwapangia Zanzibar on devolved matters; hayo ni mambo ya Mwinyi kwa sasa na baraza lake la mawaziri na bandari yao washampangisha mtu hivi tunavyoandika.

Hayo yakumpa bandari Mwarabu milele hayapo mahala popote ni upotoshaji tu, vinginevyo taja hiko kifungu.
 
Kwa hiyo Bunge walipelekewa sheria ya nchi ili waipitishe. Mimi nilidhani sheria inatokana na mapendekezo ( sio lazima yatoke serikalini) na Bungeni likiyaridhia yanapelekwa kwa Rais ili ayasaini ili yawe sheria. Kumbe Rais akisaini Mkataba unakuwa tayari sheria na Bunge wanapelekewa kutimiza wajib tu.

Kuishi sana kweli ni kujifunza. Asante kwa darsa hilo muhimu.

Amandla....
jamaa lipuudhi sana na halijielewi
Angalia vizuri utaona sign zao zimo humo upande wa pili.

Acha uongo basi ni kwamba aliyesaini hilo li IGA sio mtu wa Serikali ya Dubai wala sio mwakilishi wa Serikali ya Dubai Bali ni mtu wa DP .
Embu nionyeshe hao waliosaini upande wa Serikali ya Dubai

Angalia vizuri utaona sign zao zimo humo upande wa pili.
 
Angalia vizuri utaona sign zao zimo humo upande wa pili.

His Highness Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, huyu ndiye kiongozi wa Serikali ya Dubai.
Kwenye hilo li IGA hakuna signature yake wale power of attorney yake .
Wakati upande wetu kuna saini ya Rais na power of attorney yake ya kumuidhinisha mzanzibari mwenzake auze bandarini zetu zote

content://com.android.chrome.FileProvider/images/screenshot/1688498991925861510822.jpg
 
Nadhani umeshawai kukutana na hii phrase before ‘a contract is an agreement, but not all agreements are contracts’.

Kwanini, hapo mkataba unaozungumziwa ni commercial agreement. Ili uitwe commercial agreement (contract, kuna test zake na ya msingi ni consideration). Ambayo kwenye hiyo IGA aipo.

View attachment 2678450

Hiyo article kwanza kabisa aizungumzii IGA per se, inachozungumzia ni HGA and project activities/agreements. Kwamba wakisha ingia hiyo mikataba (commercial agreements) huko mbele ndio aiwezi vunjwa kiholela.

Kwa hivyo hiyo framework ya IGA itatumika mpaka taratibu za kuisha kwa hayo makubaliano watakayoingia kwenye commercial agreement. Kwanini hiko kipengele kimewekwa kwasababu ndani ya IGA article 20 imeelezea namna ya kutatua dispute resolution.

Sasa basi mkataba wa kibiashara (hizo agreements) watakazo ingia baadae una implied terms kadhaa ambazo ata usipoziweka kwenye hiyo mikataba zinatumika mahakamani; laws za nchi husika, precedence’s (case laws) and industry customs.
U
Hiyo IGA imepitishwa na bunge ni sheria (moja kwa moja inakuwa implied term) ata mambo yake usipoweka kwenye mikataba ya baadae wanasisitiza hiyo sheria itatumika mpaka commercial agreements zote zitakapoisha.

Na hakuna commercial agreement inakufa kishamba ata mzazi akipangisha nyumba akifa kesho, watoto awawezi kwenda kuwatoa wapangaji kiholela kabla ya muda wa mkataba kuisha ndio kinachoongelewa hapo kwenye 23 (4) sentensi ya kwanza. Na ya pili inakwambia ukitaka kufanya mabadiliko yoyote lazima ufuate taratibu walizojiwekea article 20.

Shida yenu ata abc ya contract law amna, wataalamu wa serikali wakiwaelezea amtaki mmekazana tu. Mnasoma vitu amuelewi their legal meaning nyie mnatoa tafsiri kutoka vichwani kwenu.
Wewe kweli msomi. Nakuvulia kofia.
1. Unasema kuwa paragraph ya kwanza haizumzii IGA. Hivi hiyo Agreement itakayo remain in force ni nini kama sio IGA? Hicho unakazania ni vitu vitakavyotokea ili IGA isite kuwa enforceable. Navyo ni:
1. Miradi yote iishe.
2.HGAs zote na Mikataba ya miradi iishe.
Kwisha kwa mradi mmoja au miwili na hata HGAs nyingi zikiisha ili mradi ziko ambazo ni active IGA inakuwa enforceable. Hilo la haki ya kuvunja mkataba kiholela umelitoa wapi?
2. Bado unajichanganya. Article 20 kinahusu IGA sio HGA. Na ni kimbilio pekee kama upate mmoja hautaridhika na IGA maana para 4 ya Article 23 inasema IGA haiwezi kubezwa, kuahirishwa au kuvunjwa kwa sababu yeyote ile. Wewe unatujia na mambo yako ya kufikirika ya kuvunja IGA kiholela.
3. Hii Bilateral Agreement sio mkataba wa kujenga barabara, kiwanda, kununua mafuta n.k. ndio maana sio commercial agreement. Ni mkataba wa ushirikiano baina ya mataifa mawili katika maeneo yaliyoainishwa ndani yake.
4. Mtetezi wa serikali katika masuala ya mikataba ni AG, sio wakili wa wizara. Hauoni katia pua halafu kasepa. Amewaachia nyie wanasheria uchwara na wakina Steve Nyerere kutetea kitu ambacho hakiwezi kutetewa.
Baada ya huu mjadala ndio naanza kuelewa kwa nini Law School inawafelisha kiasi kile maana hata basic reasoning hamna. Mnajiona mna uelewa zaidi ya maprofesa wenu kama wakina Shivji na former AGs kama Warioba. Mnasikitisha sana.
By the way, condition katika mkataba sio sheria. Kama hata hilo haulijui basi there is no hope for you.

Hilo jamaa Mayor Quimby ni lijinga kabisa litakuwa lilikwenda shule kusomea ujinga
 
Back
Top Bottom