Naanza kuona matunda ya Uongozi wa Eng Hersi Saidi. Alipoingia Yanga alikuta timu iko kwenye bajeti ya Bil 6. Kwa uongozi wake mathubuti jamaa ameweze kuibua vyanzo lukuki vya mapato.
Mpaka sasa Yanga ina wafadhili 9. Idadi kubwa ya independent sponsors kuliko klavu yeyote hapa Afrika Mashariki.
Kupitia hapo Yanga sasa inaweza kugenerate fund ambayo ni sawa na asilimia 70% ya thamani ya hisa za timu ya Simba SC, tena kwa msimu na wala sio lifetime.
Wakati Simba SC ikiwa na Matarajio ya Bajeti ya Tsh Bilion 13 katika msimu ujao, wenzako wameandaa Bilion 20 kama Bajeti. Hapa tunazungumzia Bilion 7 zaidi.
Yanga inaendelea kuchochora mawinguni in terms of mapato, taarifa zinaonyesha Gate collection Yanga imeongoza kwa msimu wa 3 mfululizo, kwenye upande wa sponsorship deals ndio usiseme, huko kwenye prize money ndio wameziokota vibaya mno.
Naiona Yanga SC ikifikia ndoto za kuwa Klabu ya Millenium mapema zaidi kuliko klabu yeyote ile kusini mwa Jangwa la sahara.
Shukrani ziwafikie Viongozi wote wa klabu kwa kutufikisha hatua hii ya mfano ambayo inatamaniwa na walio wenye, mmepambana kwenye kila idara kuhakikisha mambo yako perfect.
(Pichani ni Genius Eng Hersi Said)
View attachment 2668171