Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Mikoa mingi hapa nchini kwa sasa inapitia katika kipindi cha jua kali na lenye joto kali kupindukia, si usiku si mchana joto ni kali.
Bado wananchi mfumo wao wa maisha ni ule ule kutokana na wengi kutokujua umuhimu wa kunywa maji mara kwa mara hususani kipindi kama hiki.
Kipindi kama hiki watoto wadogo wamekuwa wakilia hovyo huku wazazi wengine bila kudadisi ya kuwa wana kiu kali ya maji watoto wao.
Kuna mtoto wa jirani mwenye umri wa miaka Miwili amefariki baada ya kuumwa siku chache na kuambiwa na madaktari ya kuwa alikuwa na nimonia ya joto.
Kipindi kama hiki watu waelimishwe umuhimu wa kunywa maji mara kwa mara, kwa ajili ya kulinda afya zao.