Msimu ujao 2023/2024 Simba tunahitaji sajili hizi ili tuwe imara

Ulichokieleza kinaeleweka hata kwa mimi nisiejua mpira
 
1.Djuma Shaban
2.Yanick Bangala
3.Khalid Aucho
3.Bakari Nondo Mwamnyeto
4.Jesus Moloko
5.Musonda
6.TK Master
7.Kalala Mayele, Fiston
8.Bernad Morrison
9.Stephane Aziz Ki
 
Oya pale ni anguko, wanashuka kiwango kila kukicha...msimu ujao lzm tusajili zaidi ya yanga ili tuwe bora zaidi
Simba ya Mgunda ni tofauti kabisa na Simba ya Robertinho.

Anayecheza vizuri kwenye Simba ya Robertinho ni Inonga tu. Ina maana ukimwambia Robertinho tufumie kikosi, atakwambia anawataka Kibu, Ntibazonkiza na Nyoni.

Wachezaji wengi wameshuka viwango kwa aina ya mpira wa Robertinho. Ama Robertinho si kocha sahihi au anauwezo wa kawaida sana.
 
MO nae awe tayari kutoa hela.
Yanga huwa wanajilipua ndio maana wana wachezaji wazuri.
MO ana kaubahiri fulani, anapenda cheap players.
Huwezi kumwacha Adebayo unaenda kumsajiri Okwa, halafu unataka kushindana na Mamelodi.
Nimepata za ndani kabisa, hakuna mchezaji anayekuja Simba bila idhini ya MO.

Nawapongeza sana wachezaji wa Simba wanajituma sana ingawa viwango vyao ni vya chini.
Tunashindana na wachezaji wanaosajiriwa kwa mabilioni ya pesa na mishahala ya mamilioni. Yaani mchezaji wa mshahara wa milioni kumi anacheza na mchezaji analipwa zaidi ya milioni mia kwa mwezi.

Kuna wachezaji wazuri hapa kati Kariba ya Adebayo, hawaitaji pesa ndefu sana na wanakiwango kizuri sana cha kushindania kombe la Afrika.

Lingine Simba iache kuchukua vichezaji vidogo vidogo kwa ndoto za kufanana na Luiz miquessoni.

Simba inahitaji wachezaji wenye Bodi kubwa pia. Tuachane na kuchukua vichezaji kama vitoto vya shule vikina Banda, Sackho, Okwa, nk.
 
Una dharau sana ww. Eti vichezaji kama vitoto vya shule.
 
Itakua ike yanga ya dk Mshindo Msola.
Hii yanga ya watoto wa mjini usitegemee hilo kutokea. Huoni sakata la Feisali mlivyokwaa kisiki.

Interception mmefanyiwa nyie usajili wa Aziz Ki. Na bado mtaendelea kufanyiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…