Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Hata hapa Dar es salaam, msimu wa mvua unakaribia.
Radi hapa Jijini si za kutisha , lakini tumesikia kwa mfano huko Rukwa radi imeaua karibu kila wiki.
Nyanda za Ziwa kuzunguka ziwa Victoria radi ni kitu cha kila mwaka na inaua watu wengi.
Watu wanafikiri ni uchawi lakini hewa huwa ina msuguano kutokana na mawingu yenyewe hivyo kutengeneza chembe za mawingu yanye charge hasi au chanya.
Ardhini kama kuna charge kubwa iliyo tofauti na wingu, basi umeme hutokea kuruka kama shoti ya umeme.
Hapo ndipo penye hatari maana umeme unaenda kwa kasi ya ajabu na hutafuta njia fupi zaidi.
Kama mtu amesimama ardhini na ana charge ya ardhi basi radi hukatishia kwake, na mtu huyo kuuwawa.
Tujitahidi kufanyayafuatayo kujikinga na radi:
- Tafuta mahali salama, aidha uwe ndani ya gari au nyumba kubwa
- Ondoka sehemu zozote za wazi kabisa na vilima(radi inaenda pale rahisi kabisa kufikia ardhi)
- Kama huna mahali pa kukimbilia heri kukaa chini kabisa na kutosimama, huu kichwa mtu umeinamisha
- Usikae chini ya mti mrefu na ulio peke yake(radi lazima itapiga sehemu iliyojitokeza juu)
- Ukiwa kwenye maji nenda nchi kavu, na kuondoka ufukweni haraka iwezekanavyo
Itakapokupiga huwezi kuisikia maana mwanga na umeme wa radi unaenda kwa kasi ya ajabu.
Sauti inaenda kwa kasi ndogo zaidi.
Hizi ni tips ndogo kuokoa maisha yako, pindipo mvua za radi zinayemlea eneo lako.