Msinunue Namba za magari badala ya Gari lenyewe

Huwa nawaona wajinga wanaonunua gari kwa kigezo cha Namba. Gari mashine sio Namba. Unaweza ukakuta gari ina namba ya zamani ikawa imesimama kuliko hio yenye latest plate number. Ni Ujuha tu. Nahisi haya yanasababishwa na madalali ili wamlalie mwenye chombo.
 
Kweli kabisa juzi nimekutana na Land Cruiser namba A lilikuwa jipya kabisa sijui mmiliki amelitunza namna gani
 
Na bila shaka unaiwekea zile engine oil zetu za ma trekta Sae-40/mwendo wa oil ya Tsh.28,000.
 
Na bila shaka unaiwekea zile engine oil zetu za ma trekta Sae-40/mwendo wa oil ya Tsh.28,000.
Imekuwa maarufu sana mjini...huwa naitumia kwa Carina...wajuzi wa haya mambo hebu nijuzeni ni sawa au nakosea???
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nacheka tu kama mazuri
 
Usijidanganye ukaagiza gari kupitia tradecarview.com hawa jamaa wanauza Magari kanjanja ni wachache Sana wanaobahatika kupata Magari ya ukweli
 
Fundi NOMAAA alitaka kula kote kote kwako na kwa mteja wake 😂😂😂

Nina kagari Toyota IST ambako kana namba CYZ jamaa mmoja alikuwa anakapenda haka kagari kutokana na condition yake.binafsi nlikanunua sababu ya mamsap baadaye akaja akawa anataka Crown "Toyota"...
 
Nilinunua premio old model namba B nilikagua engine na gearbox nikaona ziko Safi kabisa ila bodi ,tairi,shokapu vilikua vimechoka ..jamaa tukaingia mezani Gari akanambia anauza million tatu na laki Saba ...nikamshusha mpka 2.8 mil...tukamaliza biashara nikaenda Garage nikaiwekea mill 1.2 ...saa hvi Ni mwaka wa nne Gari Ni mwendo wa kumwaga oil kubadilisha tair, filter na oil ya gear box tu...Gari inapiga kazi balaa inaenda kokote pale ..hzi engine za haya magari Ni balaa aisee
 
Nina kagari Toyota IST ambako kana namba CYZ jamaa mmoja alikuwa anakapenda haka kagari kutokana na condition yake.binafsi nlikanunua sababu ya mamsap baadaye akaja akawa anataka Crown "Toyota"...

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] aisee nmecheka sana eti kikifurahi na kususa hahahahahah
 
Hivi kwa sasa namba za magari zimefikia D?? ipi?
Maana sisi wa kudandia boda boda na daladala hatujui kinachoendelea.

Lakini ipo siku tu.
 
Dec 31 2015 ilikuwa DFZ,

DGS itakuwa mwezi wa pili au 3 2016
mm jamaa yangu kanunua gari Mark II Oktoba 2015 JK anamkabidhi JPM
namba alipewa DAB nyie mmekimbiza mpaka DGS?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…