Msishangilie Sakata la Feitoto bali litumieni kama shule; waajili wengi hawapendi maendeleo ya wafanyakazi

Msishangilie Sakata la Feitoto bali litumieni kama shule; waajili wengi hawapendi maendeleo ya wafanyakazi

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Elimu haina mwisho!

Kila jambo halitokei pasipo sababu!
Ili kuweka misingi ya kisheria ya makubaliano yoyote huwa kuna mkataba!

Iko aina mbali mbali ya makubaliano!
Kuna ile ya kimaandishi na ile ya kimaneno! (Recorded contract)

Lakini pamoja na mambo yote mkataba huwa siyo msaafu wala bibilia kwamba hauwezi kubadilishwa.

Mwajili, taasisi au kampuni yoyote inapoona hakuna maslahi huwa inavunja mkataba na mwajiliwa yoyote kwa style mbali mbali!

Mbinu za kuvunja mkataba kwa waajili zimegawanyika katika makundi matatu!
A). Mwajili kuvunja mkataba kimkakati
B) Mwajili kuvunja mkataba kisheria
C).Mwajili kuvunja mkataba kimafia(kikatili)

Watu wengi huwa hawajui kwamba wajili wengi hutumia mbinu hizo kumfurusha mfanyakazi pale wakiona hakuna faida!
Hutumia mbinu ya kimkakati ikifeli, huangalia kama wanabajeti ya kuvunja kisheria (kulipa gharama zote), wakigundua hilo halina tija hutumia mbinu ya kiharamia (kikatili)

Mfano wa mbinu za kikatili huwa ni kumtegea mfanyakazi afanye kazi mazingira hatari, kuaandaa misheni maalum kumuua, kama kwenye site za ujenzi akizubaa mnampasua na greda chapu! Au kumpandisha gari lisilo na breki halafu dreva anaruka nakulitelekeza, sumu hata kumvamia n.k!

Hayo yote ni mbinu za kumuondoa mfanyakazi kama hakuna faida!

Waajili wengi akikuajili Leo kampuni ikiwa inaingiza 1 billion, ukapambana kuifanya iweze kuingiza 100 billion utaendelea kulipwa kama makubaliano yaliyo! Lakini kama ulikuta wanaingiza 1bilion wakafilisika basi watarudi kwako mfanyakazi kukupunguza!

Uhalisia ni UPI?

Uhalisia ni kwamba! Mwajili na mfanyakazi wanatakiwa watambuane umhimu kwa kujua kwamba huwa hakuna maisha ya marambili!

Hivyo kama kuna hasara mwajili awe na haki ya kuondoa mfanyakazi wakati wowote! Lakini Mfanyakazi naye asinyimwe fursa ya kukua au kuondoka endapo ametimiza masharti!

Kwamba hata kama mfanyakazi kasaini mkataba wa miaka 10 lakini kama kuna fursa mbele yake! Isionekane ni dhambi yeye kuvunja mkataba na kuilipa kampuni!

Inje ya hapo ni kukomoana tu pasipo sababu!
Waajili wengi hawapendi maendeleo ya wafanyakazi hata kama mfanyakazi katenda mema mengi!

Mfanyakazi anayohaki ya kuachana na kazi ikiwa tu kaona fursa au kaona kuna hatari kurndelea kukaa pale!

Sakata la FEITOO liwe shamba darasa kwa waajili na wafanyakazi kuthaminiana!

Hakuna mtu anaweza kuacha ugali bila sababu, mfano mnaweza kusema mimi nalipwa million 5 kimkataba, yes ni kweli kimkataba nalipwa lakini pesa hiyo inapitia mikononi mwa madalali waajili mi napata million moja tu!

Katika mazingira hayo siruhusiwi kutoka na endapo kama mazingira yatanishinda hawa waajili waweza hata kunijeruhi ili kunikomoa.

Kwa mazingira kama hayo ya Mimi kukosa imani hata wakisema wataniongezea mshahara nitakuwa mfanyakazi mjinga kwenda kufanya kazi katika mazingira hatari!

Msishangilie matatizo yakiwa mbali Bali yatumieni kujiimarisha kabla halijawakuta jambo!

Corona ilipo anza huko uchina! Tanzania tulikenua na kuwashangaa sana! Lakini hatukujua kuna Leo na kesho!

Sakata la FEI TOTO Liwaibue wapenda haki!
Binadamu huishi maramoja akiona fursa apewe akaitafte!

Wazawa wasaidiwe kukua na kuimarika!
Tujifunze kudanganya katika kujenga kuliko kudanganya Katika kuharibu!
Tunaweza kumuachia FEITOO kwa hekima hata kama kuna mivutano ya kisheria ili kudiscaurage wengine!

Akubaliwe kulipa hiyo hela YANGA, na mambo mengine ya faini feki kubwa za kuzugia kama zipo ili kutisha wengine!

Lakini chini ya kapeti huyu kijana asaidiwe akaendeleze kipaji chake!

Serikali ingilieni kati huyu kijana asaidiwe! Hakuna aliyemkamilifu! Hata tunaoshangilia kwamba kuvunja mkataba huenda hata uongozi tulionao tuliupata kwa rushwa!

Kama kijana huyu tunamtumia timu ya taifa, kama serikali tunamsaidiaje ili atimize ndoto zake?

Wazee wenye hekima husaidia vijana ili watimize ndoto!

FEITOO YUPO SAHIHI APEWE MSAADA!
 
Yan kwenye hili andiko ukikutana na wale bush lawyer watakuchangia buku unazidi kuwapa point. Yan unajaribu kuchanganya mambo tofauti kwenye jambo ambalo liko clear kwa maslahi yenu binafsi. Imeshaelezwa, inaelezwa na itaendelea kuelezwa Feisal ni mchezaji wa Yanga na anakiuka masharti ya mkataba kwa kutoonekana kambini. Kama kuna timu inamtaka Yanga ipo wazi na huru kumuuza.

Kama ulitaka kuongea masuala ya waajiri na waajiriwa usingeingiza swala la Feisal kwa sababu haliko kama ulivyo ainisha wewe. Kama alikua anapunjwa mshahara zipo taratibu kibao za kufuata. Hakuna huruma kwenye miakataba dogo anyooshwe mpaka aliye mpa 112M ajitokeze apeleke maombi Yanga rasmi. Huo ndio utaratibu
 
Imekuwa ndefu kweli kweli ingawa kwa mujibu wa kichwa cha habari, kuna kitu cha kujifunza .....kama ilivyo asili yangu, nitarejea kuisoma baada ya komenti za watu
 
Kwa mujibu wa kichwa cha habari (nikiwa namaana sijaisoma habari), hoja yako ina mashiko.

Hapa hauwezi kueleweka kwakua ni swala linalogusa hisia za kishabiki baina ya team mbili kubwa Tanzania.
 
Kwa mujibu wa kichwa cha habari (nikiwa namaana sijaisoma habari), hoja yako ina mashiko.

Hapa hauwezi kueleweka kwakua ni swala linalogusa hisia za kishabiki baina ya team mbili kubwa Tanzania.
Ni changomoto kubwa sana waajiliwa wanapitia sakata kama hili lilitakiwa liwaunganishe waimbe wimbo mmoja
 
It ok it ok~in piere liquid voice(mlevi wa taifa)
 
kwanini feisali haonekani kambini? kwanini kama anataka kuondoka asikae na Yanga wavunje mkataba? kwanini anaikwepa yanga? je mktaba wake umeainisha ni vitu gani vinavyoweza kuvunja mkataba? tukiacha mambo holelal holela kesho watatoka akina mayel,Morisoni,chama, n.k hili liwe funzo wamnyooshe huyu dogo
 
Kabla moto haujavuka inje huanza cheche ndani!
Sasa unataka moto urudi kuwa cheche kwasababu hukuona ili umpoteze?
Tukubali imeungua tugange yajayo
 
Kabla moto haujavuka inje huanza cheche ndani!
Sasa unataka moto urudi kuwa cheche kwasababu hukuona ili umpoteze?
Tukubali imeungua tugange yajayo
Hana namna yoyote ya kuikwepa yanga kwa sasa. Hata akaichwa Kuja kurudi tena uwanjani ni mwezi wa saba maana hakuna timu inayosajili kipindi hiki
 
Alichokifanya feisal ni either utoto ama elimu duni, ukiwa huna elimu ni rahisi sana kuhadaiwa. Niliwahi fanya kazi kwenye mazingira ya sonona sana, na mshahara kiduchu, mkataba ulikua permanent yaani mpaka miaka 60, nilitafuta kazi sehemu nyingine kimya kimya nilivyopata na kusign mkataba ndipo nikaanza kufikiria niondokaje hapa, nilienda kupata ushauri kwa watu wazoefu na walinishauri njia nzuri ambayo sikupata shida.
Kifupi dogo kazingua na acha azinguliwe na yeye poa tu.
 
Walikuacha tu ili ukapambane kwingine waliona wasikubanie!
Hakuna sababu ya kumlazimisha kwa nguvu FEI kubakia Yanga
 
Back
Top Bottom