Msitusumbue nyie si ndio mlichagua CCM kwa kishindo 2020?

Msitusumbue nyie si ndio mlichagua CCM kwa kishindo 2020?

Na Mimi leo nawapandishia bei blue wwlizokuwa wananunua 2500 nawaambia haki bei mpya Ni 4000..

Karanga walizokuwa wanunua 2000kwa kilo leo 5000 kwa kilo ...mpk maji waite mmmaaaaaaaa....tusipangiane mmeipenda wenyewe.
 
Na nyinyi ndio mkaamua kulamba asali basi ngoma droo.
 
Uko sahihi mkuu, lakini mtoa mada anamaanisha kwamba kwa nini tunafanyiwa hivyo na tunakubali? Wananchi wakiwekewa viongozi wasio wachagua wanapaswa kuwakataa kwa vitendo mpaka wajue kuwa tumekataliwa.
Lakini sie tukipewa kofia na vitenge basi ni vigelegele na shangwe huku wao wakigongeana glass za mvinyo wakisema mafala tumewaweza.
Bila kukiwasha hata kwa ngazi ya mtaaani tuu hakuna changes zozote zaidi ya kuambiwa "nendeni Burundi"

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Sio TU kofia,pia vitenge na hata wakati fululanihadi pakiti za chumvi
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Malalamiko Mara tozo Mara sijui umeme kukatika mafuta kupanda tusisumbuane.

Watanzania ndio tatizo zaidi siku za uchaguzi zikifika mnajifanya hamnazo hampigi kura na wengine mkipiga mnapigia ccm upuuzi.

Acheni kulia lia sasa haya matozo na ujinga ujinga wote unao endelea ni zao la ilani ya ccm Tatizo hatusomi ilani za vyama na kuzielewa.

Tundu Lissu kwa muda mchache wa miezi 2 aliyopiga kampeni alijaribu kutoa elimu ya uraia lakini wabongo wapi wakawa wanamtukana.

Aliyoyasema yote ndio yanayoendelea kuhusu ufisadi, mfumuko wa bei utawala wa kishikaji kutawala watu baada ya kuongoza watu.

Acha tu Mama Samia apae aende ulaya kumzika malikia kwa pesa zenu za tozo huku mikoa karibia 15 ukiwa inapishana kwa mgao wa umeme.

Hakuna update yeyote juu ya bwawa la Mwalimu nyerere.

Makamba yupoyupo tu nchi inaanguka kwenye nishati watu wapo busy na mwigulu Ila niwaambie Makamba ni tatizo kuliko Mwagulu na soon ile biashara ya Generators imeanza tena.

Ccm haijawai kuwa serious kuongoza hili taifa na Kama hamtaki iondoke msilalamike pigeni kimya.

Ongeza tozo za Gest, Condom, weka tozo kila sehemu maana sikio la kufa halisikii dawa.
Sie tulimpigia kura magufuli sio samia. Magu angekuwepo tusingelia.

We ulimuona lissu ana maana kwako na sie tuliona Magu ana maana kwetu.
 
Aliyewaweka wabunge wa CCM alitaka rasilimali za nchi ziwafaidishe wanyonge. Kilichomwondoa ndo sababu ya tozo.

Kwani hadi sasa wabunge waliopo huko bungeni si hao hao aliowaweka, mbona hawasimamii hizo raslimali zisaidie wanyonge, badala yake tozo ndio imekuwa kitanzi cha wanyonge?
 
Tozo hazitakuwa suala la serikali kuu.
Sasa hivi wanasema tozo ni kwa ajili ya kujenga shule na vituo vya afya. Katika serikali ya majimbo shule na vituo vya afya ni wajibu wa serikali za majimbo.
Kwamba kuna majimbo yatapinga tozo?
 
Uko sahihi mkuu, lakini mtoa mada anamaanisha kwamba kwa nini tunafanyiwa hivyo na tunakubali? Wananchi wakiwekewa viongozi wasio wachagua wanapaswa kuwakataa kwa vitendo mpaka wajue kuwa tumekataliwa.
Lakini sie tukipewa kofia na vitenge basi ni vigelegele na shangwe huku wao wakigongeana glass za mvinyo wakisema mafala tumewaweza.
Bila kukiwasha hata kwa ngazi ya mtaaani tuu hakuna changes zozote zaidi ya kuambiwa "nendeni Burundi"

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Kuna maneno nilitaka kuyaongeza hapo chini nikapotezea tu...

Nilitaka kuandika, CCM wana polisi, wananchi hatuna, wana maji ya kuwasha, wananchi hatuna, siku zote huwezi kwenda vitani bila silaha, lazima utapigwa.
 
Akili zikitukaa sawa kuhusu demokrasia nini tutatika hapa tulipokwama.
 
Wale wabunge wengi wa CCM kule bungeni ndio walipitisha tozo, sio watanzania, usitusingizie, na wala wale wabunge hawakuchaguliwa na watanzania, waliwekwa na aliyekuwa mwenyekiti wao.
Unataka kutuaminisha kuwa pamoja na kutochanganya betri na magunzi bado torch haziwaki?Hizo betri zitakuwa zime expire na zinavuja sumu.Maendeleo yanacheleweshwa na wapinzani!
Tudai Katiba Mpya ya Wananchi ili kujikomboa nchi yetu ya Tanganyika na Zanzibar toka mikononi mwa watawala wahuni wenye njaa ya akili na waoga wa ukweli.
 
Ni Bora Mama wa Kambo kuliko Baba wa KambošŸƒšŸƒ
 
Mara hawakuchaguliwa, Mara wamechaguliwa. Simameni upande mmoja, walichaguliwa au hawakuchaguliwa?
 
Kuna wanaccm wanalalamika sana mtaani. Nabaki nacheka tu.
Usicheke bali Tafakari kwa kina.. Huu ni wakati wa upinzani kuandaa mtu makini wa kuchukua nchi.. Hao wote wanaolalamika wapo tayari kuchagua mtu mwingine toka upinzani.. Ila kama mtaendelea kuleta wagombea mnaowataka nyie, mtaendelea kusema tumeibiwa kura..
 
Back
Top Bottom