Msitusumbue nyie si ndio mlichagua CCM kwa kishindo 2020?

Na Mimi leo nawapandishia bei blue wwlizokuwa wananunua 2500 nawaambia haki bei mpya Ni 4000..

Karanga walizokuwa wanunua 2000kwa kilo leo 5000 kwa kilo ...mpk maji waite mmmaaaaaaaa....tusipangiane mmeipenda wenyewe.
 
Na nyinyi ndio mkaamua kulamba asali basi ngoma droo.
 
Sio TU kofia,pia vitenge na hata wakati fululanihadi pakiti za chumvi
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Sie tulimpigia kura magufuli sio samia. Magu angekuwepo tusingelia.

We ulimuona lissu ana maana kwako na sie tuliona Magu ana maana kwetu.
 
Aliyewaweka wabunge wa CCM alitaka rasilimali za nchi ziwafaidishe wanyonge. Kilichomwondoa ndo sababu ya tozo.

Kwani hadi sasa wabunge waliopo huko bungeni si hao hao aliowaweka, mbona hawasimamii hizo raslimali zisaidie wanyonge, badala yake tozo ndio imekuwa kitanzi cha wanyonge?
 
Tozo hazitakuwa suala la serikali kuu.
Sasa hivi wanasema tozo ni kwa ajili ya kujenga shule na vituo vya afya. Katika serikali ya majimbo shule na vituo vya afya ni wajibu wa serikali za majimbo.
Kwamba kuna majimbo yatapinga tozo?
 
Kuna maneno nilitaka kuyaongeza hapo chini nikapotezea tu...

Nilitaka kuandika, CCM wana polisi, wananchi hatuna, wana maji ya kuwasha, wananchi hatuna, siku zote huwezi kwenda vitani bila silaha, lazima utapigwa.
 
Akili zikitukaa sawa kuhusu demokrasia nini tutatika hapa tulipokwama.
 
Wale wabunge wengi wa CCM kule bungeni ndio walipitisha tozo, sio watanzania, usitusingizie, na wala wale wabunge hawakuchaguliwa na watanzania, waliwekwa na aliyekuwa mwenyekiti wao.
Unataka kutuaminisha kuwa pamoja na kutochanganya betri na magunzi bado torch haziwaki?Hizo betri zitakuwa zime expire na zinavuja sumu.Maendeleo yanacheleweshwa na wapinzani!
Tudai Katiba Mpya ya Wananchi ili kujikomboa nchi yetu ya Tanganyika na Zanzibar toka mikononi mwa watawala wahuni wenye njaa ya akili na waoga wa ukweli.
 
Ni Bora Mama wa Kambo kuliko Baba wa Kambo🏃🏃
 
Mara hawakuchaguliwa, Mara wamechaguliwa. Simameni upande mmoja, walichaguliwa au hawakuchaguliwa?
 
Kuna wanaccm wanalalamika sana mtaani. Nabaki nacheka tu.
Usicheke bali Tafakari kwa kina.. Huu ni wakati wa upinzani kuandaa mtu makini wa kuchukua nchi.. Hao wote wanaolalamika wapo tayari kuchagua mtu mwingine toka upinzani.. Ila kama mtaendelea kuleta wagombea mnaowataka nyie, mtaendelea kusema tumeibiwa kura..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…