Msiwakatishe watoto tamaa kwa kutaka wawe kama ninyi

Msiwakatishe watoto tamaa kwa kutaka wawe kama ninyi

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Hello 👋

Wiki hii nilipeleka mtoto wangu shule uko Arusha nikiwa na rafiki yangu naye akimpeleka mwanae shule zipo tofauti ila mkoa mmoja

Baada ya kufika pale shule tukaandikisha nikaenda kumtafuta mwalimu wa darasa ni mkabidhi mtoto na nichukue ripot yake baada ya kuja kupata ripot ndio nikaona mtoto amepata 2dvn nikawa nampongeza sana sasa yule mshikaji akaanza kufoka unampongeza nini hapo wakati iyo 2 ya mwisho aliyo pata

Ikabidi na mm nifoke amejitahidi sana ana deserve kupata zawadi mimi wala sijawai fika uku so kwake kaweza lazima apate zawadi nikamgeukia mtoto nikamuuliza unataka kula nini? Akasema nikaomba kibali kwa mwalimu tukaenda fast food pale nikamwambia agiza unachotaka nitalipia

Yule mshikaji akawa anamaind kuwa naamlea mtoto vibaya af wakiume nikamulewesha kidogo akanielewa sasa alipo maliza kula nikaanza sasa kumpa no nondo Pole pole tukamludisha shule tukasepa

Shida inakuja kwa mwanae tulipo fika pale kapewa ripot mtoto nae ana 2 ila baba anataka kumkata makofi mtoto uku akisema anapoteza pesa zake nikamzuia nikamuita mtoto pembeni nikaongea nae vizuri baada ya hapo nikampa 20k nikamwambia jitahidi umefanya vyema sana tena sana mtoto akawa cool akaelewa tukamuacha shule

Hapo nani kakosea?
 
Upo sahihi
Kwaza kijana wangu ukimfokea anakuogopa then ata umuulize kitu akupi ushirikiano nimeenda nae ivyo ivyo mpaka sasa na anajua kuwa nikichukia kwahiyo mara nying anajitahidi kuepuka makosa ila makosa hayahepukiki isitoshe yupo kwenye barehe na ndio kipindi mtoto unatakiwa kuwa nae karibu sana
 
Kwaza kijana wangu ukimfokea anakuogopa then ata umuulize kitu akupi ushirikiano nimeenda nae ivyo ivyo mpaka sasa na anajua kuwa nikichukia kwahiyo mara nying anajitahidi kuepuka makosa ila makosa hayahepukiki isitoshe yupo kwenye barehe na ndio kipindi mtoto unatakiwa kuwa nae karibu sana
Kabisa tukana tukana Kila dakika humfanya mtoto awe sugu Mimi sijawahi kuwachapa watoto kwanza nawaona wadogo hawastahili adhabu mama yao ni butua mara pumbavu nyie we mbwa acha hiki acha Kile basi tafrani
 
Kbs, na unakuta Mzazi mwenyewe kwenye masomo yake alikuwa hajiwezi ni mwendo wa div 4 [emoji1787]

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
Uyo ni mimi 🤣🤣🤣🤣 kabisa ndio maana ata mtoto amateur 3 au 4 siwez foka ila huwa namwambia jitahidi usiwe wa mwisho mimi sijawai kuwa wa mwisho nilipambana nisiwe wa mwisho ila wakitaja walio faulu na mimi niwepo
 
Mkuu hii mifumo ya kikatili tuliachiwa na wakoloni wala sio asili yetu .
 
Unanikumbusha mimi nikiwa kwenye top three nafurahi mno na kumpelekea bi mkubwa ripoti

Bi mkubwa badala ya kupongeza anaanza kukandia kwa kusema "kwanini huwi wa kwanza, kwani huyo wa kwanza ana miguu minne?"
 
Back
Top Bottom