nimeona watu wengi wakitumia njia ya anonymous kupost mambo ya siri au nyeti kwenye magroup ya Facebook, wakiamini kwamba hawawezi kutambulika. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa ukweli halisi kuhusu jinsi mfumo huu unavyofanya kazi.
Kumbuka: Ingawa anonymous posts hazionyeshi jina lako kwa wanachama wengine wa kundi, admins na moderators wa group bado wanaweza kuona ni nani aliyepost. Hii ina maana kwamba hauko salama kabisa, hasa unapochapisha mambo yenye uzito kama:
- Masuala ya kisiasa
- Siri binafsi za maisha yako au ya wengine
- Matusi, kejeli
- lugha ya kuudhi Tuhuma zisizo na ushahidi
Kabla ya kuchapisha chochote anonymous, jiulize kama uko tayari kuchukua jukumu iwapo utatambulika.