Msiwe huru kupitiliza kupost "Anonymous" kwenye magroup ya facebook, Admins na Moderators bado wana uwezo wa kuwajua,

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736


nimeona watu wengi wakitumia njia ya anonymous kupost mambo ya siri au nyeti kwenye magroup ya Facebook, wakiamini kwamba hawawezi kutambulika. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa ukweli halisi kuhusu jinsi mfumo huu unavyofanya kazi.

Kumbuka: Ingawa anonymous posts hazionyeshi jina lako kwa wanachama wengine wa kundi, admins na moderators wa group bado wanaweza kuona ni nani aliyepost. Hii ina maana kwamba hauko salama kabisa, hasa unapochapisha mambo yenye uzito kama:

  • Masuala ya kisiasa
  • Siri binafsi za maisha yako au ya wengine
  • Matusi, kejeli
  • lugha ya kuudhi Tuhuma zisizo na ushahidi

Kabla ya kuchapisha chochote anonymous, jiulize kama uko tayari kuchukua jukumu iwapo utatambulika.
 

Vijana wanavyopenda kuwa Tiss .. unadhani wakifatwa watakaa kutoa taarifa?..
Mabilioni ya mama.. yakipita.😄

Basi tu Mungu awasaidie vijana
 
Asante kwa ushauri,sasa nini kifanyike kwani Tanzania yetu sote na bado wapo viumbe wana tunyamazisha usiisemee Tanzania yetu kizalendo?
 
Wao tu wanakupa hiyo notification kua admin ataona..

Hata hivyo kama ni mtu unaetumia mtandao visivyo ni lazma uchukue tahadhari zaidi ya hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…