Msoga Gang & Opposition Leaders, you guys should stop the demonization of our Late beloved President John Pombe Magufuli

Msoga Gang & Opposition Leaders, you guys should stop the demonization of our Late beloved President John Pombe Magufuli

Tulimwambia atengeneze katiba mpya yenye kumpa wananchi mamlaka zaidi kama kweli anayo uchungu na nchi lakini akasema yeye ni jiwe kwelikweli....Sasa sisi wananchi tutasemaje wakati alituacha kama alivyotukuta.
Ngoja tupambane na hali yetu...nyie ni wapambe tu kama wapambe wengine, anaewafurahisha ndo mnamshabikia ata kama hajengi misingi ya nchi kwa miaka mengine yajayo.

Sijui kwanini jamaa na uthubutu wake wote alishindwa kutengeneza strong institution??!!
 
Sijui kwanini jamaa na uthubutu wake wote alishindwa kutengeneza strong institution??!!
Alidhani atapeleka vitu kwa nguvu kama alivyokuwa anafanya na ikawa ni zaidi ya Katiba nzuri kwa nchi...umasikini wa fikra kwa nchi yetu bado ni kukwazo sana...alafu mtu kama huyo bado watu wanasema alikuwa mzalendo kwa nchi.
Alijua kabisa tatizo letu ni nini ila akaacha njia sahihi ya kutatua tatizo akakimbilia kwenye njia ya kuendeleza tatizo zaidi.
 
Huu ni mwezi wa machungu jpm wetu tarehe kama ya leo alikuwa katika hali ya maumivu. Siku tano mbele akafariki.

Wanaoenda chatle mwezi huu tujuwane tukagalagale juu ya kaburi. Mimi nishawasili chattle ardhi alozaliwa mzalendo pekee mtanzania.
 
Alidhani atapeleka vitu kwa nguvu kama alivyokuwa anafanya na ikawa ni zaidi ya Katiba nzuri kwa nchi...umasikini wa fikra kwa nchi yetu bado ni kukwazo sana...alafu mtu kama huyo bado watu wanasema alikuwa mzalendo kwa nchi.
Alijua kabisa tatizo letu ni nini ila akaacha njia sahihi ya kutatua tatizo akakimbilia kwenye njia ya kuendeleza tatizo zaidi.
Ata sasa bado kuna wajinga wanafikiri nchi itaendelea bila kua na miongozo na taasisi imara.
 
Hereby declare my interest , Mimi ni Muumini wa Damu kabisa wa Magufulification of Tanzania !!.

JPM was a kind of President tulomuhitaji Kwa miaka mingi , he was a Man of his words, a Man who made things happen .

Lets speak the truth ,Tanzania's current economic shambles , Social ,Cultural and political calamities are largely due to leadership failure by past governments.

Nani Asiyejua kua Mtangulizi wake ndio alovuta Mpunga na mikataba ambayo Leo hii imetuletea Ushoga?.

Nani asojua Ufisadi mkubwa mkubwa wakutisha ulofanywa na huyu Mtangulizi wake ??.

Kuna Kipindi kilichokua na Ufisadi, wizi, umasikin mkubwa, Wapinzani mpaka Viongozi wa Dini kula Rushwa waziwazi kama ilivyokua Kwa Uongozi wa Mtangulizi wake ??.

Nani Asiyejua JPM Alikuja kua Mkombozi aliyekinusuru Chama Cha Mapinduzi na kukifichia aibu Machoni mwa Watanzania ??.

Nani Asiyejua kua JPM alirithi Nchi iloharibika kwelikweli, huku hazina kukiwa hamna Kila kitu??.

Nani Asiyejua JPM alirithi Nchi ambayo watumishi wa Umma, hawakua na Tena na Maadili, nidhamu , na walijawa madharau?.

Nani Asiyejua kua JPM alirithi Nchi ambayo haikua na strategical projects yoyote ?

Nani Asojua JPM alirithi Nchi ambayo ilijawa Rushwa, Masikin akazidi kua Masikin, Huku wachache wakuendelea kujikimbikizia Mali na watoto wao??.

Late President JPM should not be demonized and we as Tanzanians na vile mnatuita ( Sukuma Gang ) we shall stand by to condemn any humiliation and any bad mouthing directed against our Late beloved Magufuli .

Watanzania ni lazima tusimame nyuma ya Misingi aloiacha HAYATI JPM Kuhakikisha kwamba Serikali hii iliorithi mikoba yake inatafuta appropriate solutions to the country's problems na Serikali inawajibika kama ilivyokua Kwa JPM... JPM alitatua Tatizo hapohapo, yalohitaji muda aliyapa muda.

JPM alisema, Naondoka ila nitarudi mwezi wa Saba, nikija nikute pamekamilika, na kweli Mwezi wa Saba alirudi, naole wako akute Maneno na sio kazi ilokwisha ... Utamjua !!!!!

Leo Nchi imerudi hatua za miaka kumi nyuma, mtu anaboronga anahamishwa, watu wanakula Pesa tu za Nchi, Nchi Haina hata bei elekezi,. sahizi watuingizia ma Michele na ma vyakula ya GMO , hayapimwi Wala nn !!.

Taasisi nyingi zimelala, watu wamelala, wakiamka ni kupiga Hela , Kila Mahali ni vilio, Viongozi vilio, Wananchi vilio,... Hivi hii Nchi ya wapi?? Tunaenda wapi kama Nchi??.

Tanzania Must move forward and this requires All people in this country to support the Legacy left by Late JPM.

Mtu anapofurahia Kifo Cha JPM ,Mbaba alojitoa Maisha yake, Baba aloamua kutufanya tuamini nasisi Watanzania tunaweza is just unpatriotic, disingenuous and intellectually dishonest.

Kiongozi wa Nchi unajinadi Et "Hata Mimi sipendi kutengua , kuntengua mtu ni fedheha'.... Kweli ??? Unawaambia nn?.

Unatafuta kupendwa ?.... Ndio imefikia hatua unawaruhusu wale Kwa Kamba zao?? Hatima Kila kukicha wanagombaniana Kupiga Hela za Wananchi, Miradi inasimama, alionekana Mmoja hapendi Rushwa, mnamuwashia moto, Mara vile Mara hivi.... Kama Taifa tunaenda wapi?? .


I want you ( Msoga and the Fake opposition leaders ) to know that , the lies and malicious propaganda peddled against our Late Beloved President JPM will not work anywhere in Country, will not work anywhere and this is simply because Tanzanians knows their real enemy!!.

Magufulinists
believes in Peace, development and well being of Tanzania na hivo mashetani wote mnaofanya Siasa za Kumchafua Hayati JPM na kuwagawa Watanzania on the basis of tribal and regional politics ,muache Mara Moja.

MUWENI na Aibu hata kidogo, mtalaaniwa na VIZAZI vyenu, Mambo makubwa alitufanyia Huyu Mjoli wa Mungu JPM Kwa miaka yake mitano ,tulipaswa hata TUMJENGEE SANAMU. ( Kwa kuhesabu Mazuri makubwa aloyafanya ,siwezi kuyamaliza )

Maajabu Sasa kila kukicha mnapamba na kufuta popote ambapo kuna chembechembe za Magufuli..

Na nyie Vyombo vya Dola,, nyote ni mashaidi na wenye macho kwa Mchango wa miaka mitano ya JPM katika Nchi hii, inakuaje mnachekacheka na Hawa wahuni ??.Wahuni ambao mashariti ya zile 4R zao, ni Kumchafua JPM na Kumsifia Aliyopo ?. Kwann mnaacha haya ?.

NDUGU ZANGU WATANZANIA FAHAMUNI, HATUNA WAPINZANI, TUNA KIKUNDI CHA WAHUNI AMBAO WANAPAMBANIA

👉 MATUMBO YAO

👉 PESA ZA WAZUNGU

👉USHOGA ILI TAIFA LILAANIWE , NA HUU USHOGA UNAONGOZWA KUPAMBANIWA WAPINZANI HUKU UKIFUMBIWA MACHO NA UONGOZI ULIPO.

RAI YANGU , WATANZANIA MSIKAE KIMYA, AMKENI SEMEI, PINGENI, HUKU MKIMWOMBA MUNGU AINGILIE KATI ... NAJUA UONGOZI WA SASA, UMEAMUA KUTUTOA KWA MUNGU, KWA SASA HAMNA YALE MAOMBI MAKUBWA YA KITAIFA ALOANZISHA JPM , NAJUA NI MAKUSUDI TU WANAFANYA, ILA NI MUNGU ALOTUPISHA KWENYE COVID-19, MUNGU ALOTUPUNGUZIA AJALI, MUNGU ALOTUEPUSHIA KUSHUKA KWA UCHUMI ,MUNGU ALOTUPA JPM ALOTUIMIZA TIFANYE KAZI KWA BIDII , NA HIVO BASI SISI KAMA WANANCHI, TUSIACHE KUMWAMBIA MUNGU AFANYE JAMBO, TUOMBEE VYOMBA VYA DOLA, MUNGU AVIPE WELEDI, ILI BADALA YA KUENDELEA KUSIMAMIA MTU NA KIKUNDI, WASIMAMIE MASUALA MAPANA YENYE MASILAHI YA NCHI !!.

I cannot believe what you wrote because i personally experienced what Magufuli with his friends and relatives did to me and family stay tuned there’s a lot of lawsuits coming for Tanzania and these happened with Magufuli orders so to quote James Baldwin: I can’t hear what you say because i can see what you are doing. Also Abe Lincoln said you can fool some people for some time but you can fool all the people all the time.
 
Mimi nilikua simpendi jpm lakini Kwa haya yanayoendelea nimegundua kumbe hata wapinzani ni matapeli tu ndio maana alifutilia mbali haiwezekani wapinzani hawaoni kosa lolote kwenye utawala huu ni ajabu kweli
Siasa ni Sayansi ya hali ya juu sana

Makundi ndani ya Chama yana matawi yao ambayo ndio vyama shikizi

mnyukano wa 2005-2015 ilibidi itengenezwe cinema ya Ufisadi wakapewa hiyo kashfa na jina la Mhusika, kazi ikafanywa kwa ustadi Mkubwa, alipokatwa Mhusika 2015 Watu wake wa karibu wakataka kupasua Chama, wakala aliekuwa anajifanya mtu wake wa karibu akamshauri tuachane na kupasua Chama, jamaa wa upande wa pili wametuita twende zetu…Cinema ikaisha kama ilivyoisha

sasa hivi kuna Mnyukano mwingine mkali sana makatili vs wahuni …ikashauriwa tufungue milango 'hewa iingie ndani kupunguza joto ' ila wale Jamaa zetu tuwape tena jina la ku deal nao na kweli kazi imeanza vyema na 'marehemu baba' anasemwa vya kutosha
 
Uchaguzi wa 2020 ulizidi kuonesha picha halisi ya yule jamaa. No aibu when it came to uchaguzi.
 
Umeandika ushuzi mtupu. Nyie Sukuma Gang bora mkakaa kimya. JPM aliamua mwenyewe kufunika mema yake kwa kufanya maovu yaliyomchafua. Ule ukatili wake haukuwahi kuonekana tangu nchi ipate Uhuru. Alitakiwa aongoze miaka ile ya 60 au 70 ambapo wasomi walikuwa wachache. Tunamshukuru Mungu kwa kumuondoa mapema kwasababu alikuwa na nia ovu ya kujiongezea muda wa kutawala.
 
Jpm alionyesha nini maana ya kiongozi wa nchi anapaswa kuwa,hususani suala la maendeleo kwa wananchi.
Maendeleo kwa kuwafunga watu midomo? Maendeleo gani kama nchi nzima anahakikisha Upinzani haufurukuti...?

Maendeleo gani kwa kununua wapinzani?

Maendeleo gani kwa kuzuia watu wasiajiriwe?

Maendeleo gani kwa kuwaibia watu hela mfano beural de change?
 
TUOMBEE VYOMBA VYA DOLA, MUNGU AVIPE WELEDI, ILI BADALA YA KUENDELEA KUSIMAMIA MTU NA KIKUNDI, WASIMAMIE MASUALA MAPANA YENYE MASILAHI YA NCHI !!.
Vyombo vya dola kwa sehemu kubwa vimekubali kuwa "chawa" wa viongozi na wala siyo vyombo vya kusimamia maslahi mapana ya nchi na raia wake. Kiukweli hata mimi naumia sana kila nikiona mambo yanavyoenda katika nchi yetu. Lakini nina amini, wako wachache wanaoipenda nchi yetu, na wala hawataendelea kuruhusu hali hii iendelee milele! Nashukuru na wewe mleta uzi ni miongoni mwao. Sisi tutaendelea kusema ili walau wajue kwamba wanatuumiza wananchi wanyonge wa nchi hii. Wakitufunga sawa, wakituua pia ni sawa lakini maneno yetu hayawezi kufungwa wala kuuliwa! Yataendelea kubaki Siku zote.
 
Ni kwel he is gone but still alive in majorities
Ukifa umekufa boss. Kinachobaki ni kumbukumbu ambazo nazo baada ya muda zitafutika. Kwa alichokiacha JPM duniani, kumbukumbu zake zikijitahidi sana ni miaka 100. Zaidi ya hapo ni mpaka atakayetaka azitafute kwenye historia ya maraisi wa Tanzania. Watu wasio maraisi kama mm huenda na wewe labda ujenge shule au taasisi ndo kumbukumbu zako zitatoboa angalau 50 yrs
 
Maendeleo kwa kuwafunga watu midomo? Maendeleo gani kama nchi nzima anahakikisha Upinzani haufurukuti...?

Maendeleo gani kwa kununua wapinzani?

Maendeleo gani kwa kuzuia watu wasiajiriwe?

Maendeleo gani kwa kuwaibia watu hela mfano beural de change?
Demokrasia tunayoitaka siyo hii tuliyo nayo.
JPM alikuwa sahihi kabisa.
Bora kuumiza wachache kwa maslahi ya wengi, kuliko kuumiza wengi kwa maslahi ya wachache. Hiyo ndiyo Demokrasia tunayoitaka sisi.
Angalia wenzetu wa Rwanda, nenda pale Uganda pia kwa Museven, hiyo ndo aina ya Demokrasia inayohitajika hapa kwetu pia..
 
Ukifa umekufa boss. Kinachobaki ni kumbukumbu ambazo nazo baada ya muda zitafutika. Kwa alichokiacha JPM duniani, kumbukumbu zake zikijitahidi sana ni miaka 100. Zaidi ya hapo ni mpaka atakayetaka azitafute kwenye historia ya maraisi wa Tanzania. Watu wasio maraisi kama mm huenda na wewe labda ujenge shule au taasisi ndo kumbukumbu zako zitatoboa angalau 50 yrs
Kwa aliyoyafanya JPM, kumbukumbu zake zitabaki milele. Hata wajukuu wa wajukuu wetu, watazikuta.
 
Kwa aliyoyafanya JPM, kumbukumbu zake zitabaki milele. Hata wajukuu wa wajukuu wetu, watazikuta.
MILELE?

Ndege? Zitakuwepo? Madaraja? Yatakuwa bado ni hayo hayo au watayavunja yaboreshwe? Reli? Wakoloni waliacha mangapi ambayo mpaka sasa yapo na hukumbuki kiongozi wake? Unakumbuka jina la mkoloni aliyetuongoza kujenga reli? Hapo ni miaka 60's tu. Sasa MILELE unayoisema wewe umejaribu kufikiri itafananaje?

Dunia haina huruma kwa marehemu, ni wachache sana wanaofanya vitu extraordinary mno ndo kumbukumbu zao huishi vizazi na vizazi. Embu fikiria walioacha pyramids. Unawafahamu?
 
Demokrasia tunayoitaka siyo hii tuliyo nayo.
JPM alikuwa sahihi kabisa.
Bora kuumiza wachache kwa maslahi ya wengi, kuliko kuumiza wengi kwa maslahi ya wachache. Hiyo ndiyo Demokrasia tunayoitaka sisi.
Angalia wenzetu wa Rwanda, nenda pale Uganda pia kwa Museven, hiyo ndo aina ya Demokrasia inayohitajika hapa kwetu pia..
Museven angalau anatumia akili...

JPM alikuwa anaiga Kagame kuhakikisha Upinzani ni kushinda Polisi au Risasi..

JPM hakupenda kuambiwa ukweli.. Yeye aliendesha nchi kwa jinsi alivyoamka siku hiyo...
Kamwe hakuwa sahihi
 
Back
Top Bottom