Msoga Gang & Opposition Leaders, you guys should stop the demonization of our Late beloved President John Pombe Magufuli


Sijui kwanini jamaa na uthubutu wake wote alishindwa kutengeneza strong institution??!!
 
Sijui kwanini jamaa na uthubutu wake wote alishindwa kutengeneza strong institution??!!
Alidhani atapeleka vitu kwa nguvu kama alivyokuwa anafanya na ikawa ni zaidi ya Katiba nzuri kwa nchi...umasikini wa fikra kwa nchi yetu bado ni kukwazo sana...alafu mtu kama huyo bado watu wanasema alikuwa mzalendo kwa nchi.
Alijua kabisa tatizo letu ni nini ila akaacha njia sahihi ya kutatua tatizo akakimbilia kwenye njia ya kuendeleza tatizo zaidi.
 
Huu ni mwezi wa machungu jpm wetu tarehe kama ya leo alikuwa katika hali ya maumivu. Siku tano mbele akafariki.

Wanaoenda chatle mwezi huu tujuwane tukagalagale juu ya kaburi. Mimi nishawasili chattle ardhi alozaliwa mzalendo pekee mtanzania.
 
Ata sasa bado kuna wajinga wanafikiri nchi itaendelea bila kua na miongozo na taasisi imara.
 
I cannot believe what you wrote because i personally experienced what Magufuli with his friends and relatives did to me and family stay tuned there’s a lot of lawsuits coming for Tanzania and these happened with Magufuli orders so to quote James Baldwin: I can’t hear what you say because i can see what you are doing. Also Abe Lincoln said you can fool some people for some time but you can fool all the people all the time.
 
Mimi nilikua simpendi jpm lakini Kwa haya yanayoendelea nimegundua kumbe hata wapinzani ni matapeli tu ndio maana alifutilia mbali haiwezekani wapinzani hawaoni kosa lolote kwenye utawala huu ni ajabu kweli
Siasa ni Sayansi ya hali ya juu sana

Makundi ndani ya Chama yana matawi yao ambayo ndio vyama shikizi

mnyukano wa 2005-2015 ilibidi itengenezwe cinema ya Ufisadi wakapewa hiyo kashfa na jina la Mhusika, kazi ikafanywa kwa ustadi Mkubwa, alipokatwa Mhusika 2015 Watu wake wa karibu wakataka kupasua Chama, wakala aliekuwa anajifanya mtu wake wa karibu akamshauri tuachane na kupasua Chama, jamaa wa upande wa pili wametuita twende zetu…Cinema ikaisha kama ilivyoisha

sasa hivi kuna Mnyukano mwingine mkali sana makatili vs wahuni …ikashauriwa tufungue milango 'hewa iingie ndani kupunguza joto ' ila wale Jamaa zetu tuwape tena jina la ku deal nao na kweli kazi imeanza vyema na 'marehemu baba' anasemwa vya kutosha
 
Uchaguzi wa 2020 ulizidi kuonesha picha halisi ya yule jamaa. No aibu when it came to uchaguzi.
 
Umeandika ushuzi mtupu. Nyie Sukuma Gang bora mkakaa kimya. JPM aliamua mwenyewe kufunika mema yake kwa kufanya maovu yaliyomchafua. Ule ukatili wake haukuwahi kuonekana tangu nchi ipate Uhuru. Alitakiwa aongoze miaka ile ya 60 au 70 ambapo wasomi walikuwa wachache. Tunamshukuru Mungu kwa kumuondoa mapema kwasababu alikuwa na nia ovu ya kujiongezea muda wa kutawala.
 
Jpm alionyesha nini maana ya kiongozi wa nchi anapaswa kuwa,hususani suala la maendeleo kwa wananchi.
Maendeleo kwa kuwafunga watu midomo? Maendeleo gani kama nchi nzima anahakikisha Upinzani haufurukuti...?

Maendeleo gani kwa kununua wapinzani?

Maendeleo gani kwa kuzuia watu wasiajiriwe?

Maendeleo gani kwa kuwaibia watu hela mfano beural de change?
 
TUOMBEE VYOMBA VYA DOLA, MUNGU AVIPE WELEDI, ILI BADALA YA KUENDELEA KUSIMAMIA MTU NA KIKUNDI, WASIMAMIE MASUALA MAPANA YENYE MASILAHI YA NCHI !!.
Vyombo vya dola kwa sehemu kubwa vimekubali kuwa "chawa" wa viongozi na wala siyo vyombo vya kusimamia maslahi mapana ya nchi na raia wake. Kiukweli hata mimi naumia sana kila nikiona mambo yanavyoenda katika nchi yetu. Lakini nina amini, wako wachache wanaoipenda nchi yetu, na wala hawataendelea kuruhusu hali hii iendelee milele! Nashukuru na wewe mleta uzi ni miongoni mwao. Sisi tutaendelea kusema ili walau wajue kwamba wanatuumiza wananchi wanyonge wa nchi hii. Wakitufunga sawa, wakituua pia ni sawa lakini maneno yetu hayawezi kufungwa wala kuuliwa! Yataendelea kubaki Siku zote.
 
Ni kwel he is gone but still alive in majorities
Ukifa umekufa boss. Kinachobaki ni kumbukumbu ambazo nazo baada ya muda zitafutika. Kwa alichokiacha JPM duniani, kumbukumbu zake zikijitahidi sana ni miaka 100. Zaidi ya hapo ni mpaka atakayetaka azitafute kwenye historia ya maraisi wa Tanzania. Watu wasio maraisi kama mm huenda na wewe labda ujenge shule au taasisi ndo kumbukumbu zako zitatoboa angalau 50 yrs
 
Demokrasia tunayoitaka siyo hii tuliyo nayo.
JPM alikuwa sahihi kabisa.
Bora kuumiza wachache kwa maslahi ya wengi, kuliko kuumiza wengi kwa maslahi ya wachache. Hiyo ndiyo Demokrasia tunayoitaka sisi.
Angalia wenzetu wa Rwanda, nenda pale Uganda pia kwa Museven, hiyo ndo aina ya Demokrasia inayohitajika hapa kwetu pia..
 
Kwa aliyoyafanya JPM, kumbukumbu zake zitabaki milele. Hata wajukuu wa wajukuu wetu, watazikuta.
 
Kwa aliyoyafanya JPM, kumbukumbu zake zitabaki milele. Hata wajukuu wa wajukuu wetu, watazikuta.
MILELE?

Ndege? Zitakuwepo? Madaraja? Yatakuwa bado ni hayo hayo au watayavunja yaboreshwe? Reli? Wakoloni waliacha mangapi ambayo mpaka sasa yapo na hukumbuki kiongozi wake? Unakumbuka jina la mkoloni aliyetuongoza kujenga reli? Hapo ni miaka 60's tu. Sasa MILELE unayoisema wewe umejaribu kufikiri itafananaje?

Dunia haina huruma kwa marehemu, ni wachache sana wanaofanya vitu extraordinary mno ndo kumbukumbu zao huishi vizazi na vizazi. Embu fikiria walioacha pyramids. Unawafahamu?
 
Museven angalau anatumia akili...

JPM alikuwa anaiga Kagame kuhakikisha Upinzani ni kushinda Polisi au Risasi..

JPM hakupenda kuambiwa ukweli.. Yeye aliendesha nchi kwa jinsi alivyoamka siku hiyo...
Kamwe hakuwa sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…